Envaya

/TEYODEN/post/115498: Kinyarwanda: WIVktwipSX7RNEoekdCjStU6:content

Base (Igiswayire) Kinyarwanda

TEYODEN YATOA MILINI SITA(6) KUSAIDIA VIKUNDI VYA WASICHANA WALIOJIFUNGUA KATIKA UMRI MDOGO.

Wasichana waliojifungua katika umri mdogo sasa wamepata fursa ya aina yake baada ya kukabidhiwa cheki zenye thamani ya milioni 2 kwa kila kikundi.

Akikabidhi cheki hizo mkuu wa wilaya ya Temeke katika ukumbi wa Amka youth aliwataka wasichana hao kuwa makini na pesa hizo na kwamba zitumike kwa miradi iliyokusudiwa ili kuwaletea tija katika maisha yao.katika risala yake mkuu wa wilaya ya Temeke aligusia pia suala la vijana kuwa na miradi ya kudumu ya kiuchumi na hasa masuala ya kilimo.Aliwataka vijana kutozarau kilimo na sio tu kilimo cha shambani kwa jembe la mkono lakiniĀ  kilimo cha kisasa ambacho kinatumia mbinu za kitaalam.Alisisitiza kilimo mfano cha nyanya ni sehemu ndogo tu ya ardhi inaweza kutumika na ikazalisha nyanya nyingi.Hivyo vijana hao wa kike wakaweza kujiajiri wenyewe.

Katika risala yao kupitia mwakilishi wao Zakia wasichana hao waliojifungua kabla ya umri walimuomba mgeni rasmi kuwa mlezi wa vikundi hivyo.Pia waliiitaka jamii kuwaangalia wasichana wenye umri wao kwa umakini wasije kutumbukia katika matatizo kama yao na kuwaweka katika changamoto za kimaisha kama wanazozipata wao.

Mradi huu umefadhiliwa na Population Council, unasimamiwa naTAMASHA na unatekelezwa na TEYODEN.

(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe