Fungua
Mzizi Cultural Troup

Mzizi Cultural Troup

manispaa ya Iringa, Tanzania

Wadau na wapendwa wetu...jeuri ya kujitolea katika kufungua kituo cha habari imetokanana na michango ya wanachama ya kila mwezi na mapato yatokanayo na kukodiwa ktk maonyesho ya sanaa na wadau mbali mbali! wadau wetu katika envaya Mzizi tunawaalika wote mtakaoona kuna haja ya kutumia sanaa ktk kutoa elimu ya mambo mbalimbali kuwa mzizi tunafanya shughuli hizo! tunaomba ushirikiano wenu ktk kutumia kikundi chetu ili tuweze kutimiza matarajio yetu ktk kusimamia mabadiliko chanya kwa vijana!
Habari wapendwa ktk Envaya! mzizi cultural troup tumefungua kituo cha habari na sanaa kwa vijana katika kata ya mwangata kalenga road! lengo kubwa ni kusogeza jirani na vijana huduma na taarifa juu ya afya ya uzazi na haki kwa vijana, mategemeo yetu ni kuwa na vipindi maalum kila wiki kwa makundi maalum kujadiliana juu ya afya ya uzazi na haki! tunategemea pia kuwa na siku maalum kwa wiki ambayo vijana wadogo watashindana kuandika INSHA juu ya afya ya uzazi na haki kwa vijana na mshindi atazawadiwa! Ndugu zetu ktk envaya eleweni kuwa mzizi haina mfadhili yeyote ktk kutenda haya!
Mzizi cultural troup Mwezi huu tar 7 hadi 10 tulialikwa kushirikiana na Mtandao wa vijana wanaoishi na VVU Tanzania NYP+ Tumefanya tamasha kubwa mjini kyela lililoshirikisha mbio za baiskeli kwa wasichana na mpira wa miguu kwa timu nane za wilaya ya kyela mkoani mbeya! tamasha lilikuwa na lengo la kuwapa nafasi vijana kukutana na kujadiliana juu ya afya ya uzazi! walipata nafasi ya kuchanga uzoefu wao juu ya afya ya uzazi na haki kwa vijana na kuibua mbinu mbalimbali za kujikinga na VVU!
Sanaa huibua hisia za jamii zilizojificha, hutoa wigo mpana wa tafakari zinazotoa mwelekeo wa jamii kuchambua vyanzo vya tatizo,sababu za tatizo na kuipa nafasi jamii kutafuta njia za kulitatua!