Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

 

 

MABARAZA YA WAZEE VIJIJINI/MITAANI

(KAMA ILIVYO AINISHWA KATIKA SERA YA TAIFA YA WAZEE 2003)

 

Tafsiri/Maelezo

  • Sio ya Kisiasa na kila Mzee ana haki ya kushiriki.
  • Sio Asasi zisizo za Kiserikali (NGO,CBO,FBO, CSO nk).Kwa maana nyingine mabaraza hayasajiliwi kama NGO.Yakisajiliwa, kisheria hayatatambulika tena kama Mabaraza ya wazee bali yatatambulika kama Asasi zisizo za kiserikali
  • Ni ya Kijamii nayanaundwa Vijijini/Mitaani.
  • Ni ya kujitegemea na huwapa wazee sauti na nguvu ya kujadili mambo yao kwa utulivu, Uhuru na umakini.
  • Hushawishi na kushauri watoa maamuzi kuhusu mambo yanayogusa maisha ya kila siku ya wazee.
  • Huendeshwa kidemokrasia zaidi
  • Yanaendeshwa na wazee wenyewe kwa ajili ya wazee.
  • Wajumbe wote ni wakujitolea
  • Wajumbe huamua ajenda zao wenyewe,hushirikishana taarifa mbalimbali na huibua hoja zinazowahusu wao wenyewe na wategemezi wao.
  • Ni mfumo unaohusisha wazee katika ngazi ya kijiji/Mtaa.

 

Kwa nini kuwe na mabaraza ya wazee kijijini?

  • Kuishauri na kuishawishi serikali na wanasiasa kuboresha huduma kwa wazee na wategemezi wao.
  • Kuimarisha utambuzi wa Pamoja wa wazee na kuwapa wazee hali ya kujiona nao ni sehemu muhimu ya jamii.
  • Kujadiliana na wawakilishi wa kikatiba na kujitolea kama wawakilishi wa mambo ya yanayo wahusu wazee.
  • Kuboresha mawasiliano kati ya wazee na serikali katika hali inayokubalika Kikatiba,halmashauri/Manispaa, Idara ya Ustawi wa jamii, Maendeleo ya Kijanmii,afya, Polisi, n.k
  • Kupiga kampeni na kutetea wazee kuhusu masuala ya wazee kwa mashirika , serikali, taasisi za kidini, na watoa huduma wengine wowote.

Wajumbe.

  • Ni wazee wote wenye lengo la kutafuta kuboresha hali ya maisha ya wazee wote katika jamii.
  • Ujumbe ni automatiki. Kigezo ni kuwa mzee kuanzia miaka 50. Japokuwa hii inaweza kubadilika kulingana na mazingira au mahitaji Fulani.
  • Watendaji wa serikali ambao ni wazee wanaoishi katika maeneo hayo wanaweza kuwa wajumbe kwa kigezo cha umri na si nafasi zao serikalini.
  • Watendaji wa serikali watakaoalikwa wanaweza kuwa na sauti kama wajumbe wengine.

Uongozi.

  • Kila baraza litakuwa na Mwenyekiti, makamu wa Mwenyekiti , Katibu na mtunza Hazina. Nafasi hizi kupendekezwa na kupigiwa kura na wajumbe.
  • Wajumbe wawili (Me na Ke) .Hawa ni wakusanya takwimu (OPMG – Older People`s Monitoring Group), kero za huduma za afya,Kipato,haki mbalimbali za wazee
  • Uchaguzi hufanyika siku ya mkutano wa uchaguzi kwa tarehe iliyokubalika.
  • Ili mzee aweze kuchaguliwa ni lazima apendekezwe na wajumbe na si kujipendekeza mwenyewe.
  • Viongozi ni lazima wawe wazee wenyewe na ambao wanakubalika katika kijiji na wenye nia hasa ya kujitolea kuwakilisha wazaee wenzao.
  • Baraza litapendekeza kikundi cha watu wachache ambao watasilisha mapendekezo yao na mipango kwa wahusika
  • Kundi hili litakalopendekezwa linaweza kuwa la wanaotunza wagonjwa majumbani (HBCs), Wafuatiliaji wa mambo ya sheria (Paralegals), Wafuatiliaji wa masuala ya wazee (OPMGs), waelimisha rika , n.k.

