Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Utovu wa nidhamu kwa wakubwa kizazi kipya.hujikoloh

Sango Kipozi (Dar es salaam)
June 8, 2011 at 12:39 PM EAT

Kwanini jamii yetu imetoka kabisa nje ya maadili yetu, na siku hizi wazee wanahofia kuwakanya vijana eti kwakuwa kwa kuwa sio watoto wao, wakati katika taamaduni zetu, wazazi wamekuwa huru kuwakanya watoto wao na wa wenzao? Vile vile, mara nyingine wazazi huogopa hata kuwaelekeza watoto wao wenyewe, maana huambiwa na watoto hao bila heshima, eti wamepitwa na wakati. Tufanye nini ili kurudi tulikotoka?

wilbert njarabi (nzega)
June 17, 2011 at 12:37 AM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

@Sango Kipozi (Dar es salaam): muingiliano wa tamaduni za kigeni ni moja ya sababu zinazo sababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii tamaduni hizi zinatoa uhuru mkubwa hasa kwa watoto ambao wanaitaji kuelekezwa wangali wadogo na wazazi wao,kutokana na tamaduni hizo watoto wanaachwa wajiongoze wenyewe ambavyo hupotea na kutoka nje ya maadili ya jamii.mtoto anastaili aongozwe na kuelekezwa na wakubwa kwa sababu wamekwisha kuwa na uzoefu wa maisha na wameona mengi mazuri na mabaya kwa hiyo kumuelekeza mtoto ni kutaka apite katika mazuri yatakayo msaidia kuwa na maisha yenye mafanikio mema maishani mwake.


Add New Message

Invite people to participate