Fungua
Tanzania Rehabilitation Organization

Tanzania Rehabilitation Organization

Dodoma City, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Help a KID project in Dodoma

Tanzania Rehabilitation Organization (tareo2011@yahoo.com)
31 Januari, 2013 23:55 EAT

Hii ni nchi yetu watanzania, sisi sote kwa namna moja ama nyingine tumepitia shida, tabu na matatizo ya kila aina, lakini twaweza kuwa hatuko katika hali hiyo kwa namna ile. Jiulize, na fikiria ni kwa jinsi gani uliumia na kuhangaika kutafuta namna ya kutoka katika hali ile uliokuwa nayo.

Tuna vijana wengi kwa sasa wanaopitia shida na matatizo mengi sana, wengine hawana pesa ya kulipa karo ya shule, hawana pesa ya kujipatia mahitaji ya shule. Kwa nafasi ulionayo ni kwa namna gani waweza saidia angalau kuokoa maisha ya kijana mmoja?

kwa umoja wetu tunaweza kuleta mabadiliko kwa jamii yetu na nchi kwa ujumla. Tumia nafasi ulionayo angalau uyaguse maisha ya kijana ambaye anasubiri uwepo wako.

Mradi (Help a KID) ni mahususi kwa vijana ambao hawana uwezo kabisa wa kumudu gharama za shule na pia mavazi. Tunaomba ndugu mtanzania tuwe na utamaduni wa kujitegemea na sio kusubiri wazungu waje watusaidie. tuchangie kiasi chochote ulichonacho ili kiweze kuleta mabadiliko ya kweli. pesa yote itakayopatikana itawafikia walengwa.

Kwa mawasiliano na namna ya kuweza kutoa mchango wako tafadhari wasiliana nasi kwa mawasilino yanayopatikana kwenye tovuti hii.

 

imetolewa,

Mr. PETER. T.S .

Chairperson-Tareo, Tanzania

 


Ongeza Ujumbe Mpya (Ficha)

Ikipakia...
Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.