
Terezia akiomba na kusisitiza matumizi ya dozi sahihi,hii ni baada ya kutoa ushuhuda kuwa wakina mama wengi hawana uwezo,hivyo huamua kununua dozi nusu,amesisitiza hatauza dozi pungufu.

Mkunga akiongeza jambo juu ya kumsaidia mama anayejifungua.pamoja na mafunzo Ameomba apate dawa na Mipira(Gloves)za kumsaidia mama.alisisistiza kuwa anamiaka 18 akiwa mkunga hivyo anauzoefu na atautumia kwa ajili ya kuendelea kumkinga mwanamke na kuokoa maisha yake.

Mama mwenye mtoto akisisitiza na kutoa ushuhuda wa namna alivyosaidiwa na Dawa za miso kuokoa maisha yake na mwanae kwa kutumia Dawa za MIso.

Mheshimiwa Diwani wa kata ya Nyakitonto-NDUGU MISHITA FILIPO. Akiwapongeza washiriki na kuwaomba wawe Mabarozi wa Kutoa Taarifa kwa wanawake wenzao ambao hawakushiriki semina.

Mganga mfawidhi-Kituo cha afya nyakitonto akifatoa data za Vifo vya mama wakiti akijifungua.alisisitiza Tumukinge mama sana kwa kuwa kifo cha kutoka damu ni cha huzuni sana.

Nesi muuza dawa akitoa maoni juu ya upatikanaji wa dawa za miso.ameahidi kuzinunua na kuziuza ili kuokoa maisha ya mama.

Mkunga wa muda mrefu akiomba aonyeshwe samples za dawa ya miso ili azifahamu.


