Log in
Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society

Dar es Salaam, Tanzania

Respondent: CHILDREN IN NEED OUTREACH
Time Submitted: April 29, 2011 at 2:19 PM EAT

Introduction

CHILDRENI IN NEED OUTREACH
CINO
KUHIMIZA NA KUHAMASISHA JAMII JUU YA UANDIKISHWAJI MAHUDHURIO YA LAZIMA NA UMUHIMU WA WATOTO WAO KUMALIZA ELIMU YA MSINGI LINDI
FCS/RSG/2/09/116
Dates: MARCH 27 2010 TO JUNE 2010Quarter(s): QUARTER 1
CAVIN MCHOPA

CHILDREN IN NEED OUTREACH

P.O.BOX 118

LINDI

Project Description

Policy Engagement
Governance and Accountability
1. KATIKA KIPENGELE CHA SERA, MRADI HUU UNAJIHUSISHA KATIKA KUBAINI UELEWA WA JAMII NA WADAU MBALIMBALI JUU YA SERA YA ELIMU, USHIRIKI WAO KATIKA UTEKELEZAJI WAKE, FURSA NA CHANGAMOTO ZINAZOCHANGIA KUSHUKA KWA ELIMU WILAYANI LINDI NA KWA PAMOJA KUBUNI MIKAKATI BORA YA KUINUA KIWANGO CHA UANDIKISHWAJI MAHUDHURIO NA UTOAJI WA ELIMU BORA.

2. KIPENGELE CHA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI, MRADI UNAKUSUDIA KUAMSHA UELEWA WA JAMII, WADAU MBALIMBALI NA WATENDAJI KATIKA NGAZI MBALIMBALI JUU YA WAJIBU WAO KATIKA KUSIMAMIA MAENDELEO YA WATOTO WAO.

RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiLINDIMTAMAMAKONDE,MIHOGONI,MPENDA,MVULENI NA MBALALA.2316
CHIKONJICHIKONJI,NANYANJE NA JANGWANI1075
NGAPANGAPA,CHELEWENI, MKUPAMA TANDANGONGORO, NANDAMBI NA MKANGA.1979
KIWALALAMPEMBE,RUO,MMANGAWANGA,MANDAWA,NARUNYU, KIWALALA NA MAHUBIKA1829
MINGOYOMNAZIMMOJA,MUUNGANO, MINGOYO, RUAHA NA MKWAYA.1893
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female484569
Male1024523
Total1509092

Project Outputs and Activities

1. KUONGEZEKA KWA IDADI YA WANAFUNZI WANAOANDIKISHWA , KUMALIZA ELIMU YA MSINGI NA MAHUDHURIO BORA DARASANI.
2. UELEWA WA JAMII JUU YA KUANDIKISHA WATOTO UMEONGEZEKA.
3. KUONGEZEKA KWA USHIRIKI WA JAMII KATIKA KUSIMAMIA UANDIKISHWAJI NA KUHIMIZA MAHUDHURIO YA LAZIMA
1. KUTAMBULISHA MRADI KWA VIONGOZI NGAZI YA KATA NA WILAYA.
2. KUFANYA MIKUTANO YA KUHAMASISHA JAMII KATIKA KATA 5 JUU YA UMUHIMU WA KUANDIKISHA NA KUHIMIZA MAHUDHURIO.
3. KUENDESHA MAFUNZO KWA KAMATI ZA SHULE, WATENDAJI KATA/WILAYA,WALIMU, WAWAKILISHI WA WAZAZI NA WALEZI JUU YA WAJIBU WAO KATIKA KUSIMAMIA UANDIKISHAJI NA MAHUDHURIO YA LAZIMA KWA WATOTO WAO.
4. KUTENGENEZA/KUANDAA MPANGO KAZI SHIRIKISHI JUU YA UTEKELEZAJI WA MRADI.
5. UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MRADI
6. UANDISHI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI NA USAMBAZAJI KWA WAHUSIKA1. KUTAMBULISHA MRADI KWA VIONGOZI
MKUTANO WA KUTAMBULISHA MRADI KWA VIONGOZI 20 WA NGAZI YA KATA NA WILAYA ULIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA LINGONET TARE 27.03.2010. WALIOHUDHURIA WALIKUWA:
AFISAELIMU WILAYA,MKUU WA WILAYA, MKURUGENZI MTENDAJI, MWENYEKITI HALMASHAURI YA LINDI,MWANDISHI WA HABARI,MKAGUZI WA SHULE, MWENYEKITI LINGONET,MWENYEKITI HUDUMA ZA JAMII (W), WADHAMINI 2 MJUMBE WA HAKI ZA BINADAMU, AFISAELIMU TAALUMA (w), MWEZESHAJI NA WANACHAMA WA CINO 5.

