Kwa nini mradihuu unahitajika?Kwenyemradi wetu uliopita katika kata mbili za manispaa ya Arusha yaani unga ltd na sokon 1 tuligundua watu hawakujitokeza kupima VVU/UKIMWI Katika vituo mbalimbali ndani ya manispaa kutokana nauelewa mdogo na kutojua umuhimu au faida ya kupima na kujitambua. Kwa sababu hii inachangia maambukizi kuendelea kuongzeka kila mwaka badala ya kupungua watu wengi wanafanya ngono pasipo kutumia kinga. Pamoja na usambazaji na upatikanaji wa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa hiari bado uelewa na mwitikio wa upimaji wa VVU/UKIMWI Tanzania (THIS) Uliofanyika mwaka 2003/2004 ulionyesha kuwa kiasi cha 15% tu ya wanaume na wanawake wamewahi kupima VVU. hii pia inachangiwa na wataalam wachache wenye uwezo wa kutoa ushauri nasaha na baadhi ya watu kuogopa kunyanyapaliwa ni kati ya vikwazo vinavyokwamisha kuongezeka kwa utumiaji wa huduma ya VCT pia kukosekana kwa huduma ya matunzo baada ya kupima.
May 4, 2012