LENGO KUU LA MUYODE
Kutoa mchango katika juhudi za Serikali katika kuikwamua jamii katika matatizo ya kielimu, mazingira, uchumi, haki na kuwaepusha na magonjwa mbalimbali ya ngono hasa UKIMWI.
MADHUMUNI YA MOYODE.
- Kuunganisha nguvu na juhudi za jamii katika kujiletea maendeleo endelevu.
- Kuiwezesha jamii kutambua thamani yake katika kutoa mchango wao katika kutatua matatizo mbalimbali.
- Kuunganisha jamii na wataalamu mbalimbali ili kupata mbinu bora za kupambana na umaskini na maradhi.
- Kuanzisha program zitakazoifunza jamii kuwa raia wema na wenye maadili mema.
- Kuinua vipaji vya watoto na vijana katika fani za sanaa, michezo na burudani kwa kuwa na eneo maalumu kwa ajili ya shughuli hizo.
- Kushirikiana na wataalam, asasi za kiraia na za serikali ndani na nje ya nchi ili kusaidia jamii ya kitanzania.
- Kuendesha program zenye kuinua hali za kiuchumi, mazingira bora na zenye kubadili tabia hatarishi kwa vijana na watoto kama matumizi ya dawa za kulevya, ngono zisizo salama na ubakaji.
6 Novemba, 2014