Utendaji

  • Baraza linaweza kutumika na serikali( Wabunge,wanasiasa,watendaji, n.k) na taasisi mbalimbali kama chanzo cha habari za wazee, takwimu, na mambo kadhaa ya wazee kabla ya mipango, uboreshaji huduma na utekelezaji wa mambo yanayohusu maisha ya wazee kuanzia kijiji hadi taifa.
  • Baraza linaweza pia kuwa kama sehemu ya kiutendaji ya Shirika au mashirika ya wazee yanayofanya kazi kusaidia wazee kijijini au wilayani.
  • Wajumbe hukutana kubadilishana mawazo na kupeana taarifa muhimu za maisha yao ili kuleta mabadiliko.
  • Baraza huikutana pia kuzungumzia mambo/ kero zinazogusa maisha ya wazee katika eneo lao kama vile afya, huduma za matibabu, pensheni kwa wazee wote na namna nyiongine za kipato kwa wazee, n.k.
  • Baraza katika kila wilaya litafanya kazi kusaidia au kutaarifu serikali, mashirika ya kuhudumia wazee, jamii na wazee kuhusu mamboa yanayohusu maisha ya wazee.

Mikutano.

  • Inaweza kuamliwa na wajumbe lakini mara nyingi huwa mara moja kwa mwezi.
  • Inaweza kuwa ya dharula linapotokea jambo kama msiba/mauaji, uchsaguzi wa dharula, n.k
  • Itaitishwa na Katibu kwa kushirikiana na Mwenyekiti.
  • Serikali ya kijiji au kata au wilaya inaweza kuhudhuria ili kuweza kujua na kutoa majibu juu ya matatizo yanayokabili wazee wa kijiji/Kata/wilaya husika.

Majukumu.

  • Kutoa changamoto,kushauri na kupendekeza mambo kwa ajili ya haki na huduma za wazee.
  • Kuchagua viongozi na wafuatiliaji.wanaochaguliwa wanajukumu la kutoa taarifa kwa wazee wote kuhusu maendeleo ya jukumu walilopewa.
  • Kuboresha na kupeana maarifa, uzoefu na uwezo wa wazee katika kutatua masuala mbalimbali ya msingi kama huduma za afya , usafiri, miundombinu, kushughulikia kesi mbalimbali, n.k.
  • Pamoja na kampeni kwa ajili ya usaidizi, wanaweza kuwa na shughuli za kijamii na kuandaa mikutano ya kuelimisha jamii, kufurahi, mazoezi, kukaribishwa wageni na kupata taarifa mbalimbali.
  • Kuwa kama nguzo muhimu ya kiutendaji ya mashirika   au taasisi za kusaidia kuboresha maisha ya wazee na huduma; hata serikali )informal structure).
  • Kusaidia kuboresha utambuzi wa mabvo mbalimbali yanayowakabili wazee.

Namna ya kuendesha mabaraza.

  • Itisha mkutano wa wazee wote kijijini.
  • Amua/ tengeneza vipaumbele vya mambo ya msingi yanayohitaji kuboreshwa kama afya na matibabu, usafiri, ulinzi, kipato, UKIMWI,uelimishaji rika.
  • Andaa madhumuni kuhusu masuala hayo au vipaumbele.
  • Hakikisha kuna uelewa wa kutosha kuhusu kilichoandikwa katika miongozo ya serikali kama sera, mikakati, mipango na bajeti. Fuatilia habari hizi kwa wataalamu na watendajiwa serikali.
  • Jiwekee malengo – unahitaji nini kutoka katika sekta Fulani? Utendaji? huduma?
  • Chagua viongozi kwa demokrasia.
  • Saidia wajumbe na vuiongozi kubeba na kutekeleza majukumu yao na kufikia malengo. Toa majukumu mapya kama yapo.
  • Andaa utaratibu na muundo na kufanyia kazi mambo yanayoleta migogoro au migongano itokanayo na uelewa ili kujenga mahusiano na uelewa wa Pamoja . Hapa ndipo mahali muhimu pa kuandaa masuala ya Pamoja kama sherehe,n.k.
  • Kubalianeni kipindi cha mikutano na siku ya kukutana. Itakua vema kutumia eneo moja na muda huohuo uliokubaliwa kila mwezi. Hii ni tofauti na mikutano ya dharula. Hii itarahisisha wajumbe kujua lini wanakutana bila hata kupewa taarifa. Kwa mfano mnaweza kuamua kukutana shuleni kila jummosi ya kwanza ya mwezi

