End of Year Greetings from the Envaya Team
Seasons’ greetings to all our partners, fellow NGO’s and supporters. It is finally the end of another year and we would like to take a moment to reflect on the achievements and challenges of the year 2012.
This year has marked two consecutive years of Envaya here in Tanzania. Within this time we have become Tanzania’s biggest network for NGO’s and CBO’s, with over 1,100 NGOs throughout Tanzania and some in Rwanda, most of which are within rural areas. The growth of Envaya has been organic and self-propagating, as Ngo’s have found it easy to build their own website with Envaya’s user friendly software. Through word of mouth and seminars, about a quarter of all Ngo’s within Tanzania are now using Envaya
This year we have undertaken various projects to enhance the usability of the Envaya website, we have held seminars and also mobilized our team into visiting Ngo’s in their respective offices all over Dar es Salaam.
The Envaya team has worked hard to make the Envaya website more interactive with its public. We have introduced various new features to this effect; like the Envaya News Story which we try to update every two to three weeks. So far we have done various articles that are aimed to informing, advising and inciting discussion within the Ngo community and the general public. We have covered a range of varying topics such as The 2012 National Census, the culture of Volunteerism, Vaccination Week and tips for fundraising and networking for Ngos. In all this, various Ngo’s have given their views, comments and ideas on the issues discussed.
In addition to this, we added a Volunteer Page, which allows Ngo’s to connect to potential volunteers within and outside the country. The aim of this is to bridge the gap between volunteers and Ngo’s in need of young talent. At the moment there are about 90 volunteer posts on the Envaya Volunteer Tab. We have also added a Featured News column where we highlight the latest updates from Ngo’s on the Envaya Home Page.
Outside the office, the Envaya team has mobilized itself to visit Ngo’s in their respective offices throughout Dar es Salaam to promote our SMS platform. This platform allows members of Envaya to publish news, amongst other things, using any phone through simple SMS texts.
The greatest challenge as always is encouraging more updates from Ngo’s with inactive websites. We are hoping that with time every Ngo will understand the importance of websites, social media and how it can greatly improve their work. We will continue confronting this barrier as start another year.
This has definitely been a year of progress for Envaya and hopefully for our partners and member NGO’s too. We would like to hear from you too, how has Envaya impacted your work this year? How can we better our services to you and how can you encourage other Ngo’s in the use of social media and the use of their free Envaya website? Share your stories and leave us a comments below.
Happy Holidays and a Happy New Year 2013!
Dondoo na Vidokezo kuhusu Uzalishaji kwa ajili ya CBOs na NGOs
Hivi ni nini kinachosababisha shirika lako liaminike? liwe katika kiwango cha kupewa ruzuku? liheshimike katika jamii kwa ujumla na pia litambulike kwenye serikali?
Kuna vitu ambavyo unaweza ukawa unavijua lakini unavipuuzia ingawa vina umuhimu sana na kazi unazozifanya katika jamii...makala hii itagusia baadhia ya vitu hivyo.....
Nchini Tanzania kazi za mashirika yasio kuwa ya kiserikali yaani (NGO’s) yako chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, na watoto, wanapatikana Kivukoni. Unaweza kusajili shirika lako, bure, na kupata kibali cha kuendesha shughuli zako za kujitolea, au za ki msaada. Shirika mwamvuli ambalo linalea na kusimamia mashirika yasiokuwa ya kiserikali yote nchini Tanzania linaitwaNational Non-Governmental Organization’s Council (NACONGO) limeundwa takriban miaka 8 iliopita.Je unalifahamu? na je wewe ni mwanachama? Je umefanya mawasiliano ya aina yeyote nalo? Je unazifahamu Sheria na taratibu za muongozo wa mashirika yasiokuwa ya kiserikali nchini Tanzania, kwenye kifungu cha NGO Act 2002.
Nchini Rwanda usajiri wa asasi zisizokuwa za kiserikali hufanyika chini ya bodi iitwayo “Rwanda Governance Board” (RGB) tovuti yao ni www.rgb.rw ambamo kuna orodha ya mahitaji yote yanayohitajika ili asasi iweze kujisajiri nchini Rwanda. Mojawapo ya mahitaji ni kuwa na hati inayoonyesha makao makuu ya hilo shirika na anwani kamili na mpango kazi kwa mwaka wa fedha, hilo ni hitaji moja wapo.