MAMBO YALIYOSHUGHULIKIWA: CINO KAMA WADAU WA ELIMU KUELEZEA HALISI YA ELIMU WILAYANI LINDI KWA KUTOA TAARIFA YA MATOKEO YASIYORIDHISHA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2008 KOANI LINDI, IKIONYESHA NAFASI YA MKOA KITAIFA NA WILAY KITAIFA NA MKOA. PIA KUELEZEA MAPUNGUFU NA MIKAKATI YA KUBORESHA KAMA ILIVYOJADILIWA NA KUAZIMIWA NA MKUTANO HUO MKUU WA MKOA.

PIA KUWAELEZEA WASHIRIKI SABABU ZILIZOPELEKEA KUIBULIWA KWA WAZO LA MRADI HUU NA KATA ZILIZOKUSUDIWA.

MKUTANO HUU ULIKUWA PIA HATUA YA MWANZO NA YA MSINGI YA KUPATA MAONI YAO, USHAURI NA USHIRIKIANO WAO KATIKA KUTEKELEZA MRADI HUU.

ILIKUWA PIA NAFASI NZURI KUELEWA NA KUTAMBUA KUWA WAO NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI USIMSMIZI NA UFUATILIAJI WA MRADI HUU KATIKA KUHAMASISHA NA KUSIMAMIA UTELEZAJI WA MRADI KATIKA MAENEO YAO YA KAZI.

2. KUFANYA MIKUTANO YA KUHAMASISHA JAMII JUU YA UMUHIMU WA KUANDIKISHA WATOTO KATIKA KATA 5 ZA MTAMA, NGAPA, CHIKONJI, KIWALALA NA MINGOYO ZA WILAYA YA LINDI.
MKUTANO ULIFANYIKA KATIKA KITUO CHA WALIMU MNAZIMMOJA LINDI TAREHE 17.04.2010 NA ULIHUDHURIWA NA WASHIRIKI 58 WAKIWA: WAWAKILISHI WA MADHEHEBU YA DINI 10, WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA 10, MADIWANI 5, WATENDAJI KATA 5,WENYEVITI WA VIJIJI 5 WAJUMBE WA KAMATI ZA SHULE, WAWEZESHAJI, MWANDISHI WA HABARI, WANACHAMA WA CINO 5 NA WARATIBU KATA HUSIKA.

MASUALA YALIYOSHUGHULIKIWA YALIHUSU:
WAJIBU WA KILA MMOJA KATIKA KUHAKIKISHA KUWA WATOTO WANAANDIKISHWA,
WANAHUDHURIA DARASANI NA WANAMALIZA ELIMU YA MSINGI.

MADHARA YA UTORO NA MAMBO YANAYOCHANGIA UTORO, UANDIKISHWAJI USIORIDHISHA NA MAHUDHURIO MABAYA.

TARATIBU ZA KUFANYA SENSA YA WATOTO KABLA YA ZOEZI LA UANDIKISHAJI NA USHIRIKI WAO VILIAINISHWA.

