Asili (Kiswahili) | English |
---|---|
MED KUGHARAMIA MITIHANI YA MAZOEZI IV KIKUYU SEKONDARI.Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma MED litagharamia uchapishaji wa mitihani ya Mazoezi kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kikuyu ili kuongeza maarifa kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwezi Novemba, 2013. Uamuzi huo wa MED umetolewa katika kikao cha pamoja kati ya wazazi, wanafunzi na walimu wa kidato cha nne wa shule hiyo kilichoitishwa kwa lengo la kutathimini matokeo ya kidato cha Nne 2012 na kujipanga kwa ajili ya matokeo ya mtihani wa mwaka huu. Akichangia katika kikao hicho Mratibu wa MED Bw.Davis Makundi Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa wahitimu wa mwaka huu wanafanya vizuri hapana budi jamii,walimu,wazazi,wanafunzi na wadau mbalimbali kuungana pamoja kuwawezesha wanafunzi kupata mazoezi ya mara kwa mara ya majaribio ya mitihani ya kujipima Akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne 2013 kwa wazazi mwalimu wa taaluma shuleni hapo Francis Tumaini Wambura amesema kidato cha nne kwa mwaka huu Kwa mujibu wa taarifa za idara ya taaluma shuleni hapo kati ya wanafunzi 168 wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu wanafunzi 21 mpaka sasa hawaja sajiliwa kutokana na utoro. Aidha taarifa zimeongeza kuwa zoezi la kulipia ada ya mtihani wa taifa linalotarajia kukamilika tarehe 28 mwezi huu wa pili inaonekana kusuasua ambapo wanafunzi 40 pekee ndio waliolipia ada hiyo hadi sasa. |
FINANCING OF PRACTICE IV examinations SECONDARY Figs.Friends of Education Organization Dodoma MED printing litagharamia Practice exams for students in Form Four in secondary schools Kikuyu to increase knowledge for students of the school are expected to sit for the Form Four graduation in November, 2013. The decision of the MED has been issued in a joint session between parents, students and teachers to form the school's fourth requested for the purpose of evaluating the results of the Fourth Form 2012 and organize the results for the test this year. Akichangia at the session coordinator MED Bw.Davis groups said that in order to ensure that graduates this year are doing well there must community, teachers, parents, students and stakeholders to join together to help students get practice often experimental examinations of measuring Presenting the report of the test preparation of the Form 2013 to the parents of four academic school teacher at Francis Hope Wambura said Form Four this year According to the department of education at the middle school 168 students are expected to sit for the Form Four year 21 students have so far been registered due to absenteeism servants. Further reports have increased fees to pay for the exercise test was completed on 28 national linalotarajia next month seems sluggish where 40 students only ones who pay fees to date. |
Historia ya tafsiri
|