| Asili (Kiswahili) |
English |
“CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya viziwi ina maisha bora, inayojijengea uwezo wa kujiamini, kujithamini, kujiendeleza, kukuza lugha ya alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo, kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na serikali na taasisi nyingine.”
CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya watanzania inawatambua, inawakubali, inawathamini, inawashirikisha viziwi na kuhakikisha hawasumbuliwi na umasikini, unyanyasaji, ubaguzi na ukandamizaji wa aina yoyote”
- MALENGO YA CHAVITA
Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha hili kwa:
- Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapa Tanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
- Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
- Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama ya Tanzania.
- Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
- Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
- Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
- Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
- Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.
|
-
(a) Kufanya shughuli zote zinazohusu viziwi, kutoa huduma na kuandaa mikakati mbalimbali kwa manufaa ya viziwi wanachama.
-
(b) Kuwaunganisha na kuelimisha viziwi ili wapate hali bora ya maisha, huduma muhimu kama vile raia wengine wa nchi.
-
(c) Kupigania haki na usawa, ushirikiano na jumuiya zingine, vyombo vya serikali na mashirika mbalimbali yenye lengo sawasawa na chama chetu.
-
(d) Kushirikiana na matawi mengine moja kwa moja au kupitia Chama cha Viziwi Tanzania.
-
(e) Kufanikisha malengo ya CHAVITA
-
(f) Kulinda na kuheshimu Katiba ya CHAVITA.
-
(g) Kuhakikisha matumizi sahihi ya Lugha ya Alama yanapewa kipaumbele na kutumiwa ipasavyo kwa Viziwi wote na Wakalimani katika matawi. Hivyo matawi yatabuni mbinu mbalimbali za kuboresha na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama. Pia kushirikiana na CHAVITA Makao Makuu ili kuweka mikakati ya kupata wakalimani bora wenye uwezo wa kuwaunganisha Viziwi na watu wengine wanaosikia.
-
(h) Kukusanya takwimu sahihi za Viziwi waliopo kwenye matawi (mikoa/Wilaya) zao kwa kushirikiana na ofisi za viongozi wa serikali za mitaa.
|