Kubadili Mipangilio ya Akaunti yako
Ukurasa wa Vifaa Vya Mtumiaji unakuwezesha kubadili vitu vingi kwenye tovuti yako kama namba za mawasiliano. Wakati umeingia kwenye akaunti yako ya Envaya,kifungo cha namna hii kinachoonekana juu ya ukurasa kinakupeleka kwenye ukurasa wa Vifaa Vya Mtumiaji.
Katika ukurasa huu unaweza kubadilisha jina la asasi lako, na kubadili anwani ya barua pepe na namba za simu.
Katika sehemu ya lugha ya msingi, unaweza kuchagua lugha ya msingi utakayopenda kuitumia kwenye tovuti yako.
Katika sehemu ya taarifa ya Mtumiaji, unaweza kubadilisha ili kuboresha mawasiliano yako na kufanya iwe rahisi kwa Envaya kuwasiliana na asasi yako na hata kwa wadau wengine.
Kuhifadhi mabadiliko,kifungo cha hapa chini ya ukurasa wakati wewe ni kumaliza.
Kubadilisha Jina la Mtumiaji wa Shirika lako.
Kwenye ukurasa wa vifaa vya Mtumiaji, unaweza kubadilisha jina la mtumiaji wa asasi yako kwa kubonyeza Badilisha Jina la Mtumiaji.
Kumbuka kwamba ukibadikisha jina lako la mtumiaji, anwani ya tovuti yako ya Envaya pia itabadilika (kutoka http://envaya.org/jina la zamani kwa http://envaya.org/jina jipya kwa mfano).
Kama mtu atatembelea anwani yako ya zamani, Envaya itawapeleka moja kwa moja kwenye anwani yako mpya. Baada ya kubadilisha jina la mtumiaji wa asasi yako, shirika lingine linaweza kujisajili na jina la mtumiaji yako ya zamani na kujenga tovuti kwa anuani yako ya zamani.
Kubadilisha neno la siri la Shirika lako
Kwenye ukurasa wa Vifaa Vya Mtumiaji unaweza kubadilisha neno la siri kwenye asasi yako kwa kubonyeza Badilisha neno la siri.
Kubadilisha neno la siri unahitaji kuingiza neno la siri la zamani kisha andika neno la siri jipya mara mbili. Neno la siri lako lazima liwe angalau herufi sita.