FCS Narrative Report
Introduction
Dates: Januari 01, 2012 hadi Machi 31, 2012 | Quarter(s): Kwanza |
S.L.P. 376
Mtwara
Simu: +255 787 193 774
+255 715 193 774
Nukushi: +255 23 2333 807
Barua Pepe:
Project Description
Mradi utawezesha kujenga uwezo kwa wadau tofauti wa maendeleo kuhusu mbinu na stadi za kukusanya taarifa na takwimu; kufanya uchambuzi, uandishi wa taarifa na utoaji wa mrejesho kwa wadau kuhusu mafanikio; mapungufu, changamoto na nini kifanyike ili kuimarisha mafanikio yaliyopatikana, kuboresha mapungufu yaliyojiri na yaliyopo na kutatua changamoto mbalimbali ili kuona kwamba Uwazi, Uwajibikaji na nidhamu ya matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma kwa ajili ya wakulima na wafugaji vinakuwepo kupitia DADPs na PADEP. Mradi utatekelezwa katika Halmashauri 6 za Wilaya na Manispaa za Mkoa wa Mtwara ambazo ni; Mtwara Manispaa, Mtwara Vijijini, Tandahimba, Newala, Masasi na Nanyumbu kwa muda wa miezi kumi na miwili (Mwaka mmoja) kuanzia Januari hadi Desemba, 2012.
Region | District | Ward | Villages | Total Beneficiaries |
---|---|---|---|---|
Mtwara | Mtwara Manispaa | - | - | 10246 |
Mtwara | Mtwara Vijijini | - | - | 10246 |
Mtwara | Tandahimba | - | - | 10246 |
Mtwara | Newala | - | - | 10247 |
Mtwara | Masasi | - | - | 10247 |
Mtwara | Nanyumbu | - | - | 10247 |
Direct Beneficiaries | Indirect Beneficiaries | |
---|---|---|
Female | 1863 | 18630 |
Male | 3726 | 37260 |
Total | 5589 | 55890 |
Project Outputs and Activities
2.1 Wawakilishi 60 wamepata uelewa juu ya dhana ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na rasilimali za Umma (PETS) za sekta za kilimo na mifugo DADPS/ PADEP) katika halmashauri 6 za wilaya za mkoa wa Mtwara
3.1 Kamati 6 za PETS zimeundwa na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) za sekta za kilimo na mifugo DADPs / PADEP katika mamlaka za serikali za Mitaa za Mkoa wa Mtwara umefanyika.
4.1. Kufanyika kwa uchambuzi wa taarifa na takwimu zilizokusanywa kutoka Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara na taarifa za mirejesho zimeandikwa na zimekamilika.
5.1. Mikutano 6 ya mirejesho ya taarifa za PETS imefanyika katika Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara kuhusu matumizi ya fedha katika sekta ya kilimo/mifugo kupitia DADPs/PADEP.
6.1. Kuchapishwa na kusambazwa kwa Mabango 1800, Vipeperushi 3000, Fulana 300 vyenye ujumbe wa PETS na kurushwa kwa vipindi 4 vya Radio kuhusu dhana ya PETS na kuongezeka kwa uelewa na ushiriki wa jamii.
7.1. Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara zimefanyiwa ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji mradi wa PETS kwa fedha za DADPs/PADEP
8.1. Kufanyika kwa mkutano shirikishi wa tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha walengwa/wadau 40 toka halmashauri 6 za wilaya manispaa za Mkoa wa Mtwara
2.1.1. Kufanya mafunzo ya PETS kwa wawakilishi na kubainisha kamati za kufuatilia matumizi ya fedha na rasilimali za umma (PETS ) kwa kila halmashauri 6 za wilaya / manispaa za mkoa wa Mtwara ifikapo Novemba 2011.
3.1.1. Kuchapisha na kusambaza Mbango 1800, Vipeperushi 3000, Fulana 300 vyenye ujumbe wa kuhamasisha jamii kufanya PETS na kurusha vipindi 4 vya Radio juu ya dhana ya PETS ifikapo Juni, 2012.
4.1.1. Kufanya ufuatiliaji na tathmni za maendeleo ya utekelezaji wa mradi na mwelekeo wa ufikiwaji malengo katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa 6 za Mkoa wa Mtwara.
2. Kuendeshwa kwa mafunzo ya kujengwa uwezo kwa wadau 60 tofauti wa maendeleo juu ya dhana ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) na kubainishwa kwa kamati za PETS kwa kila Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara.
3. Kuchapishwa na kusambazwa kwa wadau tofauti wa PETS; Mabango 1800, Vipeperushi 3000, Fulana (T-shirts) 183 katika Halmashauri 5 za Wilaya za Mkoani Mtwara na Manispaa ya Mtwara Mikindani.
4. Kufanyika kwa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji mradi na mwelekeo wake wa ufikiwaji malengo katika Halmshauri 5 za wilaya na manispaa ya Mtwara Mikindani.
2. Mafunzo kwa wadau tofauti kuhusu PETS:- (TZS. 7,860,000/=)
3. Kuchapisha na kusambaza machapisho tofauti:- (TZS. 5,462,000/=)
4. Ufuatiliaji na tathmini ya mawndeleo ya utekelezaji wa mradi:- (TZS. 746,000/=)
5. Ununuzi wa vifaa na samani mbalimbali ya uendeshaji mradi:- (TZS. 4,534,550/=)
Project Outcomes and Impact
2. Kuongezeka kwa uelewa na ushiriki wa jamii katika kufuatilia matumizi ya fedha na rasilimali za umma (PETS) zinazotengwa na Serikali kuinua sekta ya kilimo kupitia DADPs / PADEP.
2. Kuongezeka kwa maarifa, mbinu na stadi kwa wadau 60 tofauti wa maendeleo wa Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara katika kufanya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) hususan katika sekta ya Kilimo/Mifugo kupitia miradi ya DADPs/PADEP.
3. Kuundwa kwa Kamati 6 za Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) kwenye Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara.
4. Kusambazwa kwa machapisho mbalimbali yenye ujumbe na kuongezeka kwa uelewa wa jamii na mwamko wa kushiriki za Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara katika Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) katika sekta ya Kilimo/Mifugo na nyinginezo.
Lessons Learned
Explanation |
---|
Dhana na dhima ya PETS bado haifahamiki kikamilifu miongoni mwa watendaji/viongozi wa serikali pamoja na wananchi kiujumla. |
Wananchi wanahitaji kujengewa uwezo zaidi hususan katika ngazi za kata na vijiji ili waweze kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma katika maeneo na ngazi wanamoishi. |
Watendaji/viongozi wa serikali za mitaa bado wana mtazamo potofu kwamba kufanya ufuatiliaji wa matumizi na raslimali za umma (PETS) ni sawa na kufanya ukaguzi jambo ambalo sio sahihi. |
Challenges
Challenge | How it was overcome |
---|---|
Bajeti ya mradi kukosa (kusahaulika) kipengele cha posho ya kujikimu kwa washiriki wa mafunzo kwa kamati za PETS. | Kuendesha mafunzo katika vituo 3 badala ya 2 vilivyopendekezwa ili kuwasogelea washiriki na hivyo kutolazimu kuwalipa posho ya kujikimu. |
Watendaji/viongozi wa serikali za mitaa waliohudhuria warsha ya kuelezea malengo ya mradi kudai kulipwa posho kwa viwango vya serikali. | Kuwaelimisha na kuwaelekeza kwamba mfadhili (FCS) hazingatii viwango vya posho za serikali na kwamba wana mwongozo wa uombaji na utoaji ruzuku kwa wadau (AZAKi) na unapaswa kuzingatiwa. |
Washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo katika kufanya ufuatiliaji (PETS) kudai kiwango cha posho hakitoshelezi kukidhi haja na mahitaji ya hali ya maisha ya sasa. | Walielekezwa kwamba viwango vya malipo yote vilivyopo ni kwa mujibu wa bajeti na makubaliano ya Mkataba kati ya FCS na TCCIA Mtwara wa kutekeleza mradi husika. |
Linkages
Stakeholder | How you worked with them |
---|---|
Maafisa Kilimo, Mifugo, Mipango na Wachumi wa Halmashauri za wilaya/manispaa 6 za Mkoa wa Mtwara. | Kuhudhuria warsha ya kujenga uelewa na kuelezea malengo ya kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya Kilimo/Mifugo. |
Waandishi wa Habari | Kuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kutangaza/kuhabarisha wananchi kuhusu taarifa mbalimbali za mradi. |
Wawakilishi wa Asasi za Kiraia (AZAKi) | Kuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati hizo |
Waheshimiwa Madiwani | Kuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati hizo |
Wakulima na wafugaji | Kuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati hizo |
Future Plans
Activities Planned | 1st Month | 2nd Month | 3rd Month |
---|---|---|---|
Kufanya zoezi la kufuatilia matumizi ya fedha na rasilimali za umma PETS katika sekta za kilimo mifugo kupitia miradi ya DADPs / PADEP kwa kila halmashauri 6 za wilaya / manispaa za mkoa wa Mtwara. | xxxxxxx | ||
Kufanya uchambuzi wa taarifa na takwimu zilizokusanywa katika zoezi la PETS na kuandaa taarifa za marejesho kwa kila wilaya / manispaa za mkoa wa Mtwara ifikapo Desemba 2011 | xxxxxxx | ||
Kufanya ufuatiliaji na tathmini za maendeleo ya utekelezaji wa mradi na mwelekeo wa ufikiwaji malengo katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa 6 za Mkoa wa Mtwara. | xxxxxx | xxxxxxx | xxxxxxx |
Beneficiaries Reached
Direct Beneficiaries | Indirect Beneficiaries | ||
---|---|---|---|
Widows | Female | 75 | 750 |
Male | 225 | 2250 | |
Total | 300 | 3000 | |
People living with HIV/AIDS | Female | 34 | 340 |
Male | 24 | 240 | |
Total | 58 | 580 | |
Elderly | Female | 51 | 510 |
Male | 153 | 1530 | |
Total | 204 | 2040 | |
Orphans | Female | - | - |
Male | - | - | |
Total | - | - | |
Children | Female | - | - |
Male | - | - | |
Total | - | - | |
Disabled | Female | 17 | 170 |
Male | 51 | 510 | |
Total | 68 | 680 | |
Youth | Female | 30 | 300 |
Male | 90 | 900 | |
Total | 120 | 1200 | |
Other | Female | 1493 | 14930 |
Male | 2985 | 29850 | |
Total | 4478 | 44780 |
Events Attended
Type of Event | When | Lessons | Actions Taken |
---|---|---|---|
Mkutano wa upasahanaji wa Habari za Ruzuku toka FCS | 2008 | Namna ya kuomba ruzuku kutoka FCS kwa kuzingatia mwongozo | Kuomba ufadhili toka FCS kwa kuzingatia mwongozo na hatimaye kufanikiwa kufadhiliwa. |
Mafunzo ya Kusimamia Ruzuku ya Mradi (MYG) | Juni/Julai, 2011 | Namna ya kusimamia fedha za ruzuku toka FCS na kutekeleza shughuli za mradi kiufanisi. | Kusimamia fedha za ruzuku kwa mujibu wa taratibu na kutekeleza mradi kiufanisi sawa na mkataba uliosainiwa kati ya FCS na TCCIA Mtwara. |
Attachments
Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) - Tawi la Mkoa wa Mtwara tumeanza utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Ushiriki wa Jamii katika kufanya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) kupitia Mipango ya Kuendeleza Kilimo Wilayani (DADPs) na Mipango Shirikishi Jamii ya Kilimo na Mifugo (PADEP) ambayo ni sehemu ya mipango, mikakati na miradi ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (PKSK) au maarufu ASDP.
Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Mtwara za; Tandahimba, Newala, Nanyumbu, Mtwara Vijijini, Mtwara Manispaa na Masasi kwa muda wa miezi kumi na miwili (mwaka mmoja). Mradi huu unafadhiliwa na taasisi ya The Foundation for Civil Society ya Dar Es Salaam kwa gharama ya fedha za shilingi ya Kitanzania zipatazo Milioni Arobaini na Tano (TZS. 45,000,000/=). Mradi umeanza kwa shughuli za; Kuendesha warsha kwa viongozi/watendaji wa Serikali za Mitaa ambao ni, Maafisa Kilimo (W), Maafisa Mipango (W), Wachumi, Maafisa Maendeleo ya Jamii na Wakurugenzi na/au wawakilishi wao ambapo walielezewa malengo ya mradi na kuongezewa uelewa kuhusu dhana na dhima ya PETS. Jumla ya Watendaji/Viongozi 44 tumeweza kuwafikia kati ya 60 waliotarajiwa.
Vilevile tumeeendesha mafunzo kwa wadau tofauti 62 wa maendeleo kutoka katika halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara ambazo ndizo maeneo ya utekelezaji wa Mradi husika. Mafunzo hayo yaliweza kujenga uwezo kimaarifa, mbinu na stadi kwa wadau hao katika kufanya PETS kwa kuwezeshwa namna ya kukusanya taarifa, kuzichambua, kuandaa ripoti ya mrejesho na jinsi ya kufanya Mkutano wa Mrejesho na mbinu za kufanya ushawishi na utetezi wa matokeo ya zoezi la PETS. Mradi umeanza kutekelezwa katika kipindi cha robo ya kwanza katik ya robo nne zitakazotekelezwa katika mwaka mzima wa utekelezaji mradi husika.