Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
MRADI WA UTAWALA BORA NA HAKI ZA KIRAIA UNAENDESHWA NA ASASI YA CHAMAKIVU KWA UFADHILI WA THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIATY FCS. 3.0 HISTORIA YA MRADI HUU. Mradi huu unajulikana kama mradi wa Utawala bora katika awamu hii ya kwanza mradi umewafikia watu 370 toka Kata tatu za Vuga,Usambara na Mponde za Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga, Mahitaji ya mradi huu yametokana na Ufahamu mdogo wa sera na mipango mbalimbali katika ngazi ya Vijiji ambapo kunasababisha maendeleo ya Vijiji kuwa duni ukizingatia Vijijini ndio sehemu kubwa ya kudhalisha, Katika maeneo mengi ya Tanzania mwamko wa wananchi kufahamu sera na kushiriki katika shughuli za maendeleo na kudai mapato na matumizi ya Kijiji ni jambo lililopo kwa kiwango kidogo sana , na hivyo kusababisha kuwapa mianya viongozi wasiokuwa waadilifu kutumia nafasi hiyo kufanya wanavyotaka na kusababisha umaskini kuzidi kukithiri, Wananchi wengi wanalalamikia serikali za Mitaa/Vijiji kutokana na wao ndio wanaokusanya mapato kwa njia ya kodi,leseni,ada na vyanzo mbalimbali vya mapato,kwa hiyo ufatiliaji wa mapato hayo ni muhimu ili Serikali za Mitaa/Vijiji walete ushawishi kwa umma kuwa mapato hayo yamepokelewa kwa kufuata sheria na kutumiwa ipasavyo kwa matumizi yalokusudiwa Katika eneo la mradi (Kata sita za Wilaya ya Lushoto Halmashauri ya Bumbuli) Hakujawahi kufanyika mafunzo/matamasha yanayohusisha uhamasishaji na uelimishaji wa jamii juu ya utawala bora na haki za kiraia, licha ya kuwa kunapengo kubwa sana kwa wanajamii hao juu ya ufahamu wao kuhusiana na dhana ya utawala bora na haki za kiraia. katika kufahamu hali ya eneo la mradi CHAMAKIVU iliandaa Utafiti mdogo ambao ulituwezesha kufahamu kuwa uwelewa wa wakazi wa maeneo hayo ni mdogosana Watu wachache waliohojiwa ( 100 ) katiyaoni asilimia 12% ndo waliofahamu dhana ya utawala bora na ;-
Katika kuchochea maendeleo katika eneo la mradi CHAMAKIVU imepanga kuongeza asilimia kumi kwa kila eneo kutokana na uhamasishaji na uelimishaji utakaoendeshwa na mradi huu
4.0 MALENGO YA MAFUNZO
6. Kuwawezesha wananchi kufahamu umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo zakujitolea
5.0 SHUGHULI ZILIZOFANYWA KATIKA MRADI HUU 1) Kutoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Vijiji/Kata wadau wa maendeleo na wananchi juu ya masuala ya utawala bora na uwajibikaji, Jumla ya viongozi wa Kata, Vijiji/Vitongoji na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji 190 na wananchi 180 waliudhuria katika mafunzo ya utawala bora ngazi ya Kaya, Wanawake 200 na wanaume 170 jumla 370, Wananchi waliweza kutoa kero zao zinazowasumbua Kero ni:- v Viongzozi kutotimiza wajibu wao wa utoaji wa huduma za kijamii na badala yake kuwepo na michango mingi v Kutotekeleza mipango iliyopangwa na wananchi v Wananchi kuletewa miradi tofauti na mahitaji yao v Viongozi kutumia siasa vibaya v Viongozi kuwa bize katika vikao vya Halmashauri kuliko kuhudumia wananchi katika ngazi ya kijiji na Kata v Wataalamu na viongozi kuingiliana majukumu v Viongozi kuwa wakali sana kwa watu kwa kutoa amri badala ya kutushirikisha na kutuelemisha kwanza v Wamekuwa watu wa kutoa maamuzi v Viongozi wa kike kunyanyaswa kutokana na jinsia yao v Kiongozi kuweka ofisi nyumbani kwake badala ya jengo la serikali v Viongozi wamekata taamaa ya kuwahudumia wananchi na badala yake wamekuwa wakisubili miradi kutoka Halmashauri v Mafunzo yanapotokea wanaopelekwa hawaludishi mrejesho kwa wanakijiji v Sheria nyingi ndogo ndogo zimekuwazikitungwa na Halmashauri lakini jamii hawazifahamu sheria hizo na hivyo utekelezaji wake unakuwa mgumu na kusababisha malumbano kati ya viongozi na wananchi.
