Base (Swahili) | English |
---|---|
MADHUMUNI NA KAZI ZA UBOMA SERA 1. Kujenga ufahamu miongoni mwa jamii kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uandaaji wa Sera mbalimbali za Taifa. 2. Kuikumbusha Serikali kuhusu haki ya wananchi kushirikishwa katika michakato mbalimbali ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na Uandaaji na utekelezaji wa Sera mbalimbali. 3. Kuwashawishi na kuwawezesha wananchi kushiriki katika mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazowahusu. 4. Kufanya Utafiti na kuwapatia Taarifa wadau mbalimbali wa Maendeleo kuhusu Ushirikishwaji wa Jamii katika mchakato mzima wa uandaaji na utekelezaji wa Sera na maendeleo ya Taifa 5. Kufanya Utafiti wa Utekelezaji wa Sera mbalimbali za Taifa kwa Ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU 1. Kutoa Elimu ya Utawala Bora kwa jamii, Viongozi wa Serikali kuu na za Mitaa ili Dhana ya Demokrasia itafsiriwe kwa Vitendo na hivyo kufikia Maendeleo ya kweli. 2. Kuchapa Vitabu, Majarida na Magazeti yenye ujumbe wa Utawala Bora na Haki za Binadamu. 3. Kuainisha Uhusiano uliopo baina ya Utawala Bora na Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi. 4. Kufanya Utafiti kuhusu hali halisi ya Utawala Bora na Haki za Binadamu kuanzia ngazi ya Uongozi kwa Sekta mbalimbali zinazohusika katika Usimamizi na Kutafsiri Sheria. 5. Kutoa Elimu ya Umuhimu wa Kumiliki Ardhi Kisheria kwa Wananchi na Wakulima ili waweze kupata dhamana mbalimbali ikiwamo Mikopo katika Taasisi za Fedha. 6. Kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Sheria katika kutoa Elimu ya Sheria na Haki za Binadamu kwa Jamii. |
PURPOSE AND FUNCTION OF Boma POLICIES 1. Creating awareness among people about the importance of participating in the development of various national policies. 2. Government reminded me about the rights of citizen participation in various development processes including the Formulation and implementation of various policies. 3. Persuading and enable citizens to participate in the process of formulation and implementation of various policies concerning. 4. Conducting research and providing information to stakeholders about the development of Community Participation in the process of formulation and implementation of policies and national development 5. Doing Research on Implementation of National Policies for different level of County, District, Regional and National GOVERNANCE AND HUMAN RIGHTS 1. Providing Education for Good Governance in the community, leaders of central and local government to be translated to the concept of democratic practices and achieve genuine development. 2. Printing books, papers and magazines with the message of Good Governance and Human Rights. 3. Identify the relationship between Good Governance and Human Rights and Economic Development. 4. Doing Research on the nature of the Governance and Human Rights from the level of leadership in various sectors involved in the Monitoring and Interpretation of Law. 5. Providing Education Legal Importance of Land to Farmers Citizens and to get various securities, including loans to financial institutions. 6. Collaborating with various stakeholders of the law in providing education law and Human Rights Community. |
Translation History
|