Injira
TANZANIA SCIENCE JOURNALIST ASSOCIATION

TANZANIA SCIENCE JOURNALIST ASSOCIATION

DAR ES SALAAM, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Iran kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Sayansi

Elizabeth Mlay (kulia kwa waziri ) mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Dk. Mohammad Baqer Khorramshad

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu ICRO amesema ustawi wa kipekee wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa kisayansi ni mfano mzuri wa kuigwa na nchi za Kiafrika.

Dk. Mohammad Baqer Khorramshad alisema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania Profesa Makame Mbarawa,

Alisema ustawi wa kasi wa Iran katika uga wa sayansi na teknolojia ni natija ya juhudi na ubunifu wa wasomi na wanasayansi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha amesisitiza kuhusu azma ya ICRO ya kuimarisha uhusiano na Tanzania na kuongeza kuwa shirika hilo litatoa msaada wa masomo kwa wanafunzi 7 wa Tanzania bara na watatu kutoka Zanzibar.

Khorramshad aidha ameashiria uwezo wa Iran katika sekta kama vile utamaduni wa Kiislamu, ustaarabu, nano teknolojia, mawasiliano ya satalaiti na kilimo na kusema Iran iko tayari kubadilishana uzoefu wake huo na Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania Profesa Makame Mbarawa amesisitiza azma ya nchi yake ya kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Alisema kwa kuzingatia mahitajio mengi ya Tanzania katika sekta mbali mbali, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaweza kuwa chanzo kizuri cha kupata uwezo wa kisayansi.

 

17 Mutarama, 2013
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.