Kutokana na ufwatiliaji uliofanywa na REPOA (Special Paper 07.21), takriban asilimia 60% ya ruzuku kwaajili ya mashikia yasiokuwa ya kiserikali nchini Tanzania zinatokana na mashirika ya kimataifa. Upataji na ufwatiliaji wa ruzuku ni moja kati ya kazi muhimu sana na pia yenye changamoto nyingi sana kwa mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Kujifundisha jinsi ya kupata ruzuku na kukimu mahitaji ya ki fedha kwenye shirika kupitia shuguli za kihisani zitakazo ingiza pesa ni muhimu sana kwaajili ya shirika lako.
Mashirika mengi huwa yanatafuta taarifa za mawasiliano za mashirika yanayotoa ruzuku na baada ya hapo wanaandika na kutumia proposal ndefu yenyekuelezea mahitaji yao ya kifedha na kuelezea miradi yao na jinsi wanavyo hitaji sana msaada wa pesa. Njia hii haifanikiwi mara kwa mara na inaweza pia kupunguza uaminifu wa shirika husika linalo omba ruzuku na pia inaweza kuwakatisha tamaa kabisa wadau na wahusika wa NGO hiyo kutokana na kukataliwa mara kwa mara.
Kitu amabacho Mashirika yasiokuwa ya kiserikali yanapaswa kuelewa na kufahamu ni kwamba mashirika yanayotoa ruzuku yanahitaji kujua kuwa shirika lako linaaminika kabla ya hata kupata wazo la kutoa ruzuku kwa shirika lako na kupokea maombi yako. Njia moja ya kujenga uaminifu ni kujiweka katika mitandao ya watu wenye malengo sawa na wewe. Jenga uhusiano wa kikazi lakini pia hata wa kirafiki tu na mashirika yasiokuwa ya kiserikali kitaifa, kimataifa, wawakilishi wa Serikali za mitaa na kadhalika. Kujenga uhusiano mzuri na watu kama hao itasaidia shirika lako kujenga uaminifu zaidi kwa mashirika yanayo toa ruzuku yanapouliza kazi za shirika lako. Pia kama kuna nafasi zozote za kupata ruzuku ni rahisi sana kwa mashirika uliojenga nayo urafiki kukukumbuka na hata kuweka jina la shirika lako kwenye orodha zao za wapokea ruzuku.
Lakini kumbuka, katika yote haya . USITHUBUTU KUOMBA RUZUKU! Lengo la kuingia katika mitandao ya aina hii ni kujenga jina zuri kwaajili ya shirika lako, kwa kazi ya kuleta maendeleo katika jamii kwa ufanisi mkubwa, napia kujenga mtandao amabo unaweza hata kuthibitisha uwepo na uwezo wa shirika lako.
Mfumo mwengine wa kukusaidia kujenga mtandao kiurahisi ni kuwa mwanachama wa vyama vilivyo sajiliwa au hata vyama tu vya mashirika yanayo kutana mara kwa mara kubadilishana mawazo lakini hawajasajiliwa kama mtandao kitaifa. Jiunge na vyama vilivyopo karibu na wewe. Mfano wa mashirika kimtandao ni kama NACONGO, TANGO, FCS, ENVAYA, na kadhalika. Kama si mwanachama wa mtandao wowote basi kuna nafasi na fursa nyingi ambazo unazikosa.
Uwepo wako katika mtandao wa internet ni fursa tosha kwako wewe. Jaribu kujenga picha hii akilini mwako, unapo peleka proposal kwa watoa ruzuku na mtoa ruzuku huyu anaamua alitafute shirika lako kwenye mtandao wa internet lakini jina lako halileti majibu yeyote, au anapata taarifa ambazo zimewekwa zamaani sana hazijawekwa mpya ….hiyo inamjengea picha gani huyu mtoa ruzuku?? kwa kweli hii haileti picha nzuri kabisa. Website yako ndo kama uso wa shirika lako ambao unaonyesha nyie mnasimamia nini katika jamii na mnaleta maendeleo gani katika jamii zenu. Envaya imekupa website ya bure kabisa – itumie kikamilifu. Usipuuze fursa hii. Jaribu kuweka taarifa mara kwa mara kuhusu miradi na mipango ya baadae, taarifa za mawasiliano na jitangaze duniani kote.
