SHOP KATIKA UFUATILIAJI WA FEDHA ZA UMMA ZILIZOTENGWA KWAAJILI YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU
Asasi ya SHOP kwa sasa inatekeleza mradi wa kuimarisha uwajibikaji wa viongozi na wananchi ndani ya serikali za mitaa katika kata tatu za Mwakibete, Mwasanga na Tembela jiji la Mbeya. mradi huu umefadhiliwa na the Foundation For Civil Society. katika utekelezaji wa mradi huumpaka sasa asasi imefanikiwa kuendesha mafunzo ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma katika sekta ya elimu kwa kamati za shule za msingi na bodi za sekondari pia kufanya mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa ya kata za Mwakibete, Mwasanga na Tembela Jiji la Mbeya juu ya uwajibikaji na utawala bora.
Vilevile asasi ilifanikiwa kuunda kamati ya ufuatiliaji mara baada ya mafunzo ya ufuatiliaji kufanyika. kamati hiyo ya ufuatiliaji yenye wajumbe 21 wakiwemo waandishi wa habari 2 wajumbe 10 kutoka kamati za shule za msingi na bodi za sekondari na wajumbe 8 ambao ni wanachama wa asasi kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji mashuleni.
Mambo mengi yameweza kubainika wakati kikosi kazi hicho kilipokuwa kikitembelea shule za msingi na sekondari za serikali zilizopo katika kata za Mwakibete, Mwasanga na Tembela. mambo hayo ni kama vile
- Shule ya msingi ya Mwasanga kuwa na tatizo la vyoo, ambapo idadi ya wanafunzi ni 715 na matundu ya choo wanayotumia ni 2 hivyo kusababisha mrundikano wa wanafunzi mrangoni wakisubiriana kwa vurugu kubwa. Katika tatizo hili wananchi wa kata hiyo ya Mwasanga walilalamika sana na kusema wamekuwa wakichanga michango ya ujenzi wa vyoo kila Mwaka bila ya mafanikio ya kuona vyoo vikijengwa.
- Pia tatizo la Mbao za matangazo kutokuwepo na kuwepo eneo lisilo la wazi limeonekana ni tatizo linalojirudia katika shule zote.
- Katika shule zote idadi ya wanafunzi ni kubwa ukilinganisha na madarasa yaliyopo isipokuwa shule moja tu ya sekondari ya Mwasanga bado inawanafunzi wa chache kwani ndo kwanza Imeanza kidato cha nne mwaka huu.
- Katika shule za sekondari zote mbili, Mwasanga na Mwakibete kuna uhaba wa walimu wa sayansi.
- Walimu wa shule zote za msingi na sekondari wamelalamikia tatizo la fedha za kaptation kuchelewa kufika kwa wakati pia haziji idadi yote kama inavyotakiwa.