Fungua
LUSHOTO SECONDARY SCHOOL

LUSHOTO SECONDARY SCHOOL

lushoto, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Upinzani Syria kushiriki mazungumzo

Sunday, 19 January 2014
Imetumwa kwenye Jamii

A UN report has put the number of refugees fleeing Syria at more than a million. Around half are children

Baada ya mjadala mkali, kundi la upinzani nchini Syria limekubali kuhudhuria mazungumzo ya amani mjini Geneva wiki ijayo.

Uamuzi huo ulipokelewa vyema na wafadhili wake wa Magharibi waliosema ni hatua muhimu huku wakionyesha matumaini katika mazungumzo hayo.

Mataifa ya magharibi yenye uwezo mkubwa yamekuwa yakiushinikiza upinzani huo kushiriki katika mazungumzo hayo ambayo pia yatashirikisha serikali ya syria.

Swala la iwapo kuna umuhimu wa kuhudhuria mazungumzo hayo yaliugawanya upinzani huo huku wengi wa wanachama wa kundi hilo wakiamua kujiondoa.

Mwandishi wa BBC amesema kuwa kutakuwa na maswala mengi kuhusu vile wawakilishi wa upinzani huo walivyojitayarisha.

Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amepongeza uamuzi wa upinzani wa Syria kwenda kwa mazungumzo nchini Switzerland.

Lengo la mkutano ni kuona ikiwa inawezekana kuunda serikali ya mpito, ili kumaliza mzozo wa Syria.

Mgogoro huo wa miaka mitatu, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000(P.T)

Asilimia 98 wasema Ndio kwa katiba Misri

Sunday, 19 January 2014
Imetumwa kwenye Jamii

Kamati ya tume ya uchaguzi iliyotangaza matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya

Mamlaka nchini Misri imetangaza kuwa katiba mpya ya taifa hilo imeungwa mkono na 98.1% ya watu waliopiga kura katika shughuli ya kura ya maamuzi wiki jana.

Serikali hiyo inayoungwa mkono na jeshi,imesema kuwa hatua hiyo ni mwanzo mpya wa taifa la Misri.

Lakini vuguvugu la Muslim Brotherhood lililosusia kura hiyo limesema kuwa,asilimia 40 ya watu ambao hawakuinga mkono inaonyesha wazi kwamba shughuli hiyo ilifeli.

Katiba hiyo itachukua mahala pa sheria zilizowekwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi ambaye aliondolewa madarakani mwaka uliopita.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry ,amesema kuwa demokrasia ni kuwepo kwa zaidi ya kura moja ,huku akitoa wito kwa serikali kuidhinisha haki na uhuru ambao katiba hiyo inapigania.

Idadi ya waliojitokeza ilikuwa 38.6% ya watu milioni 53 wenye kadi za kupiga kura.

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya ni hatua ya serikali kutaka kuhalalisha hatua ya kumwondoa mamlakani Morsi mwaka jana.

Watu kadhaa walifariki kwenye ghasia zilizotokea wakati kura ya maoni ilipokuwa inafanyika.(P.T)

Ayman Mjengwa...

Sunday, 19 January 2014
Imetumwa kwenye Jamii

Mtoto wa mdogo wangu wa baba mkubwa Raphael Mjengwa. Pichani pia ni shemeji yangu, mke wa Salim Mjengwa. Salim na mkewe wanaishi Songea na wamenikaribisha chai nzito ya asubuhi.(P.T)

Good morning Songea, Good morning The World. .!

Sunday, 19 January 2014
Imetumwa kwenye Jamii

Mahenge, Songea Town, Tanzania.(P.T)

Serikali yawabeba waliofeli kidato cha pili

Sunday, 19 January 2014
Imetumwa kwenye Jamii

The Minister for Education and Vocational Training, Dr Shukuru Kawambwa

Wakati Watanzania wakisubiri matokeo ya kidato cha pili mwaka 2013, imebaini kuwa Serikali imetoa agizo kwamba wanafunzi wote waliofeli mtihani huo kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, huku wakisoma mafunzo ya kurudia mtihani wa kidato cha pili.Licha ya matokeo hayo kutotangazwa hadi sasa, imebainika kuwa waliofaulu mtihani huo uliofanywa Oktoba 7 hadi 21 mwaka jana ni asilimia 62 tu, asilimia 31 wakitakiwa kukariri (kurudia) kidato cha pili mwaka huu, huku asilimia saba wakishindwa mtihani huo kwa mara ya pili.

Jumla ya wanafunzi 531,457 walitajwa na Wizara ya Elimu mwaka jana kuwa watafanya mtihani huo.

Uamuzi huo wa Serikali ni tofauti na ule uliotolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa Novemba 4, mwaka 2012, kwamba kuanzia wakati huo mtihani wa kidato cha pili utakuwa ni wa mchujo na kwamba atakayefeli atatimuliwa.

Dk Kawambwa alisema matokeo ya mtihani wa kidato cha pili yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama 30.

Alisema mtahiniwa ataruhusiwa kukariri kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi.

Gazeti hili limeiona barua iliyoandikwa Januari 16 mwaka huu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusainiwa na Katibu Mkuu wake, Profesa Sifuni Mchome, kwenda kwa wadau wa elimu nchini, wakiwamo maofisa elimu wa mikoa na Chama cha Wamiliki wa Vyuo na Shule Binafsi (Tamongsco).(P.T)

19 Januari, 2014
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

Herman Joseph (Lushoto) alisema:
THAT IS THE "BIG RUSULT NOW"
23 Februari, 2014

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.