Log in
Jumuiya Endelevu Bagamoyo

Jumuiya Endelevu Bagamoyo

Bagamoyo, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

JEBA Society, ni kifupisho cha neno Jumuiya Endelevu Bagamoyo. Lilianzishwa mwaka 2000 na kupata usajili wa kisheria mwaka 2001, na kupewa cheti namba SO.11190. Lilianzishwa na vikundi vya kijamii kutoka wilaya ya Bagamoyo mjini na jimbo la Chalinze. Lengo kuu lilikuwa ni kuondokana na uonevu waliokuwa wakipata wakati misaada iliyokuwa inawalenga wao kupitishiwa halmashauri ya wilaya na kuwekewa vikwazo na mwisho wa siku huduma hizo kuishia kwa baadhi ya watu wasio walengwa. mf. hai ilikuwa ni fedha zilizokuwa zikitolewa na shirika la UNDP, kusaidia kuwajengea uwezo vikundi.

  Tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hii imepata mafanikio makubwa sana. Moja ya mafanikio makubwa iliyopata ni pamoja na kuongeza vikundi vya kijamii kutoka 14 wakati huo na kufikia 40 kwa sasa. Vile vile Jumuiya iliweza kuanzisha chombo chake cha fedha kwa ajili ya kuwapatia walegwa wake mitaji katika shughuli zao. Na mwisho kabisa Jumuiya iliweza kujenga mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani ya wilaya ya Bagamoyo na nje ya wilaya. mf. mashirika ya kimataifa km MS/ACTION AIDTZ, JICA na wafadhili wengine muhimu kama The Foundation for Civil Society, CRS, REPOA n.k.