WASHIRIKI KATIKA MAKUNDI WALIJADILI JUU YA MATATIZO YANAYOCHANGIA WATOTO KUTOANDIKISHWA IPASAVYO,UTORO WA KUDUMU HATUA ZA KUCHUKUA DHIDI YA MATATIZO HAYO NA WAJIBU WA KILA MMOJA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MATATIZO HAYO.

3. KUENDESHA MAFUNZO KWA KAMATI ZA SHULE: WATENDAJI KATA, WAWAKILISHI WA WAZAZI NA WALEZI KATIKA KATA 5 ZA MRADI, WAJUMBE WA KAMATI ZA SHULE, WARATIBU ELIMU KATA, WALIMU WAKUU, WAWAKILISHI WA WAZAZI, MKAGUZI WA SHULE,MPIGA PICHA, WANACHAMA WA CINO. JUMLA YA WASHIRIKI WALIKUWA 38 NA MAFUNZO YALIFANYIKA TAREHE 02.05 2010 KATIKA UKUMBI WA KITUO CHA WALIMU MNAZIMMOJA LINDI.

MASUALA YALIYOSHUGHULIKIWA:
MADA ILITOLEWA KUHUSU WAJIBU WA WADAU MBALIMBALI KATIKA KUFANIKISHA UANDIKISHAJI NA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI KATIKA SHULE ZA MSINGI LINDI. VIPENGELE VILIVYOJADILIWA KWA KINA VILIKUWA:
TARATIBU ZA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI.
TARATIBU ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA SENSA
UMUHIMU WA KUFANYA SENSA
HALI YA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI KATIKA WILAYA YA LINDI.
MADHARA YA UTORO.
MAJADILIANO YALIHUSU ; NINI CHANZO CHA WANAFUNZI KUTOANDIKISHWA IPASAVYO

NINI CHANZO CHA UTORO WA KUDUMU NA WA REJAREJA

NINI KIFANYIKE KUTATUA MATATIZO YALIYOIBULIWA


4. KUANDAA MPANGO SHIRIKISHI WA UTEKELEZEJI WA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA WAKATI WA UHAMASISHAJI NA MAFUNZO YA WASHIRIKI MBALIMBALI KATIKA KATA 5 ZA MTAMA, KIWALALA, CHIKONJI, MINGOYO, NA NGAPA WILAYA YA LINDI. WASHIRIKI WALIKUWA 35 AMBAO NI :

MASUALA YALIYOSHUGHULIKIWA NI:

WASHIRIKI WOTE 35 WAKIWA KATIKA MAKUNDI 2 TOFAUTI WALIANDAA MPANGO KAZI NA BAADAYE UKAJADILIWA KWA PAMOJA NA KUUNGANISHWA TAYARI KWA UTEKELEZAJI.KUNDI LA KWANZA LILIKUWA LA WARATIBU ELIMU KATA NA WATENDAJI KATA. KUNDI LA PILI LILIKUWA LA WALIMU, WAJUMBE WA KAMATI ZA SHULE NA WAWAKILISHI WA WAZAZI.

UFUATILIAJI NA TATHMINI.
WANACHAMA WA CINO WALITEMBELEA KATA ZOTE TANO NA KUONANA NA WARATIBU ELIMU NA WATENDAJI KATA ILI KUONA MWITIKIO WA JAMII BAADA YA UHAMASISHAJI NA MAFUNZO. TAKWIMU AMBAZO TUMEAMBATISHA KULINGANA NA DODOSO TULILOTUMIA ZINAONYESHA KUPANDA KWA MAHUDHURIOHASA KWA MADARASA YA 11 HADI VII, HII INATOKANA NA MUDA MRADI ULIPOTEKELEZWA.
SHUGHULI ZOTE ZILIZOPANGWA ZILFANYIKA KAMA ILIVYO KUSUDIWA ISIPOKUWA KULIKUWEPO NA UCHELEWAJI WAKATI WA KUANZA NA KUMALIZA MRADI KUTOKANA NA FEDHA KUCHELEWA KULETWA TOKA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY.
SHUGHULI KIASI CHA FEDHA

1.KUTAMBULISHA MRADI KWA NGAZI YA WILAYA NA KATA. 635,000.00

2.KUFANYA MIKTANO YA KUHAMASISHA NA KUELIMISHA JAMII
JUU YA UMUHIMU WA KUANDIKISHA WATOTO NA KUHIMIZA
MAHUDHURIO. 1,053,000.00

3. KUENDESHA MAFUNZO KWA KAMATI ZA SHULE,WATENDAJI NA WAZAZI 1,306,500.00

4. KUTENGENEZA MPANGO SHIRIKISHI JUU YA UTEKELEZAJI WA MRADI NA
KUANDAA VIPEPERUSHI. 175,000.00

5. UFUATILIAJI NA TATHMINI 200,000.00

6.UANDISHI WA TAARIFA NA USAMBAZAJI 365,000.00

7, MATUMIZI YA OFISI 1,119,000.00

Project Outcomes and Impact

HALI YA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI KWA MADARASA YA PILI HADI YA SABA KWA KATA ZOTE TANO KWA MWAKA 2011 YAMEONGEZEKA KULINGANA NA MAHUDHURIO YA 2010 KAMA INAVYOONEKANA KATIKA KIAMBATISHO.MATOKEO YA KATA HIZI MBILI KATI YA KATA 5 ZA MRADI YANAONYESHA MAFANIKIO YA MUDA MFUPI WA MRADI YALIYOTARAJIWA. KATA ZINGINE TATU ZIMEONYESHA MABADILIKO YA MAFANIKIO KAMA HAYA VILEVILE.


1. VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI WAMEANZA KUTAMBUA MCHANGO WA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI KATIKA MAENDELEO YA JAMII.
2. WASHIRIKI MBALIMBALI KATIKA MRADI HUU HASA WAWAKILISHI WA MADHEHEBU MBALIMBALI NA WANASIASA WAMETAMBUA KUWA NAO PIA KWA NAFASI YAO WANAWAJIBIKA KATIKA KUSIMAMIA NA KUHIMIZA ELIMU WILAYANI LINDI.
3.WANAFUNZI WENGI WAMEJITOKEZA KUANDIKISHWA NA KUVUKA MALENGO MWAKA 2011 KATA YA MINGOYO.
4. USHIRIKI WA JAMII UMEONGEZEKA KATIKA KUSIMAMIA UANDIKISHWAJI NA KUHIMIZA MAHUDHURIO KUTOKANA NA WAZAZI KUJITOKEZA WENYEWE KWENYE OFISI ZA WENYEVITI NA VITONGOJI KUANDIKISHA WATOTO BILA KUSUBIRI WALIMU WAWAFUATE MAJUMBANI KAMA HAPO AWALI.
5.BAADHI YA SHULE WAMEANZA UTARATIBU WA KUTOA CHAKULA CHA MCHANA ILI KUPUNGUZA UTORO NA KUHIMIZA MAHUDHURIO.

.
MRADI PIA UMEPANUA UELEWA WA WANACHAMA KATIKA KUJUA HALI HALISI YA ELIMU WILAYANI LINDI NA HIVYO KUFIKIRIA ZAIDI JUU YA KUENDELEZA MRADI HUU ILI KUKABILIANA NA CHANGA MOTO ZILIZOJITOKEZA.

KUMEKUWEPO NA USHIRIKIANO WA KARIBU NA WATENDAJI NGAZI ZA KATA NA WILAYA WAKATI WOTE WA UTEKELEZAJI WA MRADI HUU.
TOFAUTI KUBWA ILIYOJITOKEZA NI ILE YA UCHELEWEVU WA KUPATA FEDHA TOKA FCS.

Lessons Learned

Explanation
KUWEPO NA KUIMARIKA KWA MAHUSIANO NA MASHIRIKIANO MAZURI KATI YA SHIRIKA LETU LA CINO,WANANCHI,ASASI ZINGINE NA MAMLAKA ZA SERIKALI KATIKA NGAZI MBALIMBA HUSUSAN IDARA YA ELIMU NA MAENDELEO YA JAMII.
WALIMU, WATENDAJI KATA NA WANANCHI KWA UJUMLA BADO HAWAJAJENGEWA UWEZO WA KUTOSHA KUHUSU SERA YA ELIMU,UMUHIMU NA FAIDA YA ELIMU KWA WATOTO WAO.
ADHABU NDOGO TENA ZA KULINDANA ZINAZOTOLEWA KWA WANAFUNZI AU WAZAZI WANAOCHANGIA UTORO NA MIMBA ZA UTOTONI HAZIJATATUA TATIZO LILILOPO ITAKIWAVYO.
WANANCHI NA WATENDAJI HASA NGAZI YA KATA WAKIWEMO WALIMU HAWAPATI MAPEMA TENA KWA UFASAHA TAARIFA ZA MABADILIKO KATIKA UBORESHAJI WA ELIMU IKIWA NI PAMOJA NA MITAALA NA VITABU VIPYA KWA WAKATI.
MUDA WA MAFUNZO KATIKA MRADI HUU UMEKUWA MDOGO SANA KIASI AMBACHO MAMBO MENGI YANAHITAJIKA KUTOLEWA KWA WALENGWA ILI KUBORESHA UTOAJI WA ELIMU WILAYANI LINDI.
WATENDAJI KATA AMBAO WAMEPEWA MAJUKUMU MAKUBWA YA KUSIMAMIA MAENDELEO KATIKA NYANJA ZOTE NDANI YA KATA WANAONEKANA KUZIDIWA NA MAJUKUMU HAYO MAHALI PENGINE WENGI WAO KUTOKUWA NA UELEWA WA KUTOSHA JUU YA MAMBO YA MSINGI; MF SERA YA ELIMU NA PIA SHERIA YA ELIMU.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
MRADI ULIKUSUDIWA KUWA WA MIEZI MITATU TU NA ULITEGEMEWA KUANZA NOVEMBA 2009 HADI FEBRUARY 2010 NA MATOKEO YAKE YA AWALI KUONEKANA MACHI 2010. KUTOKANA NA KUCHELEWA KUPATA MAFUNZO NA FEDHA TOKA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY MRADI ULIANZA KUTEKELEZWA RASMI MACHI 27 2010.PAMOJA NA KUCHELEWA KUANZA KWA MRADI KWETU ILIKUWA PIA NAFASI NZURI YA KUHAMASISHA JAMII NA WATENDAJI JUU YA MAJUKUMU NA WAJIBU WAO KATIKA UANDIKISHAJI NA MAHUDHURIO. KAZI ILIFANYIKA ZAIDI KATIKA MIKUTANO NA WARSHA ZILIZOHUSU TATHMINI YA ELIMU MKOANI NA WILAYANI LINDI.
MAENEO YALIYOOMBEWA MRADI (KATA 5) TU KATI YA KATA 28 ZA WILAYA YA LINDI NI KIDOGO KUTOKANA NA KIWANGO CHA FEDHA KILICHOOMBWA NA UCHANGA WA SHIRIKA.SHIRIKA LIMEKABILIANA NA CHANGAMOTO HII KWA KUHAKIKISHA KUWA LINATEKELEZA MRADI HUU KWA KIWANGO CHA JUU NA MATOKEO YAKE YA AWALI YANAONEKANA ILIVYOKUSUDIWA ILI LIWEZE KUPATA NAFASI YA UFADHILI WA KIWANGO CHA JUU ZAIDI NA HIVYO KUFIKIA KATA NYINGI ZAIDI NA KWA UFANISI ZAIDI
SERA YA ELIMU BADO HAIJAELEWEKA IPASAVYO KWA WATENDAJI WENGI NA JAMII PIA. MFANO KUNA UTATANISHI JUU YA KEPENGELE KATIKA SERA KINACHADAI KUWA KILA MTOTO MWENYE UMRI WA KWENDA SHULE ANALAZIMIKA KWENDA , LAKINIWAKATI WA KUANDIKISHA WATOTO, WENGI WAO HUACHWA KWA MADAI KUWA KUNA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA NA UPUNGUFU WA WALIMU.WASHIRIKI WAMEAZIMIA KUENDELEA KUHAMSISHA JAMII KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUANDAA MIUNDO MBINU YA KUTOSHA KWA AJILI YA KUWAPOKEA WATOTO WOTE , LAKINI PIA SHIRIKA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO LIANDAE MAFUNZO,MIJADALA NA MIDAHALO JUU YA SERA YA ELIMU NA UTEKELEZAJI WAKE.
WASHIRIKI WENGI KATIKA MRADI HUU HASA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI NA WANASIASA HAWAKUJUA KABISA KUWA WAO PIA KWA NAFASI ZAO WANAHUSIKA KATIKA KUHAMASISHA SENSA YA WATOTO, UANDIKISHWAJI NA MAHUDHURIO YA LAZIMA.KUTOKANA NA MPANGO SHIRIKISHI KILA MSHIRIKI AMEFAHAMU WAJIBU WAKE NA WAMEAHIDI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UANDIKISHWAJI NA KUHIMIZA MAHUDHURIO.
KUTOKUWEPO KWA MPANGO WA CHAKULA CHA MCHANA KWA WANAFUNZI KUMECHANGIA MAHUDHURIO HAFIFU.HALMASHAURI YA WILAYA YA LINDI IMEANZA UTARATIBU WA KUTOA CHAKULA CHA MCHANA KATIKA MASHULE KWA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI WA SHULE HUSIKA.
ONGEZEKO LA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KAMA YATIMA NA WALE WANAOKABILIWA NA HALI NGUMU YA KIUCHUMI LIMEONEKANA PIA KUATHIRI MAHUDHRIO YA WATOTO SHULENI.WASHIRIKI WALISHAURI ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI ZIANGALIE UWEZEKANO WA KUSAIDIA KUNDI HILI, LAKINI PIA IKAPENDEKEZWA SERIKALI KUU NA SERIKALI ZA MITAA ZITENGE KATIKA BAJETI ZAO FEDHA ZA KUSAIDIA WATOTO HAWA.
KUTOKUWEPO KWA MADARASA YA AWALI KATIKA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI AU KATIKA ENEO LA JIRANI NA SHULEWASHIRIKI WAMEAZIMIA KUSISITIZA AGIZO LA WIZARA YA ELIMU NA UFUNDI KUWA KILA SHULE YA MSINGI BUDI IWE NA SHULE YA AWALI.
BAADHI YA SEHEMU HESHIMA KWA WALIMU IMEPUNGUA NA HIVYO JAMII KUTOWAPA USHIRIKIANO HASA WAKATI WA KUFANYA SENSA NA UANDIKISHAJI.WASHIRIKI WAMEAZIMIA KUSHUGHULIKIA MASUALA HAYA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA KIJIJI, WATENDAJI KATA KATIKA KUTAMBUA NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI TOFAUTI ZINAZOJITOKEZA NDANI YA JAMII MBAZO KWA NJIA MOJA AU NYINGINE ZINADIDIMISHA ELIMU.
MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA DHANA YA (HAKI ZA MTOTO) MWALIMU AU MZAZI ANAONEKANA KUTOKUWA NA SAUTI KWA MTOTO AU MAMLAKA YA KUMWADHIBU MTOTO MARA ANAPOKOSEA KWA KUHOFIA SHERIA INAYOMLINDA MTOTO ITAMWANDAMAWASHIRIKI WALISHAURI MAFUNZO YATOLEWE ZAIDI JUU YA SHERIA INAYOMLINDA MTOTO.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
SERIKALI YA WILAYAWATENDAJI NGAZI YA KATA NA WILAYA WALIHUSISHWA TANGU HATUA ZA AWALI KWA NJIA YA KUTOA TAKWIMU ZA HALI HALISI YA ELIMU KUANZIA NGAZI YA KATA, WILAYANI NA MKOANI.

WAMESHIRIKISHWA KATIKA UTAMBULISHO WA MRADI,MAFUNZO,UHAMASISHAJI, UANDAAJI WA MPANGO SHIRIKISHI NA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA MRADI. MKUU WA WILAYA AKIWA MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI.
IDARA YA ELIMU WILAYANI NA MKOATUMEWASHIRIKISHA KATIKA KUANDAA NA KUTOA BAADHI YA MADA ZILIZOKUWA ZIMEKUSUDIWA KATIKA HATUA MBALIMBALI ZA MRADI.

TUMEKODI MAJENGO YA VITUO VYA WALIMU ILI KUBORESHA MAHUSIANO NA KUWAONGEZEA KIPATO.
WATENDAJI WA NGAZI YA WILAYA, KATA NA SHULE WAMESHIRIKISHWA KATIKA HATUA YA UIBUAJI WA MRADI, UHAMASISHAJI, MAFUNZO, MAANDALIZI YA MPANGO SHIRIKISHI NA UFUATILIAJI WA MANDELEO YA ELIMU KWA KARIBU ZAIDI.
ASASI ZISIZO ZA SERIKALI.ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI NA MTANDAO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI VIMESHIRIKISHWA WAKATI WA UTAMBULISHO WA MRADI.TAASISI ZA DINI NA SIASAWAMESHIRIKISHWA KATIKA HATUA ZA AWALI KATIKA KUTAMBUA MAENEO YAMRADI NA WALENGWA WA KATA HUSIKA.

WAMESHIRIKI MIKUTANO YA UHAMASISHAJI NA MAFUNZO.
MADIWANIWAMESHIRIKISHWA KATIKA MIKUTANO YA UTAMBULISHO WA MRADI, UHAMASISHAJI NA MAFUNZO.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
KUTEMBELEA KATA ZOTE 5 KUONA UTEKELEZAJI WA MPANGO SHIRIKISHI, KUKUTANA WATENDAJI KUPATA MAONI YAO JUU YA MWITIKIO WA JAMII KUHUSU SUALA LA ELIMU.V
KUWA OFISINI NA KUANDIKA TAARIFA YA ZIARA ZA KATA HUSIKA.V
KUTEMBELEA SHULE ZILIZOKO KATIKA KATA HUSIKA ,KUKUTANA NA WALIMU NA KUJADILI KWA PAMOJA HALI YA UANDIKISHWAJI NA MAHUDHURIO KABLA NA BAADAYA UHAMASIHAJI NA MAFUNZOV
KUENDELEA KUKUTANA NA WADAU MBALIMBALI WALIOSHIRIKI KATIKA MRADI KUPATA MAONI YAO JUU YA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO WAKATI WA MAFUNZO NA NINI KIFANYIKE BAADAYE KATIKA KUBORESHA ELIMU WILAYANI LINDI.. VV
KUWA OFISINI KUANDAA TAARIFA,KUUNGANISHA NA KUTAFSRI TAKWIMU ZILIZOTOKA KATIKA KATA NA MASHULE NA MWISHO KUANDIKA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI NA KUSAMBAZA KWA WALENGWA NA WAHUSIKA WAKUU.VV
KUKUSANYA TAARIFA NA TAKWIMU MBALIMBALI KWA KUSHIRIKI MIKUTANO YA TATHMINI YA ELIMU KIWILAYA NA KIMKOA, KUTEMBELEA KATA ZINGINE KWA NIA YA KUTAMBUA KUKUTANA NA WATENDAJI NGAZI YA KATA, SERIKALI ZA VIJIJI, NA WANAJAMII KUIBUA NA KUTAFITI ZAIDI MAMBO YANAYOPELEKEA KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU WILAYANI LINDI.V

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale1157
Male3779
Total48136
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total0(No Response)
ChildrenFemale4441(No Response)
Male4379(No Response)
Total8820(No Response)
DisabledFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
YouthFemale1764
Male3856
Total55120
OtherFemale(No Response)4569
Male(No Response)4523
Total09092
WATU WENGINE NI IDADI YA WANAJAMII WALIOKO KATIKA VIJIJI VILIVYOKO KATIKA KATA 5 ZA MRADI

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
MAFUNZO JUU YA MBINU MBALIMBALI ZA UTUNISHAJI WA MFUKO12 HADI 16 APRIL 2010.CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOKABILI AZAKI KATIKA SUALA LA UHAMSISHAJI WA RASILMALI NA UTUNISHAJI MFUKO

DHANA YA UTAFUTAJI WA RASILMALI NA UTUNISHAJI MFUKO ASASI ZA KIRAIA

UADAAJI WA MKAKATI MPANGO WA UTUNISHAJI MFUKO

KANUNI NA MIIKO YA UTAFUTAJI FEDHA NA RASILMALI.

VYANZO VYA MAPATO NA RASILMALI NYINGINEZO.

SHUGHULI MAHSUSI ZA UTUNISHAJI MFUKO.

UANDIKAJI WA ANDIKO LA MRADI NA UUZAJI WA MCHANGANUO.

UTUNISHAJI WA MIFUKO KUPITIA MAKAMPUNI.

KUJENGA UHUSIANO NA KUIMARISHA MSHIKAMANO KATI YA ASASI ZA KIRAIA NA WAFADHILI.

UANDAAJI MPANGO MAWASILIANO NA UTUNISHAJI MFUKO KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.


TUMENDIKA MAANDIKO YA MRADI NA KUPELEKA SEHEMU MBALIMBALI.

TUMEFUNGUA MINI STATIONERY KWA AJILI YA WATEJA NA WANACHAMA

WATU BINAFSI WAMECHANGIA ASASI YETU KWA NIA YA KUWASAIDIA YATIMA NA WATOTO WALIOSHINDWA KUJIUNGA NA SHULE ZA SEKONDAR BAADA YA KUFAULU.
KUWAJENGEA WASHIRIKI UWEZO NA STADI ZA KUWEZESHA.21.02.2011 HADI 25.02.2011MAANA NA TOFAUTI YA MENTORING NA COACHING.

DHANA YA MCHAKATO WA UWEZESHAJI (CONCEPTS OF FACILITATION SKILLS)

CHANGAMOTO ANAZOKABILANA NAZO MWEZESHAJI. (FACILITATORS CHALLENGES)

MBINU ZA UWEZESHAJI.(ART OR CULTURE OF FACILITATION)

TABIA ZISIZOKUBALIKA KWA MWEZESHAJI.( UNACCEPTABLE BEHAVOURS)

MBINU ZA UWEZESHAJI ( FACILITATION TECHNIQUES .

NINI MAANA YA MAWASILIANO NA HATUA ZA MCHAKATO WA MAWASILIANO.

MATUMIZI YA MUDA (TIME MANAGEMENT)
WANACHAMA WAMEPEWA MREJESHO NA WAMEANZA KUWEZESHA KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI YA WALENGWA.
MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI KWA ASASI09.HADI 12.03.2011KUJENGA UELEWA WA WATEKELEZAJI KATIKA:

1. UFUATILIAJI NA UTEKELEZAJI MIRADI.

2. TATHIMINI YA MIRADI.

3. UANDISHI WA TAARIFA.

4. UTUNZAJI KUMBUKUMBU MUHIMU ZA MIRADI

5. KUHUSIANISHA JINSIA NA HAKI ZA BINADAMU KWENYE UTEKELEZEJI.
MREJESHO UMETOLEWA KWA WANACHAMA NA TUMEANZA KUTEMBELEA KATA 5 TULIZOFANYIA MRADI.

Attachments

« Previous responseNext response »

« Back to report