Base (Swahili) | English |
---|---|
Wanachama wa MTWANGONET walio katika mradi wa Ukimwi na Jinsia wapo MASASI wakihudhulia mafunzo ya siku sita ya Uendeshaji wa Shirika(Organizational Deveopment Training) Mafunzo hayo yanalenga kuboresha utunzaji mzuri wa kumbukumbu za shughuli na miradi, upangaji mipango na utunzaji wa kumbukumbu za Fedha ili waweze kutekeleza mradi huu wa utetezi maswala ya Ukimwi na Jinsia lakini pia miradi mingine ambayo wataitekeleza. Akihojiwa na Afisa habari wa Mtwangonet Mwanyekiti wa Mtwangonet Bw. Saidi Ally Nassoro amewashukuru sana GIZ kwa kuwezesha wanachama wa Mtwangonet katika mradi huu pia yeye mwenyewe kama mshiriki wa Mafunzo hayo amesema kwa kweli mafunzo haya ni muhimu sana kwa Asasi zetu ili ziweze kusimama zenyewe "Mafunzo ni mazuri na wawezeshaji ni wazuri pia nawasisitiza viongozi wote wa Asasi zilizo katika Mradi huu zizingatie fursa hii Adimu" Alisisitiza Bw. Nassoro. Mafunzo haya yanaendelea katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Masasi Mjini mkoa wa MTWARA, TANZANIA. |
Members of MTWANGONET those in the AIDS and Gender Project Iqaluit they are training six days hudhulia Management Corporation (Deveopment Organizational Training) The training focused on improving the proper handling of records of activities and projects, planning and maintenance of financial records in order to implement the project's advocacy of AIDS and gender issues but also other projects which will be fulfilled. Interviewed by the official news of the Mtwangonet Mtwangonet Mwanyekiti Mr. Saidi Ally Nassoro has thanked very GIZ to enable members of Mtwangonet in this project also himself as a member of the training was said in fact this training is very important for the organization of our order to be able to stand up for themselves "Training is good and the trainers are nice too nawasisitiza officials of Organizations that are in the project comply with this rare opportunity, "He insisted Mr. Nassoro. Studies are continuing in the Catholic Church Forum of Urban Masasi in Mtwara Region, Tanzania. |
Translation History
|