Kero za viongozi;-
Mada ni :-
Mwezeshaji alitoa vichangamsho washiriki waliimba na kucheza na kuwafanya wachangamke kila mara na kuwa tayari kwa ajiri ya kupokea masomo mwezeshaji aliweza kueleza mambo mbalimbali katika uongozi stadi za uongozi
Muezeshaji aliwasilisha mada yake iliyojikita kwenye ufahamu wa jinsi ya kufanya uchambuzi katika uongozi aligawa makundi na kila kundi alilitaka kuleta majukumu yake akiwa yeye ndio kiongozi a) Watenda wa Vijiji /Kata na Madiwani 1 Kushirikisha/mshirikishaji 2 Ushawishi 3 Mbunifu 4 Mwenye maono 5 Mwenye kutoa motisha 6 Mwenyekugawa majukumu 7 mwenye kuwa na mpango kazi wa muda mrefu na mfupi 8 Mfuatiliaji na mwenye kutathimini b) Kuorodhesha majukumu kama kiongozi wa kijamii 1 kufuatilia huduma za kijamii 2 kufanya utafiti wa mahitaji katika jamii 3 kuweka kumbukumbu 4 kutoa mrejesho c) viongozi wa dini taasisi, maimamu na maskofu 1 kulea waumini kiroho na kimwili 2 kuwahimiza waumini kuwa na maadili mema 3 kulinda na kutetea maslahi ya waumini Viongozi wa elimu maafisa wa elimu wa Kata na walimu wakuu 1 Kusaidia utoji wa taaluma shuleni 2 Kusimamia matumizi ya fedha ya umma 3 Kuhakikisha shule inamiuondombinu sahihi 4 Kusimamia nidhamu ya walimu,wanafunzi na watumishi wengine wa Shuleni 5 Kusimamia vikao na kuweka kumbukumbu 6 Kuwa kiungo kati ya shule na jamii 7 Kuwa na mpango kazi wa muda na mbadala 8 Kuhudhuria vikao vya kijiji na Kata Mwisho mwezeshaji alijumuisha mada iliyomezani na kuongeza kazi za kila kundi Mwezeshaji pia aliwapa faida za mawasiliano katika uongozi jambo ambalo walishindwa kulitaja katika makundi yote na kueleza kuwa faida za mawasiliano ni:- 1 Kuokoa muda 2 Kupata taarifa kwa wakati 3 Kupunguza malalamiko 4 Kuinua pato la jamii na taifa 5 Kupata marafiki 6 Kuelimika 7 Kupunguza migogoro 8 Ni kiunganishi kati ya jamii na viongozi
Mwezeshaji aliwaeleza vizuizi vya mawasiliano ili kuwafanya waweze kuwa makini katika njia hii ya mawasiliano 1 kukosa kipato 2 kuwa na miundombinu mibovu 3 kukosa lugha nzuri ya kuwasiliana 4 kutoitisha vikao 5 kucheleweshwa au kutotoa mrejesho 6 migogoro na migongano katika mazingira 7 maumbile ya watu mfano walemavu
6.0 MATOKEO Watendaji/Wenyekiti katika ngazi ya Kijiji na Kata wamefahahamu umuhimu wa uwazi,uwajibikaji katika majukumu yao ya kila siku. kutokana na mafunzo haya viongozi hawa wamefahamu jinsi ya kutofautisha majukumu yao binafsi, kifamilia na ngazi waliokuwa katika jamii jambo ambalo mwanzoni hawakufahamu na muda mwingi walikuwa wakitumia katika mambo yao binafsi,familia na safari nyingi za Halmashauri kuliko kuwatumikia wananchi ilifikia wakati ndani ya wiki ofisi ya kijiji hufunguliwa mara mbili hadi tatu na si kwa masaa ambayo kiongozi huyo anatakiwa kukaa katika ofisi hiyo. Viongozi wamelewa jinsi ya kutengeza kalenda ya msimu jambo ambalo lilikuwa hawalifahamu na kusababisha wananchi wengingi kutoudhulia katika mikutano ya Vijiji kutokana na siku za mikutano huwa kipindi cha kulima,mavuno,siku ya soko na siku za ibada hivyo wameweza kufahamu jinsi ya kupanga kalenda ya msimu. Wamefahamu jinsi ya kupanga vipaumbele na aina tatu za kupanga vipaumbele
Viongozi wamefahamu jinsi ya kuweka mapato na matumizi katika mbao za matangazo Viongozi wamefahamu kamati kuu tatu ambazo ziko kisheria nazo ni:
Na kufahamu kamati zingine ni kamati ndogo ndogo zinazotokana na kamati kuu tatu jambo ambalo mwanzoni viongozi hao walichanganya kamati na kushindwa kutofauti kamati ambazo zipo kisheria na zile zilizotoholewa kutoka katika kamati kuu tatu,
Viongozi wamefahamu kuwa kamati hizo tatu za kisheria inashauri kuwa mwenyekiti wa Kitongoji/Kijiji asiwe kiongozi katika kamati hizo na badala yake kati ya wajumbe ndio wawe kiongozi katika kamati hizo na wamejua sababu za kwanini wameshauriwa hivyo.
Viongozi wamefahamu kuwa wanaweza kumualika mwananchi wa kawada wanawezaq kumualika katika mkutano wa Halimshauri ya kijiji kutoa ushauri wake ikiwa kunasababu ya kumualika mwananchi huyo 7.0 MATOKEO KWA WANANCHI wananchi wametambua kuwa wanahaki ya kushiriki katika mikutano ya Kijiji na kuhoji mapato na matumizi, mwanzo wananchi walikuwa hawashiriki mfano: Kuna wafanya biashara walikuwa wakija kukata miti katika kijiji cha Vuga lakini wananchi hawakushirikishwa na hawafahamu pesa za mfanyabiashara huyo zimekwenda wapi? Kutokana na mafunzo haya wananchi wamepeleka kesi kwenye vyombo vya sheria na sasa linashughuilkiwa. Mfano mwengine ni wanakijiji walikuwa wakihukumiwa kutokana na sheria ambazo zinakiuka katiba ya nchi katika kijiji cha kwemzuza mwananchi ambae hakubaliani na matakwa ya viongozi basi huchukuliwa mifugo kama fidia kutokana na kuhoji au kumpinga kiongozi bila kufuata utaratibu wa kisheria na wananchi hawashirikishwi katika maaamuzi badala yake wanaleta maagizo tu wa nini wafanye. Kwa sasa wananchi wamefahamu majukumu yao kama vile kuhakikisha kiongozi aliyemchagua anatimiza wajibu wake ipasavyo na anaongoza wananchi kwa mujibu wa sheria na pia wamefahamu kuwa wana haki ya kupinga uonevu katika jamii ikiwemo rushwa,uonevu,wizi na ubadhilifu wa mali za umma.
MABARAZA YA KATIBA MPYA, WAENDESHAJI CHAMAKIVU WAFADHILI THE FOUNDATIO FOR CIVIL SOCIATY CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA P.O.BOX 112 SONI-LUSHOTO-TANGA. E-mail vugalushoto@yohoo.com htt://envaya.org/CHAMAKIVU UTANGULIZI CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA , Ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi Tanzania nzima ambapo makao makuu ya shirika yapo Kjiji cha Bazo Kata ya Vuga Jimbo la Bumbuli Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Malengo ya CHAMAKIVU ni:- Kuelimisha jamii juu ya maswala ya kilimo na ufugaji Kuelimisha jamii juu maswala utawala bora na haki za raia Kuelimisha jamii juu ya VVU/UKIMWI
CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA(CHAMAKIVU) lilianzishwa rasmi mwaka 2006 na kupata usajiri wake tarehe 18/12/2008 namba ya usajiri NGO/00002774, lina wanachama 15 wa kujitolea wakiwa na lengo la kufikisha taarifa sahihi katika ngazi ya Kaya. CHAMAKIVU imetekeleza mradi wa kujengewa uwezo wa shirika mradi ambao ulisaidia CHAMAKIVU kuweza kufahamu namna ya uandishi wa miradi,utunzani wa taarifa za fedha na uandaaji wa mpango mkakati na masuala ya mazingira Mradi ambao pia uliwaalika vikundi vingine vitano navyo ni kikundi cha mazingira,kikundi cha Jitegemee,kikundi cha Mwela theatre group na kikundi cha Mapambano na kikundi cha Muungano nao wapate fursa ya kushiriki mafunzo hayo sababu CHAMAKIVU waliweza kuwatafuta wataalamu kutoka ndani ya asasi yetu ,kutoka Wilayani Lushoto na wengine toka Dar es Salaam SHUGHULI ZA SASA ZA SHIRIKA. 1) kuelimisha jamii juu ya kusimamia akiba ya chakula na biashara 2) kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya zana bora za kilimo 3) Kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa vikundi vya kijamii 4) Kuyasaidia makundi yaliopo katika mazingira magumu. 5) Kuelimisha jamii juu udhalishaji wa mazao na bustani 6) Kuelimisha jamii juu ya matumizi ya mbolea 7) Kuelimisha jamii juu ya kilimo cha umwagiliaji 8) Kuelimisha jamii juu ya kudhalisha mazo kwa nishati mbadala
Shirika linatekeleza shughuli zote zilizotajwa hapo juu kwa kujitolea na huku likijitahidi kuhamasisha makundi mengine kushirikiana nayo katika utekelezaji wake.
HISTORIA YA MRADI HUU. Mradi huu unajulikana kama mradi wa uimalishwaji wa Asasi mradi uliowafikia wanachama 10 wa CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA watu 15 toka katika vikundi vya kijamii hususani vikundi vya kilimo .Mradi huu ulilenga kuongeza ufahamu juu uandaaji wa miradi shirikishi,uandaaji wa mpango mkakati,maswala ya kilimo kwanza utunzaji wa kumbukumbu za fedha za wafadhili na zile zitokanazo na michango ya wanachama na wadau wengine. Mahitaji ya mradi huu yametokana na kutokuwepo kwa wanachama wa CHAMKIVU na vikundi vidogo viidogo vya kijamii wenye ujuzi juu ya uandaaji wa miradi,maswala ya kilimo kwanza, utunzaji wa mahesabu na uandaaji wa mpango Mkakati,Hakukuwa na mwanachama au mwanakikundi yeyote aliyekwisha wahi kushiriki au kushirikishwa katika mafunzo ya namna yeyote kati ya mafunzo yaliyotajwa hapo juu,tangu Shirika lilivyoanzishwa mwaka 2006 Tumekuwa tukipoteza fursa nyingi zilizopo kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi huo.Hatukuwa tunaweza kuandaa miradi ,hatukuwa na mfumo/muundo unaoweza kuchochea/kuleta matokeo chanya,hatukuwa na utaratibu mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu ambazo zimekuwa kama hitaji mojawapo muhimu kwa wahisani/wafadhili pindi watoapo vigezo vya upatikanaji wa ruzuku.hatukuwa tunafahamu mambo mbalimbali ya kilimo Kwa minaajiri hiyo wanachama tuliona ni vema kuomaba ufadhili toka Foundation For Civil Society shirika ambalo linatoa ruzuku kwaajili ya kujengea uwezo asasi za kiraia.Baada ya miezi kadhaa maombi yetu yalikubaliwa na utekelezaji ulianza mara moja. Shirika liliazimia na lilitimiza ushirikishaji wa wadau wote muhimu katika kuandaa malengo ya pamoja ili utekelezaji ,ufuatiliaji na tathimini vifanywe kwa pamoja. MALENGO YA MAFUNZO uwaongezea ufahamu wanachama 10 wa Chama Cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Vuga (CHAMAKIVU) na viongozi 15 wa vikindi vya wakulima juu ya maswala ya uandaaji wa miradi,usimamizi wa fedha na maswala kilimo kwanza
Kuwaongezea ufahamu wanachama 10 wa Chama Cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Vuga (CHAMAKIVU) juu ya uandaaji wa mpango makakati
SHUGHULI ZILIZOFANYWA KATIKA MRADI HUU 1) Kutoa mafunzo ya uandaaji ,wa miradi kwa wanachama 10 wa CHAMAKIVU na wawakilishi wa vikundi vya kilimo watu 15. Kati ya mambo waliyojifunza ni pamoja na ,
1) Mafunzo juu ya usimamizi wa fedha kwa wanachama 10 wa CHAMA CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII VUGA na wawakilishi wa vikundi vya kilimo watu 15 Shughuli hii imeandaliwa kwa lengo la kujua/kufahamu juu ya kufanya malipo ndani na nje ya shirika ,kujaza Analyisis book na cash book na namna ya kufaili hati za malipo.Mambo tuliyojifunza nipamoja na
1) Mafuzo juu ya uandaaji wa mapango mkakati kwa wanakikundi 10 wa CHAMAKIVU Shirika liliandaa shughuli hii kwa lengo la kutoa maelekezo juu ya maana ya mpango makakati na namna ya kuandaaa mpango mkakati na umuhimu wake. Mambo tuliyojifunza nipamoja na
1) Mafuzo juu ya maswala ya kilimo kwa wanakikundi 10 wa CHAMAKIVU na wanakikundi 15 toka katika vikundi vya wakulima Shirika liliandaa shughuli hii kwa lengo la kujua maana na ubora wa kilimo kwanza na umuhimu wake.
MHUTASARI Mradi huu umewawezesha washiriki katika utoaji wa maoni ya marekebisho ya Katiba na hivyo kuzima vilio, huzuni na malalamiko yasiyoisha ambayo yangetufanya tusipate Katiba isiyo na uwakilishi sawia wa wananchi. Malalamiko ambayo yalilamikiwa wakati wa kuchukua maoni ya mala ya kwanza na hata uundwaji wa mabaraza ya Katiba ya vijiji kwa kusema kuwa washindi walioshinda hawakushinda kihalali na hivyo wasingeweza kutoa maoni yao lakini kwa kupitia mradi na wataalamu tuliowatumia walikuwa wanaudhoefu wa kutosha juu ya masuala ya kuendesha mikutano ya aina hii,shughuli za mradi tulifanya na Mikutano kwa siku 3 kwa vikundi vya kijamii na wadau kutoka katika jamii Pia tulifanya usambazaji wa rasimu ya Katiba kwa wadau hao na waliweze kuchangia na kutoa maoni kwa uhuru na haki. HISTORIA YA MRADI HUU Kulikuwa na malalamiko mengi ya wananchi katika Kata yetu ya Vuga kutokana kukosa taarifa ya ujio wa tume ya kuchukua maoni ya marekebisho ya Katiba na hivyo watu wengi kukosa fursa ya kushiriki katika kutoa maoni yao na wasijue wanaweza wakatumia njia gani kuwakilisha maoni kutokana na eneo la mradi kuwa Kijijini sana Pia katika eneo la mradi kumekuwa na matatizo ambayo yalijitokeza kipindi cha kuchagua mabaraza ya Katiba na. Wagombea wengi wamechaguliwa kwa misingi ya uanachama wa vyama vyao waliomadarakani . Suala hilo lilijitokeza maeneo mengi ya mradi ukivihusisha vyama hivyo. Vyama hivi kila kimoja kilihamasisha wanachama wake kuchagua wagombea kutoka katika chama chake dhidi ya wagombea wa chama kingine. Kutokana na utafiti huo asasi yetu iligundua kuwa wafuasi wa vyama vya siasa walipita nyumba hadi nyumba kuomba kura kwaajili ya wagombea wao. Katika maeneo mengine viongozi wa kada mbalimbali za kisiasa katika vyama waliendesha kampeni za wazi kuhimiza kuchaguliwa kwa wagombea kutoka vyama vyao kinyume kabisa na nia nzuri ya Tume kuwa mchakato huu usitawaliwe na itikadi za vyama. Baadhi ya viongozi wa serikali walipigania zaidi watu wao waingie na kuwaachafua wale wenye sifa na hata kauli za baadhi ya viongozi hao walisikika wakisema kuwa wao waatahakisha watu wao wanapita sababu wao ndio serikali na hivyo kuzua manung”uniko mengi katika jamii kwa kupitia mradi huu tunaimani kuwa wananchi watakuwa na imani na kuitumia vizuri fursa yao ya kiKatiba kwa kutoa maoni yao kwa amani na utulivu na kutumia haki yao kiKatiba LENGO LA MRADI Kuviwezesha vikundi vya kijamii na makundi maalumu katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya marekebisho ya Katiba MATOKEO YA AWALI Vikundi vya kijamii na wanajamii wameelewa na wameshiriki katika kutoa maoni ya marekebisho ya Katiba 2.Uelewa umeongezeka kwa wanajamii 158 toka katika makundi maalumu ya Kijamii toka Vijiji vya Bazo na Vuga Kishewa wametoa maoni ya marekebisho ya Katiba. MATOKEO YA KATI Vikundi vya Kijamii na makundi maalumu katika jamii wanatoa maoni ya marekebisho ya Katiba mpya UTANGULIZI
MAKUNDI HAYO NI
MRATIBU ALIFANYA HESABU JUU KUJUA IDADI YA WASHIRIKI NA KUPATA JUMLA YA IDADI YA WASHIRIKI MIA MOJA NA MBILI(102) ME-50 &KE-52) MRATIBU ALIMKARIBISHA MWEZEJI ILI KUENDELEA UTOAJI WA MADA. v MWEZESHAJI ALIANZA KWA KUSALIMIA WASHIRIKI NA KUENDELEA KAMA IFUATAVYO:
MUWEZESHAJI MALENGO YA BARAZA Kuviwezesha vikundi vya kijamii na wanajiamii kuweza kutoa maoni ya mabadiliko ya rasimu Katiba mpya Baada ya mwezeshaji kutoa maelezo ya malengo ya rasimu ya Katiba mpya alianza kuelezea na kuwataka washiriki kufungua ukurasa no 31 sura ya sita ambayo inaelezea muundo wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na mwezeshaji kuwataka washiriki kuunda vikundi ambavyo vitajadili katika eneo hilo la muungaNo na jumla ya vikundi 8 ambayo kila Kikundi kilikuwa na jumla ya washiriki 13 Maswali muhimu yaliyojadiliwa ya(Sura ya sita Ibara ya 60)
v Serikari ya Jamhuri ya muungaNo wa Tanzania v Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar v Serikali ya Tanzania Bara.
MAPENDEKEZO:(VIKUNDI)
MWEZESHAJI: Kuuliza wanavikundi kama wamekubaliana na masawali husika ambayo yalikuwa yanajadiwa. Kisha kukaribisha mapendekezo Kikundi No.1 v Muungano wa serikali moja. Sababu: -kukiwa na serikali zaidi ya moja kutakuwa na gharama kubwa ya uendeshaji gharama ambazo watakao bebeshwa ni wananchi na kusababisha kuongezeka kwa umaskini kwa wananchi na kusababisha didimio la uchumi wa nchi -kuwaenzi Waasisi wawili wa muungaNo Nyerere na karume.ambao wao kwanamna moja waliweza kusaidia kutunganisha pamoja ili kuwa taifa lenye nguvu na tija
2. Nyongeza katika swali la pili -uwiaNo wa ugawaji wa lasilimali za taifa. mfano utakuta zanziba ni sehemu ndogo sana tofauti na Tanzania bara lakini panapotokea mgawanyo wa rasilimali hazigawanywi sawa kutokana na hilo Tanzania bara hupata kidogo na wakati huo zanzibar hupata kikubwa hali ya kuwa wao ni sehemu ndogo. Kikundi No 2 v Kuwe na Serikali moja Sababu: Umaskini, hii ni kutokana na nchi yetu kuwa maskini na kushindwa kukidhi mahitaji ya wananchi. Kundi hili liliona kuwa na serikali moja kutasaidia maendeleo ya haraka kutokana na muunganiko wa mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuleta maendeleo
Mapendekezo Kifungu cha sita kisiwepo kwasababu kitaleta migogoro katika serikali hiyo kwani vyama vingine vinataka ushindani na uadui Kundi hili liliweza kujadili kwa kina na kutaka kuwa vyama vya siasa visiwepo katika masuala muungano kutokana na vyama hivyo vinaweza kuleta udini,ukabila na kusababisha uadui na migogoro katika jamii Na wakashauri kuwa kuwepo na wasajiri wawili Tanzania bara na Zanzibar msajiri wa Zanzibar atakuwa anashughulikia vyama vya Zanzibar msajiri wa Tanzania bara atakuwa anashughulikia vyama vya bara, Kikundi No.3 v Kuwe na serikali moja Sababu kupunguza ubaguzi kundi hili liliweza kutoa ufafanuzi wa ubaguzi na kueleza kuwa iwapo kutakuwa na serikali tatu kila serikali kutakuwa na sheria na kanuni zake ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwa raia wa upande mmoja anapokuwa upande mwingine wa serikali nyingine.
WanaKikundi walitoa ufafanuzi kuwa umuhimu wa kuwepo na serikali moja kutasaidia kuwepo na uhuru wa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na kuweza kushrikiana na kufuata sheria na kanuni za pamoja
WanaKikundi walitoa ufafanuzi kuwa kukiwa na jeshi la pamoja kutasaidia kulinda mipaka yetu kwa pamoja na kuzuia maadui waliokuwa na nia mbaya na nchi yetu
2 Mapendekezo. Kuwe na usawa katika malipo kwa wafanyakazi wa selikari. Kwasababu wengine wanalipwa mishahara midogo wengine mikubwa mfaNo waalimu wanalipwa na mishahara midogo tofauti na kazi wanayofanya na kutosikilizwa mawazo yao na kuyathamani. Walimu waliweza kutoa maoni kwa kutaka kutugwa kwa sheria ya upandishwaji wa madaraja pindi wanaporudi kutoka vyuoni. Kikundi Namba 4 Swali la kwanza v Serikali tatu Kundi namba 4 liliweza kujadili juu ya Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na serikali ya Jamhuri ya muungaNo wa Tanzania Sababu Hii inaonyesha kuwa hata waandaji wa rasimu hii wanaijua vilivyo -Ubaguzi, imeonekana kuwa kuna ubaguzi kati ya wana Zanzibar na Wana Tanzania bara kwasababu Zanzibar wana baraza lao la wawakilishi na hakuna muwakilishi hata mmoja kutoka Tanzania bara.
