Fungua

/PCCTP/news: Kiswahili: WI8D5l7qsDAt7GmNX5muq9M9:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiingereza) Kiswahili

Wafanya kazi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB wametakiwa kuendeleza mshikamano na umoja miongoni mwa sambamba na kuongeza juhudi katika kazi ili kuongeza tija na kuiwezesha bodi ya Utalii kuendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika tafjia fupi ya kupongezana iliyofanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa Mikocheni Resort Center ulioko mikocheni jijini Dar es salaa Sambamba na hayo  amewataka  wafanyakazi kuendelea pia kufanya kazi kwa nidhamu jambo ambalo amesema litasaidia kudumisha taswira nzuri ya Bodi ya Utalii kwa jamii.

Katika tafrija hiyo iliyohudhuriwa pia na wafanyakazi kutoka matawi mengine ya mikoani bibi Devota Mdachi pia aliwatambulisha rasmi wafanyakazi bora wa shirika mwaka huu ambao ni Bw. Rossamu Mduma ambaye ni mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na  Ester Solomoni wa Tawi la Bodi ya Utalii Arusha.  Tafrija hiyo ilinogeshwa vilivyo na muziki wa dansi uliokuwa ukiporomoshwa na bendi ya Utalii (Utalii Band).

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe