Asili (Kiswahili) | English |
---|---|
Tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha mwaka 2012. Tunawapa Envaya kheri ya mwaka mpya pamoja na Wadau wote. Mwaka 2011 tumeumaliza kwa majonzi makubwa kutokana na Taifa kupoteza rasilimali watu, kila upande yalipotokea mafuriko ni vilio kwa Watanzania wengi kupoteza ndugu, rafiki na jamaa, pia makazi, mali na wengi kukosa ajira. Tukiangalia upande wa makazi - wengi hawana mahali pa kuishi; wenye nyumba - zilibomoka kabisa na wapangaji kuhangaika huku na huku kutafuta mahali pa kuishi pamoja na familia zao. Tunaishukuru Serikali yetu kwa hatua za haraka zilizochukuliwa kwa wengi kuwaweka sehemu moja kwa ajili ya kuwapatia malazi, chakula na nguo za kujisetri, upande wa mali - wengi hawana matumaini ya kupata tena mali zao walizozipoteza katika mafuriko haya vile vile ajira za wengi zimekoma kutokana na viwanda vyao kubomoka na mali zote kuchukuliwa na mafuriko pia mashine zao kuhitaji matengenezo makubwa ili kuanza kufanya tena uzalishaji. AYORPO, tunawapa pole sana WAHANGA wa mafuriko pia ndugu, jamaa, na rafiki zetu waliopoteza maisha katika mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kutokea hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam. AYORPO kama Wadau tunaoshughulika na jamii limetugusa sana, ombi kwa ndugu zetu Wahanga na wengine walioguswaguswa kidogo, waisikie sauti ya Serikali yetu kwa kuhama mara moja mabondeni na kuhamia mahali salama walipopatiwa na Serikali yetu Tukufu. Ndugu zetu tunapaswa kuzitii Mamlaka husika za hapa duniani ndipo tutafunguliwa makubwa ya kumheshimu Mungu wetu tunaemwabudu kila siku katika Makanisa au Misikiti yetu (kwa ujumla wake tumwogope Mungu aliyeziweka Mamlaka hizi chini ya jua). Na katika upande wa Serikali - ombi letu ni kwamba; kwa wale ambao bado hawaoni umuhimu wa kuhama na hata wengine wanadai mambo ambayo si rahisi kwa Serikali kutekelezea kila familia au mtu mmoja mmoja, basi; tuendelee kuwaelimisha kwa upendo na amani, kwa kuwa wameshaathirika - wanahitaji upendo mkubwa na umakini kutokana na yale yaliyowatokea kama binadamu. Mwisho, tunaomba Mwenyezi Mungu aufanye mwaka 2012 wa mafanikio, masahihisho kwa yale yaliyopita na tudumishe amani, upendo na utu wetu unaotokana na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya familia zetu na pia kuikomboa nchi yetu Tanzania ipate kusonga mbele katika kila jambo tukiukataa kabisa umasikini unaoleta kuombaomba. |
We thank God for bring us in 2012. We give Envaya Happy new year with all stakeholders. In 2011 we finished with great sorrow for the loss of national human resources, each side emerged flooding is stagnation for many Tanzanians lost relatives, friends and relatives, as well as housing, property and majority unemployment. Looking toward the settlement - most do not have a place to live, the house - zilibomoka with tenants struggling around finding a place to live with their families. Tunaishukuru our Government for swift action taken by many of them one for providing shelter, food and clothing kujisetri, on the property - many have no hope of getting back their property were zozipoteza in flooded these as well as employment and many are extinct due to manufacturing crumble and all their possessions taken and flooded their machines also require major repairs to start doing more productive. AYORPO, very sorry we gave the flood victims are also brothers, relatives, and our friends who lost their lives in floods that have never been possible, especially for residents of Dar es Salaam. AYORPO as partners we are dealing with very limetugusa community, prayer for our brothers victims and others who guswaguswa little, hear the voice of our Government to immediately leave the valleys and they do get moved to a safe place and our esteemed government. Brethren, we must obey the relevant authorities of this world that we opened our big honor God we emwabudu every day in our churches or mosques (in general Fear God who put these powers under the sun). And in terms of government - our plea is that, for those who still do not see the importance of movement and even some people claim things that are not easy for the government carrying out each family or individual, therefore, continue to educate with love and peace, to have been affected - they need a great love and attention from what yaliyowatokea as humans. Finally, we ask Allah aufanye 2012 success, the corrections in the past and tudumishe peace, love and our humanity arising from working hard for our families and also to liberate our country may be moving forward in everything we rejected all the poverty that makes beg. |
Historia ya tafsiri
|