Mapendekezo Wanapendekeza mambo yote saba ya muungano yapitishwe. Kikundi Namba 5 v Wapendekeza kuwa na serikali zote 3 Sababu:Lugha, hii ina maana kuwa kuwepo na Serikali inayoitwa Tanzania bara badala ya kuitwa Tanganyika - Hii itasaidia kulinda asili ya muungano - Usalama kwa serikali zote tatu kwa sababu kutakuwa na usawa - Kutakuwa na umoja na ushirikiano
Mapendekezo Michezo- Michezo iimarishwe ili kuziwakilisha nchi zetu Nje. Elimu- Mitaara yote iwe ya Jamhuri ya muungano Mavazi- Lazima kuwe na vazi la muungano
Kikundi Namba 6. v Wanapendekeza serikali mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya ya Zanzibar. Sababu:Hii itasaidia mgawanyo bora wa rasilimali za Taifa -Ulinzi bora ndani ya jamhuri na mpakani
Mapendekezo Hakuna haja ya kuomba uraia kama kutakuwa na serikali mbili au kama vitakuwepo lakini kusiwe na masharti magumu cha msingi ni kufuata sheria ya muungano
KIKUNDI Namba 7 v Wapendekeza serikali moja Hoja:Kuzuia kuporomoka kwa uchumi
MAPENDEKEZO. Kusiwe na vigezo vigumu kuomba uraia Mambo yote saba ya muungano yapitishwe
KIKINDI NAMBA 8. v Kuwepo na serikali tatu: Yaani Serikali ya Tanzania, Serikari ya Zanzibar na Serikari ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hoja:
Mapendekezo:Raia wawe huru kuomba uraia katika serikali zote tatu bila kuwa na masharti magumu Kwa maana hicho kifungu cha sita cha mambo ya muungano kisiwepo. Mambo sita ya muungano yaliobakia yawepo. MAONI YA WANAJAMII
v Mwanajamii 1(ME) Anapendekeza kuwa na serikali moja Hoja-Hii ni kutokana na umaskini wa wananchi hivyo wameona kuwa kukiwa na serikali moja kutasaidia kupunguza umaskini wa nchi zote mbili.
Mwanajamii 2 (ME) v Anapendekeza kuwa na serikali tatu: Hoja:Jamhuri ya Mungano wa Tanzania tayari ni shirikisho la nchi mbili tofauti yaani Tanzania na Zanzibar na kuzalisha kitu kimoja yaani Tanganyika -Tayari ni matakwa ya waliokuwa wengi. Tume ilitambua kuwa Watanzania walio wengi wanapendekeza serikari tatu. - Kutokuwa na usawa, kuwa na serikari tatu kutasaidia utendaji mzuri wa kujamii, kiuchumi na hata kisiasa.
Mwanajamii 1(KE) v Anapendekeza kuwa na serikari tatu Hoja: Kuepuka garama, hii itasaidia kupunguza gharama kwasababu watu wako kitu kimoja rais atakuwa mmoja tofauti ya kuwa na serikari tatu zenye raisi zaidi ya mmoja. -Matabaka, hii itasaidia kuondoa matabaka kwasababu watu wote watakuwa wamoja. -Vita, hii pia itasaidia kuondoa vita kwasababu hakutokuwa na matabaka.
Mwanajamii 4(ME) v Anapendekeza kuwa na serikali tatu Hoja, hii itasaidia kupata ajira haraka hasa kwa vijana kwani tayari kutakuwa na upana wa utafutaji wa masoko - Kila serikali iwe na mfumo wao ili kuepuka ubaguzi (kidini) - Kulinda historia ya jina la Tanganyika kwani Tanzania imebakia kuwa Tanzania bara na Sio Tanganyika kwani Zanzibar imebakia kuwa Zanzibar. MAPENDEKEZO Muundo wa shirikisho Ibara ya 57 sura ya 6 kifungu cha kwanza -Michezo na Utamaduni viwe katika Jamhuri ya muungaNo ili vijulikane ndani na nje ya nchi -Elimu, Mtaala uwe mmoja si Tanzania wala Zanzibar.
