Dondoo na Vidokezo kuhusu Uzalishaji kwa ajili ya CBOs na NGOs
Hivi ni nini kinachosababisha shirika lako liaminike? Liwe katika kiwango cha kupewa ruzuku? Liheshimike katika jamii kwa ujumla na pia litambulike kwenye serikali?
Kutokana na ufwatiliaji uliofanywa na REPOA, takriban asilimia 60% ya ruzuku kwaajili ya mashikia yasiokuwa ya kiserikali nchini Tanzania zinatokana na mashirika ya kimataifa. Upataji na ufwatiliaji wa ruzuku ni moja kati ya kazi muhimu sana na pia yenye changamoto nyingi sana kwa mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Kujifundisha jinsi ya kupata ruzuku na kukimu mahitaji ya ki fedha kwenye shirika kupitia shuguli za kihisani zitakazo ingiza pesa ni muhimu sana kwaajili ya shirika lako.
Je una mawazo yeyote au mada unayotaka uchangie kwenye makala hii? Umewahi kufanya shughuli za kihisani na ukafanikiwa?