Envaya

Translations: English (en): User Content: WI000BA3B846A2E000002794:content

Base (Swahili) English

Jumuiya ya The Poultry Farmers Development Organization (POFADEO) ni jumuiya ya wafugaji iliyoanzishwa na wafugaji wakishirikiana na baadhi ya wataalamu wa mifugo. Jumuiya hii ilianzishwa kwa lengo la kuandaa mazingira bora ya ufugaji ili wafugaji hususan wa kuku na jamii za ndege waweze kuendeleza shughuli zao za ufugaji kwa ufanisi zaidi.

Jumuiya ya POFADEO tangu kuasisiwa kwake miaka kumi iliyopita, imefanya kazi nzuri ya kuwashajiisha wafugaji kuendeleza shughuli za ufugaji kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji ili kuboresha uzalishaji katika mifugo yao. POFADEO inatumia wataalamu waliomo katika jumuiya hiyo kuawapatia taaluma wafugaji kuhusu umuhimu wa kuchanja mifugo yao, ulishaji bora wa kuku katika umri tofauti, utotoaji bora wa vifaranga, kujikinga na magongwa mbali mbali na mambo mengineo. 

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA

jumuiya ya POFADEO tangu kuasisiwa kwake imefanya mambo mabli mbali kama vile kutoa taaluma ya utawala bora kwa wajumbe wa kamti za masheha katika shehia mbali mbali za wilaya Wete, Chake chake, Micheweni na Mkoani (wilaya nne za kisiwa cha Pemba). Mradi huu uligharamiwa na shirika la The Foundation for Civil Society (FCS) ambapo jumla ya shilingi ishirini na moja, ishirini na nane elfu na mia mbili (21,028,200/=) zilitumika katika kufanikisha mradi huo. 

Miradi mingine iliyofadhiliwa na shirika la The Foundation For Civil Sciety ni mradi wa kuijengea uwezo jumuiya ya POFADEO kuhusu utawala bora ambapo jumuiya ilipata jumla ya shilingi milioni tano (5,000,000/=).

POFADEO vile vile iliweza kutoa mafunzo kwa wafugaji kuhusu ufugaji bora wa kuku wa asili kutokana na ufadhili wa shirika la Tanzania Buisness Development Scheme, chini ya mpango wa Matching Grants Scheme. Shirika hili lilitoa jumla ya shilingi milioni nne, laki nane, mia tano na hamsini.

Mbali na miradi hiyo jumuiya ya POFADEO inafanya miradi mbali mbali ya kuwafundisha wafugaji kwa kutumia nguvu na michango ya wanajumuiya na wataalmu waliomo ndani ya jumuiya hiyo.

The stock breeding Farmers Community Development Organization (POFADEO) is a community of herders and farmers established in collaboration with some of veterinary professionals. This community was founded for the purpose of preparing a better environment for livestock to livestock, especially poultry and bird communities can sustain their farming operations more efficiently.

Community POFADEO since her establishment ten years ago, has done a good job of kuwashajiisha pastoral livestock development activities based on best practice principles to improve livestock production in their livestock. POFADEO uses professionals who are in the academic community kuawapatia farmers about the importance to immunize their animals, feeding the best chicken in a different age, utotoaji best of chicks, prevention and hit far away from a variety of other things.

Gains

POFADEO community since his establishment has become far things such as providing education of good governance for members of the storyteller kamti in various districts shehia Wete, Chake Chake, Micheweni and region (four districts of the island of Pemba). This project was financed by the organization of The Foundation for Civil Society (FCS), where a total of twenty-one shillings, twenty-eight thousand two hundred (21,028,200 / =) were used in accomplishing the project.

Other projects funded by the organization of The Foundation For Civil Sciety is a project of community capacity build me POFADEO about good governance where the community received a total of five million shillings (5,000,000 / =).

POFADEO also managed to train farmers on better farming of poultry due to the nature of corporate sponsorship of Tanzania Buisness Development Scheme, under the Matching Grants Scheme. The organization released a total of four million, eight hundred thousand, five hundred and fifty.

Apart from the projects POFADEO community makes various projects to teach farmers to use force and contributions of community members and will almu those within that community.


In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register

Translation History

Google Translate
October 1, 2010
The stock breeding Farmers Community Development Organization (POFADEO) is a community of herders and farmers established in collaboration with some of veterinary professionals. This community was founded for the purpose of preparing a better environment for livestock to livestock, especially poultry and bird communities can sustain their farming operations more efficiently. – Community POFADEO since her establishment ten years ago, has done a good job of kuwashajiisha...