MUHIMU

KUIMARISHA MABARAZA

  1. Mabaraza ya wazee yatakutana kila baada ya miezi mitatu:-
  • Januari - March
  • April – June
  • July – September
  • October – December.

         (Idara ya Ustawi wa Jamii Wilaya itafuatilia muhtasari wa        kila kikao kwa kila robo mwaka)

  1. Baraza linaweza pia kukutana kwa dharula kutokana na masuala muhimu ya wazee yatakayojitokeza kama ajenda ya lazima.
  2. Mwenyekiti/Katibu ni lazima kutunza dondoo za mikutano yote kwa manufaa ya rejea hapo baadaye.Kila Baraza la kijiji lina watakwimu wawili (Me na Ke) hawa wanajulikana kama OPMG (Older People Monitoring Group) au OCMG (Older Citizens Monitoring Group): na watatambuliwa na uongozi wa Kijiji, Kata na Wilaya.
  3. OPMG/OCMG wamechaguliwa kwa kupigiwa kura na mabaraza ya wazee katika vijiji.
  4. Kazi ya OPMG/OCMG ni kukusanya taarifa na takwimu mbalimbali na hususani kuhusu huduma za afya kwa wazee katika viyuo vya afya vya serikali.
  5. Jukumu la pili la OPMG/OCMG ni kutembelea Wazee na kujaza fomu maalum kuhusu uelewa wa wazee kuhusu taratibu za mchakato wa kuomba mikopo kwa ajili ya kukuza kip[ato kwa wazee.OPMG/OCMG (Me na Ke) watajaza fomu moja (Afya /Kipato) kwa Pamoja wakishirikiana kupata taarifa sahii kila mwezi toka kwa wazee wote.
  6. Kila watakwimu (2) watafanya ufafanuzi wa taarifa/takwimu walizokusanya katika kijiji chao kuhusu masuala ya wazee.
  7. Katika ngazi ya Kata , watakwimu (OPMG/OCMG) wa vijiji wote watakutana mara moja kila mwezi.(Watakubaliana wenyewe tarehe ya mkutano kila mwezi)
  8. Kila watakwimu wa kijiji watahudhulia katika kikao cha watakwimu wa Kata wote wakiwa na fomu za taarifa/takwimu zao.
  9. Kwa Pamoja watakwimu wa Kata watafanya majumuisho ya takwimu za kila kijiji na kupata tafsiri na takwimu za kata nzima.
  10. Tafsiri za majumuisho ya Takwimu za Kata nzima itatumika kama ushahidi wa uelewa wa Wazee na changamoto zinazowakabili.
  11. Baadhi ya changamoto zilizo ndani ya uwezo wa baraza la Wazee zinajadiliwa na Baraza la Wazee na kupatiwa utatuzi.
  12. Huduma zinazowezekana kuchangiwa na jamii zitashughulikiwqa katika ngazi ya kijiji.
  13. Changamoto zilizo nje ya uwezo wa kijiji na baraza la Wazee yanayopelekwa katika ngazi ya Kata (WDC) na mwakilishi wa Kata wa Wazee katika Baraza la Kata.

Imeaandaliwa na

Peter Alexander Mwita

Programme Manager

Morogoro Elderly People`s Organization (MOREPEO)

Boma road, Riti Area, Ushirika Building,Morogoro,Tanzania.

+255 785 938891

+255 622 938891

+255 759 119798

29 Desemba, 2015
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

Morogoro Eldrely People`s Organization (MOREPEO) (Boma road, Riti Area, Ushirika Building,Morogoro,Tanzania) alisema:
God bless you MOREPEO for the GREAT work, purposely for Older people in Morogoro Region and Tanzania
29 Desemba, 2015

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.