Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
Kikundi hiki kimeundwa na wanawake walio athirika na Virusi vya ukimwi. Baada ya kugundua hali zetu mbaya za kiafya mwaka 2006 ndipo tulipo amua kuanzisha kikundi hiki. Mwezi February tarehe 9 mwaka jana ndipo tulipo pata usajili wa kuwa NGO rasmi. Kwakuwa kikundi chetu kilikuwa ni kichanga, hatukujua namna sahihi ya kupata ruzuku. Hivyo tukakubaliana na shikrika linalo fanya kazi na wa athirika TANOFA kuwa tuchangie kiasi cha shilingi laki tano alafu baada ya mwezi watupe mkopo wa milioni mbili tufanyie kazi alafu marejesho yataanza baada ya miezi miwili toka mkopo utakapotolewa. Lakini mkopo haukutolewa na fedha tulizowapa hazijarejeshwa mpaka sasa. Kwa sasa tatizo letu kubwa ni kwamba tumeshindwa kulipa kodi ya pango, kwahiyo ofisi zetu tumezihamishia katika nyumba ya mwenye kiti wa shirika letu Bi DORA MWALUKO. Tunajihusisha na miradi tofauti ili kupata kujiwezesha. Habari zaidi naomba usome kipengele cha miradi. |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe