
Wa kwanza katika Picha ni Ndugu Michael kisonzera,akiandaa malpo ya Nauli za washiriki wa semina ya Kujengea uwezo.

Ndugu,Lawrance Chuma kutoka AGENDA PARTICIPATION,mwezeshaji wa mafunzo ya kujengea uwezo wanachama wa Nyakitonto Youth for Develpment Tanzania.Anawezesha somo la kupanga mapato na matumizi kwa kuzingatia vipaumbele vya asasi kwa jamii.

Mh.Diwani,Ndugu Maftah Baila akisaini kitabu cha wageni katika ukumbi wa Redcross tayari kushiriki mafunzo yaliyoendeshwa na Nyakitonto youth for development Tanzania na Kufadhiliwa na FCS kwa ajili ya kujengea uwezo viongozi na wanachama wa NYDT.

Bi.Christina Stephan akisiliza mafunzo ya Kujengea uwezo wanachama wa NYDT

Bi Terezia Phabian ,Muuza dawa za Binadamu katika kijiji cha Mugombe akiuliza namna ya Kuzipata za Misoprostol kwa ajili ya kuwauzia wananchi huko kijijini.

Mkunga akiomba apatiwe dawa za miso na Groves kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na watoto ambao ni walengwa wa dawa za misoprostol

Binti aliyehudhuria mafunzo akiomba ufafanuzi wa Idadi ya Vidonge vya kuwapa walengwa wa Dawa za miso.

Mkunga wa jadi,akiomba ufafanuzi juu ya Nani ni mlengwa wa dawa za Miso. Alijibiwa na mwezeshaji kuwa ni mama aliyejifungua,na kupewa dawa.

Muuza dawa Katika semina ya Miso,akinukuu maelekezo ya Namna ya kutumia dawa ya miso ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Washiriki wa semina ya Taarifa sahihi za Misoprostol katika ukumbi wa IRC-Nyakitonto wakisiliza kwa makini.