Base (Igiswayire) | English |
---|---|
Wananchi wa kijiji cha Nyamhoza wamemshikiria mwenyekiti wao wa kijiji kwa tuhuma za kula fedha za pemebeo za kilimo ambapo alishirikiana na kamati ya vocha ya kijiji kula fedha hizo.Aidha mtendaji wa kijiji hicho ameshatoroka na hadi sasa hajulikani aliko. Juhudi hizi zimefanyika kupitia mradi wetu wa ufuatiliaji wa matmizi ya umma. Habari nyingine tulizozipata wakati wa ufuatiliaji na tathimini ya mradi kutoka kijiji cha Kirando mwenyekiti wa kijiji hicho amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye hasa baada ya kubainika kwamba alitumia milioni 9 za kijiji kununua mashine yake ya kusoza jambo ambalo lilibainika wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya umma katika kijiji hicho. Wakati hayo yakiendelea katika vijiji hivyo huko Sunuka wananchi walichukua hatua za kumhoji mheshimiwa diwani juu ya taarifa za ujenzi wa hosteli katika shule yao ya kata kwa thamani ya shilingi 220,000,000/= ambapo hadi sasa msingi haujachimbwa kabisa licha ya kuwa mwaka wa fedha kwa ajili ya kazi hiyo unakwisha june mwaka huu. Aidha Diwani huyo alikiri kuwepo kwa bajeti hiyo katika mwaka huu wa fedha na kueleza kuwa muda si mrefu mkandarasi ataanza kufanya kazi hiyo. Lakini kama si kufanyika kwa mradi huu hakuna aliyekuwa na taarifa juu ya ujenzi huo. |
Citizens of the village of Nyamhoza they have crowns chairman of the village to eat money accusations pemebeo farm where he collaborated with the village committee voucher eat money hizo.Aidha executive village and up to now has shatoroka unknown invitation. These efforts have been done through our project monitoring matmizi public. News we found during the monitoring and evaluation of the project from the village of Kirando chairman of the village had voted down the no confidence and especially after identified that he spent 9 million of the village to buy a machine his point with something that lilibainika during the process of monitoring the use public in the village. While these are underway in the villages so there Sunuka citizens took steps to interviewing Mr. councilor on the reports of the construction of hostels at the school of their wards in the value of Shs 220,000,000 / = which up to now based on the ujachimbwa completely despite being in the money for the job So you have june this year. Either Councillor admitted the existence of the budget in this fiscal year and state that not long term contractor will begin working. But if not done with this project which had no information on the construction. |
Ibyasobanuwe
|