Envaya

Translations: English (en): User Content: WIGmGWmFyix3bhgzfdsYdj97:content

Base ((unknown language)) English

KATIBA YA KIKUNDI CHA KISESA WOMEN NETWORK

Utangulizi:

Chama cha KISESA WOMEN NETWORK ni miongoni mwa vyama/ vikundi vya hiari vya watu wenye ulemavu/ waishio katika mazingira hatarishi. Kikundi hiki ni kati ya vikundi vinavyotokana na makundi maalum.

 

 

Aidha watu wanaotokana na makundi maalum, wanazo changamoto nyingi, ambazo zinawafanya wasikubalike haraka kwenye jamii, kiasi cha kunyanyapaliwa na hata kutopata huduma za Afya, Elimu na hata ustawi kiasi cha kuwafanya waishi chini zaidi ya kiwango cha umaskini.

 

Uhuru, Haki na Usawa umeelezwa vizuri kwenye katiba ya nchi. Uhuru huo ndio unaotoa fursa ya kila kundi lenye lengo fulani na vikwazo fulani kuungana kwa pamoja kuifikia jamii ili kupunguza au kuondoa vikwazo vilivyopo. Na kuhitaji uundwaji wa Kikundi/Chama KISESA WOMEN NETWORK.

 

SEHEMU YA KWANZA.

 

1.    Jina la Chama - KISESA WOMEN NETWORK

2.   Makao Makuu : Makao makuu ya kikundi yatakuwa Kisesa – Jiji la Mwanza Wilaya ya Magu    DIRA : kuhakikisha kwamba jamii inashirikishwa na kushiriki katika jahudi za kuondoa utegemezi/ umaskini wa wanawake wenye ulemavu, yatima, wajane na wanawake waishio katika mazingira magumu.

 

4.       MADHUMUNI:

          Madhumuni ya uundwaji wa kikundi ni kufanya yafuatayo:-

a)    Kuinua maisha ya wanawake wenye ulemavu, yatima, wajane na waishio katika mazingira magumu.

b)    Kutoa elimu ya staili mbalimbali za kuyamudu maisha (ujasiliamali)

c)    Kujenga moyo wa kujiamini.

d)    Kujenga na kuboresha mahusiano na mashirika mengine ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yanayosaidia wanawake.

e)    Kulinda haki na maslahi ya wanawake wenye ulemavu, yatima, wajane na waishio katika mazingira magumu kiafya ki-elimu, kijamii na ustawi wa akina mama .

f)     Kuelimisha Umma juu ya matatizo ya kisayansi ya wanawake wenye ulemavu, yatima, wajane na waishio katika mazingira magumu.

g)    Kuhakikisha na kudumisha heshima na haki za binadamu kwa wanawake waishio katika mazingira magumu.

h)   Uanzishaji wa SACCOS

i)     Kushirikisha wanawake katika masuala ya uatawala bora, haki za binadamu, demokrasia na vita dhidi ya rushwa.

j)     Wanawake kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vipya vya ukimwi

k)    Kuhakikisha wanachama wanapata ufahamu wa kutosha juu ya kushiriki na kushirikishwa katika kuchanganua changamoto kadhaa zinazowakabili katika kuelekea kujiondolea umasikini wa mawazo na kipato n.k.

 

SEHEMU YA PILI

 

UANACHAMA.

(i) Kutakuwa na aina tatu za uanachama:

a) Uanachama wa kawaida – mwanamke mwenye ulembavu, mjane au anayeishi katika mazingira magumu , yatima.

 

b) Uanachama wa kushirikishwa – mtu yeyote ambaye si mwanamke ambae kukipenda kikundi na kupenda kukichangia kikundi kwa hali na mali .

 

c) Uanachama wa Heshima – mtu yeyote au chama ambacho kitakuwa na umuhimu mkubwa kwa kikundi katika kufanikisha malengo ya kikundi .

 

ii) Kuomba Uanachama:

Mtu yeyote ambaye hakuwa mwanachama mwanzilishi katika kifungu cha kwanza (a) na (b) atatambulika kwenye kikundi kuwa wanakikundi kwa kujaza fomu maalum ya maombi na kuipeleka kwa mratibu wa kikundi ambaye ataiwakilisha kwa uongozi kwa ajili ya maamuzi ya mwisho.

 

iii) Kiingilio:

a)    Kutakuwa na kiingilio cha uanachama ambacho kitatafasiliwa na uongozi .

b)    Kutakuwa na Ada ya kila mwanachama kwa mwaka ambayo itaamualiwa na uongozi.

 

2. KIKOMO CHA UANACHAMA

Uanachama unaweza kukoma:-

a)    Kwa kujitoa mwenyewe baada ya kutoa taarifa ya siku tisini (90)

b)    Kwa kuachishwa kutokana na utovu wa nidhamu na kutokua muadilifu.

c)    Kuwa kichaa na kuthibithishwa na daktari au kufariki dunia.

d)    Mwanachama ambaye amejiondoa au ameachishwa na amepona kichaa akitaka kujiunga tena ni lazima aombe upya kwa kufuata taratibu za sehemu ya pili kifungu cha kwanza namba (a) na (b) ya katiba hii baada ya miaka 2.

 

3. HAKI ZA MWANACHAMA:

Kila mwanachama atakuwa na haki zifuatazo:-

a)    kushiriki katika shughuli zote za chama kulingana na taratibu zilizowekwa.

b)    Kuhudhuria na kutoa maoni yake kwenye vikao/ mikutano ya kikundi.

c)    Kuchagua na kuchaguliwa viongozi wa kikundi na kuwa mkweli na kuwa na utayari wa kukosolewa na kuachia au kupata madaraka.

d)    Kuwa na moyo wa kujitolea kusikilizwa kujitetea na kutoa maelezo yake mbele ya vikao halali vya kikundi.

e)    Kuwa mwaminifu kutumia ujuzi wake kwa manufaa ya chama.

f)     Mwanachama wa kushirikishwa na mwanachama wa heshima ataruhusiwa kugombea uongozi au kupiga au kupigiwa kura.

 

4. WAJIBU WA MWANACHAMA.

Wajibu wa kila mwanachama utakuwa kama ifuatavyo:-

a)    Kutetea, kutekeleza sheria na kanuni za katiba hii ili kutekeleza kwa vitendo Madhumuni ya kuanzishwa kikundi hiki:-

b)    Kuwa tayari kukosea, kukosolewa na kutumia kipaji kuendeleza kikundi.

c)    Kutunza, kuthamini, kulinda mali na kubuni njia bora za kuendeleza kikundi.

d)    Kuwa tayari kujielimisha kwa bidii na kwa uwezo wake wote na kutumia elimu hiyo kwa fadia ya kikundi.

e)    Kushauri Uongozi kwa busara katika kusimamia mipango yote ya maandeleo au ya uendeshaji kwa manufaa ya kikundi.

 

 

 

SEHEMU YA TATU.

1. UONGOZI:

Kutakuwa na viongozi wafutao:-

  • Mwenyekiti.
  • Katibu
  • Mweka hazina.

 

2. SIFA YA UONGOZI.

Kiongozi yeyote sharti awe na sifa zifuatazo:-

  • Awe mwanachama hai.
  • Awe mwanamke, mwenye ulemavu, yatima, mjane au anayeishi katika mazingira magumu.
  • Awe mwenye moyo safi na uzoefu wa uongozi.
  • Awe na akili timamu.
  • Awe na Uzoefu wa kutetea haki za watu wenye ulemavu, yatima, wajane na waishio katika mzingira magumu na awe mwanamke.

 

3. MIIKO YA UONGOZI:

Kwa kiongozi yeyote ni mwiko:-

  • Kutumia madaraka yake aliyopewa kwa ajili ya manufaa yake binafsi.
  • Kula rushwa, kushiriki katika mambo ya kuhujumu kikundi na uchumi wake wa manufaa yake binafsi.
  • Kutumiwa na watu wa nje au ndani kuhujumu kikundi.
  • Kushiriki kwa njia yeyote kukashifu kikundi na kukitangaza kwa sifa yoyote mbaya ya kudhalilisha.

 

SEHEMU YA NNE

1. Uendeshaji wa Chama / Kikundi:-

Kutokana na:-

  • Mkutano mkuu wa kikundi.
  • Kamati ya Uongozi.
  • Kamati Tendaji.

 

2. Mkutano mkuu:

Ni chombo chenye maamuzi ya mwisho katika uendeshaji wa kikundi majukumu yake ni:-

  • Kuchagua viongozi wa kikundi, Mwenyekiti / Katibu na Mweka Hazina.
  • Kuidhinisha uundwaji wa kamati tendaji
  • Kubadili au kurekebisha katiba.
  • Kupokea taarifa ya mwaka ya mwenyekiti .
  • Kupitisha bajeti ya kikundi.
  • Kuteua Mkaguzi wa mahesabu.
  • Kupitisha jina la mlezi wa kikundi.
  • Kuchagua wajumbe 2 watakaoungana na M/kiti , Katibu na mweka hazina kuunda kamati tendaji
  • Utachagua mwakilishi yeyote kwenda kwenye vyombo ambavyo vinahitaji kikundi kuwakilishwa.
  • Utasikiliza utetezi wa wanachama waliofukuzwa au kupewa adhabu mbalimbali na kutoa maamuzi ya mwisho.
  • Utafanya mikutano yake mara moja kwa mwaka lakini unaweza kufanya mkutano usiokuwa wa kawaida wakati wowote iwapo kamati ya uongozi itaona inafaa au 2/3 ya wanakikundi watataka kuitisha mkutano mkuu (maalum).
  • Mwenyekiti wa kikundi ndiye atakuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu na mratibu atakuwa katibu (m) wanachama wote ni wajumbe wa mkutano mkuu.

 

3. Kamati ya uongozi ya kikundi.

Kutakuwa na kamati ya uongozi ya kikundi ambayo itakuwa na wajume wafuatao:-

  • Mwenyekiti wa kikundi.
  • Mweka hazina wa kikundi.
  • Katibu wa kikundi.