Mwisho kabisa, baadala ya kusubiri ruzuku kutoka nje shirika lako linaweza likasimamia njia njingeni za kupata pesa kupitia hafla za kihisani, hata kwaajili ya miradi midogo midogo. Shughuli za kihisani zinaweza zikachukua sura tofauti: kwanzia kuuza vitabu vya zamani, na nguo au hata kufanya matukio ambayo yanaweza kuhudhuriwa na watu kwa viingilio. Moja ambayo imechukua chati sana hivi karibuni mkoani Dar-es-salaam, ni Mechi Ya Mpira Wa Mguu Wa Kihisani ulio husisha waigizaji wa filamu(bongo movie stars) wa hapa tanzania wakishindana na waimbaji wa muziki wa bongo flava. Inasemekana kuwa zilichangishwa millioni 100 kutokana na hafla hii na zote zilienda kwenye misaada kwenye sector ambayo waliokuwa wanai support.
Mfano wa uchangishaji wa fedha uliofanya hivi karibuni kutoka Rwanda ni ule wa Taasisi ya sayansi na teknolojia inayohusika na jamii ya wanafunzi iliyopo jijini Kigali (KIST). Wanafunzi hawa walifanya kongamano la muziki wakitumia vipaji na kalama zao ili kuwezesha uchangishaji wa hosteli za kulala kwa wanafunzi wa kike na kuwatia moyo wanafunzi wa kike kuingia katika taasisi ya teknolojia. Tamasha hili la uchangiaji lilihudhuriwa na wageni mbalimbali walioalikwa, wanafunzi, wanamuziki na watu mbalimbali walioshirika tamasha hili. Katika tamasha hili la uchangishaji kilipatikana kiasi cha farangha 821,000 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania milioni mbili. Tamasha hili dogo na rahisi liliandaliwa na wanafunzi wenyewe japokuwa halikufanikiwa kupata pesa kama matarajio yalivyokuwa lakini ni mwanzo mzuri.
Lakini hii isikuvunje moyo kwani si lazima utafute wasanii au waigizaji ili uwezeshe matukio kama haya...unaweza tu ukafanya matukio katika mtaa wako tu ukahusisha wasanii wadogo wadogo ambao wako mtaani kwako vijana wanao cheza ngoma za asili na kuigiza, na mambo mengine mengi sana ya ki burudani na unaweza ukaalika walioko karibu na mtaa wako wahudhurie waone vijana wamewaandalia nini. Tafuta kitu ambacho kinafurahisha jamii , kama ni michezo basi tafuta hata TV uonyeshe michezo kwa bei nafuu, hata shilingi 500/= tu. Au kuna uwezekano wa kuandaa maigizo na muziki, basi hata hivyo itapendeza.
Shirika lisio kuwa la kiserikali linaweza kukimu mahitaji yake ya kifedha bila kutegemea watoa ruzuku kila mara. Ki uhalisia inasaidia shirika lako kujenga uamnifu zaidi na kuonyesha kuwa unamapenzi na jamii yako na hufanyi shughuli hizi ili kujivunia na kujiwezesha tu mwenyewe,
Je una mawazo yeyote au mada unayotaka uchangie kwenye makala hii? Umewahi kufanya shughuli za kihisani na ukafanikiwa? Tujulishe imeendaje, changamoto na mambo uliyojifunza...acha mawazo yako kwenye nafasi iliopo hapo chini
UTEKELEZAJI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI KWA MWAKA 2012
Hili ni zoezi la nne la sensa ya watu na makazi tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania mwaka 1961. Sensa hii hufanyika baada ya miaka kumi kama utaratibu ulivyo tangu kuanza kwa zoezi hili. Kwa mwaka huu zoezi lilianza tarehe 26/08/2012 kwa nchi nzima.Umuhimu wa zoezi hili ni kujua idadi ya watanzania na makazi yao ili serikali iweze kupanga mikakati yake ya maendeleo katika sekta mbalimbali kama vile afya, kilimo, elimu, miundombinu, uwekezaji na sehemu nyingine muhimu. Pia zoezi hili linaiwezesha serikali kujua namna ya kugawanya rasilimali zake kwa wananchi wake.
Watanzania waliamshwa na makalani wa sensa katika kuhesabiwa na kuulizwa maswali kama, “ni nani aliyelala na kuamkia kwenye familia hii?”. Kabla ya serikali kuanza kutekeleza zoezi hili tulisikia juu ya kugoma kwa makalani kutokana na kwamba walicheleweshewa malipo ya posho zao kama yalivyokuwa mapatano yao na serikali, pia tulisikia migomo mbalimbali kutoka kwa raia, viongozi wa dini na wenyeviti wa vijiji katika kona mbalimbali za nchi kwa madai ya kutoshiriki zoezi la sensa.
Kufuatia hayo yote, Envaya kama shirika la kijamii liliamua kufanya utafiti ili kujua utekelezaji wa mchakato mzima. Timu yake ilifanya utafiti wake kwa asasi zifuatazo ; AWITA, BRIGHTY Destiny TANZANIA, KINONDONI NETWORK OF PEOPLE LIVING WITH HIV, TANZANIA SCIENCE JOURNALIST ASSOCIATION , WAYETA n.k utafiti huu ulikuwa katika mundo wa dodoso na tuliwahoji wawakilishi wa asasi zote ambazo zimetajwa hapo juu ili kupata maoni yao juu ya utekelezaji wa zoezi la sensa 2012.
Mfano mmoja wa mhojiwa ambaye aliomba jina lisiandikwe, aliilaumu serikali kwa kushindwa kutoa elimu ya kutosha kuhusu sensa kwa wananchi,aliendelea kusisitiza kuwa wananchi wengi wa Tanzania hawajui maana na madhumuni ya kuhesabia. Endapo raia wangekuwa wameelimishwa vizuri nadhani haya maandamano na migomo isingetokea. Aliendelea kusema "baadhi ya maswali yanakuja akilini mwetu kwamba : kwani serikali ya Tanzania haijawahi kufanya zoezi kama hili kwa miaka iliyopita? Sasa mbona tunakuwa wageni wa jambo hili? Hii sasa hivi ni sensa ya nne katika nchi yetu kwanini tumeshindwa kujirekebisha? Matatizo yanajirudia yaleyale mfano; tunasikia sare za makalani hakuna, posho hakuna, vitendea kazi hakuna kwa ujumla kwanini serikali inashindwa kujirekebisha? Alisisitiza mhojiwa mbele ya timu ya Envaya kwa kusema serikali yetu inaigiza sana!”
Baadhi ya watu wanaona zoezi la sensa kwa wiki nzima ni muda mrefu na halina maana, wakati wengine wanakiri na kusema kwamba ni zoezi ambalo lina umuhimu mkubwa sana kwa nchi. Pia kuna wengine ambao wanaliona zoezi hili la sensa kama utamaduni tu wa kila baada ya miaka kumi lakini kimsingi halina maana.
Mwanamke kutoka AWITA alisema "baadhi ya watu walishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa zoezi hili, lakini japokuwa walishiriki wala hawaoni faida yoyote ya kuhesabiwa. Alisema “hatuoni faida yoyote na wala hakuna dalili zozote za mabadiliko katika maendeleo, naona serikali inafanya zoezi hili ili labda tu kujisifia mbele ya mataifa mengine kwamba ina idadi kubwa ya watu. Baada ya sensa huwa hatuoni taarifa yoyote kurudi kwa wananchi, na kuambiwa mikakati yoyote ya kimaendeleo itakayofanyika baada ya zoezi la sensa”.