Mwanajamii wa 5(ME) Mapendekezo : Mambo saba ya muungaNo. Ushuru wa bidhaa, Anapendekeza kuwa kama mtu atalipia ushuru Tanzania basi apite Zanzibar bila kulipa tena, hivyo hivyo mtu akilipia Zanzibar basi Tanzania asilipe tena.
Mwanajamii wa 6(KE) Kuwe na serikali moja. Hoja-Hii itasaidia Nchi zote kufanya vitu kwa uhuru bila kuingiliwa na nchi nyingine
MAPENDEKEZO: -Serikari Ya Tanzania iitwe Tanganyika na sio Tanzania bara kama inavyojulikana kwa wengi. -Kuhusu usajili wa vyama vya siasa- anapendekeza kusajiliwa isipokuwa chama ambacho kitajulikana kitaleta machafuko nchini haswa kuchochea vita. -Kuwe na bunge la muungaNo kujadili mambo ya muungaNo -Uraia na uhamiaji, Wanapendekeza uraia kuwa mmoja. Sarafu ya benki kuu inatosha kuwa kielelezo tosha cha muungaNo kwani Kuna picha mbili za waasisi wa MuungaNo yaani Nyerere na Karume.
Mwanajamii wa (6) (ME) v Kuwe na serikali moja. Udini, Kukiwa na serikali tayari kutakuwa na matabaka ya kidini ambayo Tayari yatachochea uadui kati ya serikali hizo
Mapendekezo: Swala uhamiaji na uraia lisiwe swala MuungaNo
Mwanajamii wa (7) (ME) v Serikali moja Hoja: Huyu anapendekeza kuwa na serikali moja kwani hii itasaidia -Kuondoa matabaka -Watu wote kuwa sawa (Tanzania na Zanzibar) -Itasaidia kuondoa umasikini.
Mwanajamii wa (8)(ME) v Kuwa na serikali moja Hoja, Uadui , Kuwa na serikali tatu kutazua migogoro miongoni mwa nchi hizo tatu kwani kila nchi itakuwa na sheria zake ambazo zimejiwekea hivyo kuwabana wengine wan chi nyingine.
Mapendekezo: Kusiwepo na wawekezaji katika selikari hiyo itakayokuwepo kwani watakuwa kikwazo na chanzo cha mgogoro.
Mwanajamii wa (9)(KE) v Kuwa na serikali moja Hoja:Migogoro, kama kutakuwa na serikari tatu ina maana watu lazima watakuwa na migogoro hasa ya ya ardhi(mipaka) kwani kila mmoja atapende nchi yake iwe bora kuliko nyingine.
CHANGAMOTO. Washiriki kudai posho Washiriki kuwa wengi kuzidi bajeti ya mradi Lugha- Washiriki walikuwa wakichanganya lugha ya (kigeni)
HITIMISHO: v Walio wengi wanapendekeza serikali moja.
CHANGAMOTO
MAPENDEKEZO v TUTENGEWE BAJETI YA KUTOSHA v WANANCHI ELIMU YA DHANA YA KUJITOLEA v FUNGU LITOLEWE KWA MUDA ULIOPANGWA v FUNGU LIWE KUBWA ILI TUWEZE KUFIKIA VIJIJI VYOTE
SHUKRANI The foundation for civil society kwa kutoa ufadhili Wanajamii walioshiriki katika mkutano Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kutupatia kibali na rasimu za kutosha za Katiba Mkuu wa shule ya sekondari Vuga Bazo kwa kutupati ukumbi kwa siku zote za mkutano Wanachama na viongozi wa Chama cha Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Vuga Vikundi vidogo vidogo vya Kijamii kwa kukubali wito wetu na kushirikiana nasi kwa muda wote Tunawashukuru pia Waandishi wa Habari kwa kuchukua habari zetu katika mkutano wetu wa mabadiliko ya Katiba. Tunamshukuru muwezeshaji wetu Prisca Roti Kaniki kwa kuendesha mjadala kwa umahili wa hali ya juu Tunamshukuru mchua dondoo wetu Naima Amiri kwa kuchukua taarifa za washiriki kwa umahiri wa hali ya juu. Tunamshukuru mratibu Jumaa Dhahabu kwa usimamizi mzuri katika shuhuli zote. Tunawashukuru viongozi na wanachama wote wa CHAMAKIVU Tunamshukuru Mishi Mgahawa aliohudumia vizuri chakula kwa washiriki wetu. JUMAA IDD DHAHABU MRATIBU & MSIMAMIZI WA MIRADI
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe