Log in
Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society

Dar es Salaam, Tanzania

Respondent: WINGS ENVIRONMENT AND EDUCATION TRANSFOMATION UNITY
Time Submitted: May 2, 2011 at 10:50 AM EAT

Introduction

WINGS ENVIRONMENT AND EDUCATION TRANSFOMATION UNITY
WEETU
UFUATILIAJI WA RASILIMALI ZA UMMA (PETS)
FCS/MG/1/10/208
Dates: Januari 1, 2011 to March 31,2011Quarter(s): 1
MODEST JOSEPH MKUDE
P.O BOX 6692
MOROGORO

Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unalenga kuiwezesha jamii/wananchi kuimarisha misingi ya utawala bora na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kujenga uwezo wa kufuatilia fedha na rasilimali za umma na pia kufanya zoezi la ufuatiliaji wa matumizi hayo ili kusimamia na kuwawajibisha watendaji katika sekta ya elimu wilayani Mvomero na Morogoro vijijini na kuongeza ufanisi na ubora wa sekta ya elimu kwa ujumla
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MorogoroMVOMERO NA MOROGORO (V)Doma, Melela, Mlali, Mzumbe, Kisemu, Mkuyuni, Langali, Bunduki ,Tchenzema, Kikeo, Kibati, Maskati, Tawa, Mvomero, Hembeti, Mtibwa, Diongoya, Mhonda, Kanga, Sungaji, Mvuha, KirokaSEWE, MTIPULE,MELA,MELELA,MONGWE,MANZA,YOWE,MIFULU,MASANZE,LUBUNGO,MHONDA,UBIRI, LUSANGA,DIONGOYA,TURIANI,KISALA,MLAGUZI,MLUMBILO, KUNKE,LUNGO,KANGA,DIHINDA,KILOKA,DIOVUVA,KONDE,MTAMBA,UPONDA,MILAWILILA,KITUNGWA,KILENGEZI,CHANGA,KIBUKO,MKUYUNI,MAKUYU,MGUDENI,MVOMERO,HEMBETI,KISIMAGULU,KIBATI,GONJA,NDOLE, MASKATI,KINDA,LANGALI,TENGERO,MAGURUWE,BUNDUKI,BUMU,PINDE,VINILE,LUALE,MASALAWE4000
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female7002000
Male6002000
Total13004000

Project Outputs and Activities

•Mafunzo ya namna ya kushiriki na kufuatilia matumizi ya fedha za umma na rasilimali nyingine katika sekta ya elimu yametolewa kwa kamati za maendeleo za shule kwa kata 22 za wilaya 2
Kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za shule na wawakilishi wa wajumbe wa serikali za vijiji juu ya namna wanavyoweza kufuatilia rasilimali za fedha zinazotengwa katika sekta ya elimu Wilayani Mvomero na Morogoro vijijini katika kata 22 kwa vituo 5 kwa siku 3 wajumbe 50 kila kituo.
Kituo cha Langali, Mvomero,Mhonda,Mlali na Mkuyuni tumefanya yafuatayo:- Kutoa mafunzo: kwa kamati za shule juu ya majukumu na wajibu wa kamati za shule,muundo wa serikali na mitaa na maana yake,dhana ya mipango na bajeti, maana na umuhimu wa ufuatiliaji wa Fedha na rasilimali za umma, sheria na wajibu wa umma katika kufanya PETS.Idadi ya washiriki katika vituo hivyo ni hivi :-Mlali-49,Mvomero-44,Mhonda-54,Mkuyuni-51Langali -50.
Tofauti iliyopo ni idadi ya wajumbe wa warsha za mafunzo katika vituo ambapo tulitegemea kila kituo washiriki wangekuwa 50 lakini kulikuwa na tofauti kama ifuatavyo:-Langali-50,Mlali-49, Mvomero-44, Mhonda-54,Mkuyuni-51
-Chakula na vinywaji kwa washiriki wa semina/warsha 4,464,000,
-Malazi kwa washiriki 5,952,000
-shajara 602,000
-usafiri 8,605,000
-honolaria kwa wawezeshaji 4,500,000
-Posho ya mtunza hazina na mratibu 1,200,000
-malipo ya ukumbi 720,000
-ununuzi wa vifaa vya utendaji na ofisi 3,500,000
-Pango la ofisi 450,000
-Mawasiliano 60,000
Jumla ya matumizi 30,053,000.

Project Outcomes and Impact

Kamati za shule zinatekeleza majukumu yao hasa katika ufuatilaiji na upangaji wa shughuli za maendeleo za shule na kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha zinazotengwa na pia ushiriki wa wananchi katika kupanga na kusimamia maendeleo na rasilimali za umma katika sekta ya elimu umeongezeka
Asilimia 75 ya wajumbe wa kamati za shule hawakufahamu majukumu na wajibu wao hasa katika suala la umililiki ya shule .baada ya utekelezaji wa mradi wajumbe wamefahamu nafasi zao katika kusimamia shughuli za maendeleo ya shule kitaaluma na kimiundo mbinu.

Walimu wakuu na wajumbe wa kamati za shule wamefahamu umuhimu wa kuwa na mipango ya maendeleo ya shule hivyo kila shule zilizopata mafunzo wameweka mikakati ya kuwa na mpango ifikapo Julai 2011.

Wajumbe wa kamati wameelewa wajibu wao wa kufuatilia mapato na matumizi ya Fedha na Rasilimali za shule na kijiji na wametambua kuwa ni haki yao kujua. Hivyo baadhi ya wajumbe wameanza papo kwa papo kuuliza mapato ya shule toka kwa walimu wakuu wao wa shule zao.

Pamoja na hilo wajumbe wa kamati za shule wameanza kuulizia mipaka ya shule zao na namna watakavyoweza kufanya upimaji wa ardhi ya shule zao.
Idadi ya wajumbe wa kamati zashule imeongezeka mara baada ya kufahamu idadi kamili za wajumbe na kamati za shule. Aidha kamati za shule zimeweza kujigawa katika kamati ndogondogo za utendaji baada ya kupata maelekezo toka wa wawezeshaji wa Semina.

Utafutaji wa rasilimali umeongezeka baada ya wajumbe kuelewa wajibu wao kwa maendeleo ya shule.

Maofisa elimu wameona haja ya kuendeleza mafunzo haya kwa shule nyingine ambazo hazipo katika eneo la mradi.
Kamati nyingi hazijawahi kupata mafunzo ya wajibu wao.
Wanananchi wakiwemo wajumbe wa kamati za shule zilibaki katika hali ya kutofahamu kuwa wana haki ya ya kuhoji mapato na matumizi ya Fedha na rasilimali za umma.

Rasilimamali fedha toka Serikalini hazifiki kama zilivyopangwa katika ngazi ya vijiji na kama zinafika ni kiasi kidogo ukilinganisha na kiasi kilichotolewa na wizara. Kwa MMeM kisera inaonesha kila mwanafunzi alitakiwa kupata Tsh 10,000,lakini kwa maelezo ya walimu wakuu waliohudhuria mafunzo hakuna hata shule moja ambayo mwanafunzi amepata zaidi ya Tsh.5,000.

Lessons Learned

Explanation
Kamati za shule na jamii vijijini hawajui haki zao za msingi za kufahamu na kuhoji mapato na matumizi ya fedha na rasilimali za umma.

Walimu wakuu na walimu wengine katika shule hasa zile za vijijini wanatumia mwanya huu wa kutokufahamu kwa wajumbe na jamii juu ya mapato na matumizi ya fedha na rasilimali za umma kutumia vibaya yaani nje ya makusudi halisi ya fedha au rasilimali husika.
Shule na vijiji hazina mipango ya maendeleo na hivyo kutokuwa na vipaumbele vya utendaji.mwanya huu unawapa nafasi fedha toka wilaya kutumika nje ya vipaumbele vya shule/vijiji.
Utekelezaji wa Mpango wa MMEM katika ngazi za vijiji vilivyo mbali na miji na barabara kuu hasa ujenzi wa vyumba vya madarasa upo chini sana kwa idadi na ubora.
Wanakijiji wakielimishwa wana uwezo wa kuelewa na kutenda.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Kufika katika vijiji husika vya mradi kwa wakati haikuwa rahisi kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu.Kukodi gari imara lenye 4w ili kumudu kufika katika vijiji hivyo.
Baadhi ya madiwani kushindwa kuhudhuria mafunzo muhimu ya kamati za shule kutokana na malipo madogo ya FCS/WEETUKukutana nao uso kwa uso kuwaeleza umuhimu wa mafunzo.
Kuwaalika wawakilishi wao
Gharama za kununua vifaa hasa vya ofisini kuwa kubwa zaidi ya bajeti ya mradi. Mfano Photocopier ya ofisi.Kuandika barua kwa msimamizi wa mradi kuomba kuunganisha bajeti ya printer na photocopier ili kununua photocopier.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Ofisi ya Afisa elimu msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Morogoro vijijiniMkutano wa kutambulisha mradi huu wa PETS
-kupata wawezeshaji kwa mafunzo ya kamati za shule.
-kupata maelezo ya mipango na bajeti za Halmashauri kwa maendeleo ya elimu katika vijiji vya mradi.
Waratibu elimu kata na watendaji wa vijiji.-Kuandaa shughuli za mafunzo na kuwaarifu wajumbe.
-Kueleza mipango ya kijiji na ya shule katika maeneo yao.
Waandishi wa habari-Kutoa taarifa kwa wananchi juu ya dhana na mchakato wa kufanya PETS.
Mashirika mengine yasiyo ya kiserikali yanayofanyakazi katika vijiji vya mradiKubadilishana ratiba na mawazo ili kutogongana katika kuwatembelea wanakijiji kwa makusudi ya kutekeleza miradi.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuunda timu na kufanya mafunzo ya utafiti wa PETS. Washiriki 50 watapatiwa mafunzo na kushiriki katika kufanya PETS, na watapatikana toka eneo la mradi
AprilMayJune

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
Washiriki wa mafunzo ni 248 kutoka katika kata 22

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Tuzo2009Utendaji wa asasi na wajibu kwa jamii katika kuleta mabadlikoya kweliKuimarisha asasi yetu kwa kuongeza watendaji na vifaa ilikutimiza wajibu wetu kwa jamii walengwa.
Kuhudhuria mafunzo ya uendeshaji wa miradi2010Jinsi ya kuandaa taarifa za utendaji na Fedha kwa Asasi Kuboresha taarifa za shirika ilikuwezesha wadau kupata taarisa sahihi kwa maendleo ya jamii.

Attachments

« Previous responseNext response »

« Back to report