Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

LINGONET kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society imetekeleza mradi wa Kuimarisha uhusiano wa wananchi na wabunge majimboni kwa kufanya midahalo katika majimbo matatu ya LindiMjini ,Mtama na Mchinga,midahalo hii ilihusu Mchakato wa Katiba mpya,Utawala bora,Usawa wa kijinsia na Mabadiliko ya tabianchi.

midahalo ilifanyika katika vijiji vya Mtama,Nyangao,Madangwa,Mnazimmoja,Ng'apa,Mchinga,Milola,Mitwero na Lindi mjini,watu mbalimbali walihudhuria na kutoa michango yao ya mawazo katika mda husika ambazo zilitayarishwa na kuwasilishwa na wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya wilaya ya Lindi,pia midahalo hii ilihudhuriwa na madiwani,watendaji wa kata na vijiji na kupata bahati ya kufunguliwa na Mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi,Mheshimiwa Mbunge wa viti maalumu mkoa wa LINDI na katibu tawala wa wilaya ya Lindi

LINGONET pia kwa uhisani wa Jukwaa la katiba Tanzania iligawa nakala za katiba kwa wananchi kufuatia hoja katika midahalo hii kuwa ingawa wanajadili katiba wengi wao hawajawahi kuiona katiba iliyopo hivyo ingekuwa bora wakapata katiba iliyopo ili waweze kutoa maoni yao kwa ufasaha zaidi

 

MABARAZA YA AZAKi YA WILAYA

Mwezi august 2013 kuanzia tarehe 27-29 LINGONET iliendesha mabaraza ya AZAKi katika wilaya ya LINDI

Katika kuhakikisha jamii inashiriki ipasavyo katika mchakato wa katiba LINGONET kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society (FCS) iliunda mabaraza ya AZAKi katika majimbo yote ya matatu ya wilaya ya Lindi yaani Mtama,Mchinga na Jimbo la Lindi Mjini.

mabaraza haya yalikaa kwa siku tatu katika kata za Nyangao kwa jimbo la Mtama ,kata ya Mchinga kwa jimbo la Mchinga na Jimbo la Lindi Mjini likakaa katika ukumbi wa PRESS club lindi mjini na kuipitia na kuichambua rasimu ya katiba hatimae wajumbe wa mabaraza walitoa mapendekezo yao na kuwasilishwa katika tume yamabadiliko ya katika kama ilivyoelekezwa na Tume

 MRADI WA WAPE HAKI WENGI WASIO NA SAUTI

kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la SWEDEN (SIDA) LINGONET imesaini mkataba wa nyongeza wa miezi 18 kuanzia julai 2013 mpaka Disemba 2014 kutekeleza mkataba wa wape haki wengi wasio na sauti wa Tanzania kwa kushirikiana na SAVE THE CHILDREN Tanzania katika wilaya za Lindi,Ruangwa na Kilwa.

katika mradi huu LINGONET itawajibika kuratibu na kusimamia shughuli za kujenga mabaraza ya watoto,kuibua vitendo vya ukiukwaji haki za watoto na kuzifanyia rufaa,kutoa elimu kwa jamii ili waweze kuacha vitendo vya ukiukwaji haki za watoto,kuhakikisha mawazo na maoni ya watoto yanashirikishwa na kuthaminiwa na jamiii pamoja na mamlaka za kiserikali lakini pia na asasi zisizoza  kiserikali zinajumuisha shughuli zao na zile za haki za watoto ili kuifanya jamii inayofuata na kuthamini haki za watoto

Mradi huu ambao unatekelezwa katika wilaya 7 hapa nchini ulianza mwaka 2009 na kuishia mwaka 2012 disemba kabla kuanza tena katika awamu ya pili mwezi julai 2013