 

4. Kazi za kamati ya Uongozi:

Kamati ya Uongozi itakuwa na kazi zifuatazo:

  • Itasimaimia utekelezaji wa maamizio yaliyopitishwa na mkutano mkuu wa kikundi.
  • Itasimamia na kuongoza shughuli za maendeleo ya kikundi.
  • Itaangalia mienendo na vitendo vya wanachama vya wanachama na vyombo vyote vya kikundi.
  • Itafanya mikutano ya kawaida mara moja kila baada ya miezi 3 au wakati wowote itakapobidi. Kufanya mikutano.
  • Itaunda idara nyingine ndogo ndogo ikiwa wataona inafaa kwa manufaa ya uendeshaji bora wa kikundi.

 

5. Kamati Tendaji

Kutakuwa na Kamati tendaji ambayo itaundwa na:-

  • Mwenyekiti wa kikundi.
  • Katibu wa kikundi.
  • Mweka Hazina na wajumbe 2 waliochaguliwa na mkutano mkuu.

 

6. Kazi za kamati Tendaji

  • Hii ni kamati muhimu sana ambayo ndiyo kamati itakayobuni mipango na miradi ya kikundi.
  • Itapanga bajeti ya kikundi na kuipeleka kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kupitishwa.
  • Itabuni mipango, miradi mipya na kuiendesha.

 

SEHEMU YA TANO.

1. UONGOZI WA CHAMA.

Kutakuwa na viongozi wakuu wa kikundi wafuatao ambao watachaguliwa kila baada ya miaka mitatu (3)

  • Mwenyekiti wa kikundi.
  • Katibu wa kikundi.
  • Mweka hazina wa kikundi.
  • Wajumbe wawili wa kamati tendaji.

 

1.1. Kazi ya Mwenyekiti wa kikundi:-

  • Atakuwa ndiye msemaji mkuu wa kikundi na atakuwa anajitolea.
  • Atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kikundi.
  • Atakuwa na kura za turufu endapo pande mbili zitalingana.
  • Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya chama
  • Kama mwenyekiti hatakuwepo, atachaguliwa mwenyekiti wa muda kuongoza vikao.

 

1.2. Kazi za Katibu

  • Kuwa katibu wa vikao vyote vya chama na anaweza akaajiliwa.
  • Ndiye mtendaji mkuu wa kikundi.
  • Ni mwenyekiti wa kamati ya nidhamu pamoja na wajumbe wawili wa kamati tendaji.
  • Atawajibika kuitisha vikao vyote vya chama akiwasiliana na mwenyekiti.
  • Ataweka orodha sahihi ya wanachama na kutunza kumbukumbu za mali na amana za chama.
  • Atatunza kumbukumbu za kudumu za shughuli za kikundi za kila siku. Atatoa taarifa za vikao kwa kila mwanachama na atajulisha wajumbe wa kamati za kikundi juu ya kuchaguliwa kwao kazi watakazozifanya.
  • Atakuwa ndiye mtasisi mkuu wa katiba ya kikundi na mtunzaji wa nyaraka muhimili za kisheria za kikundi.

 

1.3. Kazi za Mweka Hazina:-

  • Atakusanya, kupokea na kuweka mahesabu ya fedha zote zinazoingia na kutoka katika kikundi kwa michango, ruzuku, misaada na malipo ya aina mbalimbali. Na ataweza kuajiliwa.

 

  • Atakuwa ni mjumbe wa kamati ya uongozi na kamati ya mipango fedha na uendeshaji.

 

  • Ndiye afisa mipango wa kikundi katika kubuni vyanzo vya mipato kwa kushirikiano na kamati ya mipango, fedha na uendeshaji.

 

  • Kwa kushirikiana na kamati ya mipango, fedha na uendeshaji atapanga bajeti ya kikudni na atatayarisha taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi.

 

1.4. Watia saini akaunti za kikundi.

Kutakuwepo na watia saini katika akaunti za benki ambazo ni

(i) Mwenyekiti, Mratibu na Mweka Hazina.

 

SEHEMU YA SITA.

 

1.1. Mlezi wa kikundi:

Kutakuwa na mlezi wa kikundi atakayeteuliwa na kamati ya uongozi na kuthibitishwa na mkutano mkuu wa kikundi.

 

1.2. Kazi mlezi wa kikundi:-

Atakuwa ni mishauri muelekezi wa kikundi kwa masuala ya maendeleo ya kikundi. Pia atashauri katika kukubali, kutafuta au kuridhia ufadhili.

 

1.3. Mapato ya Chama.

Chama kitapata mapato yake kutokana na:-

  • Ada na michango ya wanachama.
  • Miradi, vitega uchumi n.k.
  • Ruzuku, misaada ya haki na mali kutoka serikalini, mashirika ya uuma, makampuni, wahisani wa nje na ndani.

 

KUKOMA / KUFUTWA KWA KIKUNDI.

Pindi kikundi kitakapositisha shughuli zake au kufutwa basi miliki zote za mali zitagiwiwa kwa vyama vya kiraia vyenye madhumuni sawa na kikundi.

 

 

 

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register