Timu ya Envaya iligundua kuwa baadhi ya maeneo kulikuwa na hali ya kutoelewana baina ya wenyeviti wa mitaa/vijiji na makalani wa sense. Eneo kama la Manzese makalani wengine walipata shida sana kwa sababu walikuta nyumba nyingine zimefungwa na hakuna mtu. Wengine walifukuzwa kwa visu na mapanga na pia makalani wengine walishindwa kuruhusiwa kwenye familia zingine kufanya zoezi hilo kwasababu hawakuwa na sare za kazi. Alisisitiza kijana kutoka asasi ya BRIGHT DESTINY TANZANIA (BDT).
Wengi wa waliohojiwa kupitia dodoso za timu ya Envaya walisema suala la kugomea zoezi la sensa kwa baadhi ya wananchi ni kutokana na ukosefu wa elimu ya sensa. Walisema kama serikali ingekuwa imetoa elimu ya kutosha kwa wananchi wake maana ya sensa, umuhimu na faida zake hakuna mtu hata mmoja angegoma kuhesabiwa. Walisema pia serikali haipaswi kuwashitaki wale waliogomea zoezi hili kwasababu si kosa lao bali ni kosa la serikali yenyewe kutokutoa elimu ya sensa.
Vile vile, waliohojiwa walisema ili serikali kwa siku za usoni iweze kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi mkubwa lazima ishirikishe kwa ukaribu sana viongozi wa ngazi za chini kabisa kama wajumbe na mabalozi kwa maana hao ndo wanaishi karibu na jamii zao wanazielewa familia zote kwahiyo taarifa zitakazotolewa kwa kalani mbele ya mjumbe zinakuwa zina ukweli mkubwa. Sahivi watu hawatoi taarifa za ukweli kwa makalani kwa sababu hawawajui na kulingina na mila zetu mtu hawezi kutoa taarifa zenye ukweli kwa mtu asiyemjua.
Alisema mmoja wa mhojiwa, kwa sababu sensa ina umuhimu katika kuweka misingi ya kimaendeleo ya nchi, kama serikali itakuwa inatoa taarifa kwa wananchi ya nini kimefanyika baada ya sensa, watu wataelimika na watakuwa tayari kuhesabiwa kwa hiari kabisa na si kwa kulazimishwa kwa sababu watakuwa wameshajua umuhimu wa kuhesabiwa.
Alisema mmoja wa mhojiwa, pia natoa ushauri kwa viongozi wote wa dini lazima kuwaelimisha wafuasi wao juu ya umuhimu wa sensa katika nchi yoyote badala ya kuwahimiza kugoma, kwa sababu viongozi wa dini wana nguvu na ushawishi mkubwa sana kwa waumini wao.
Fikira iliyotawala juu ya zoezi lote hili la sensa ni kwamba wananchi wanahitaji kujua zaidi kuhusu umuhimu wa zoezi hili ambalo hufanyika kila baada ya miezi 10. Ndani ya wiki ya zoezi hili la sensa tumeona vipindi vingi kwenye runinga na kusikia kwenye maredio kuhusu umuhimu wa sensa, lakina bado jamii inahitaji taarifa zaidi ili kuelewa haswa sensa ina umuhimu gani na inamaana gani. Kwa bahati mbaya watu wengi wamegundua baadae sana umuhumu wa sensa ambapo zoezi limeshamalizika. Ni jukumu letu kama mashirika madogo na makubwa yasiyo ya kiserikali kujua umuhimu wa sensa na kuelimisha jamii zetu. Kama tunaona hata sisi wenyewe hatujaelewa tusisite kufuata taarifa serekalini hata kuomba semina kwaajila ya mashirika kama yetu ili tuweze kuelewa na kuelewesha jamii zetu kuhusu zoezi hili...
Toa maoni yako hapo chini!
Ushiriki wa asasi za kiraia katika kuachana na mila hatarishi katika Tanzani
Tanzania ni nchi yenye utajiri wa mila na utamaduni na hujivunia hazina za urithi wao.Utamaduni wa kitanzania ni mzuri sana wenye heshima na adabu katika jamii. lugha rasmi nchiniTanzania ni Kiswahili lakini pia watu wengi huzungumza Kiingereza. Watu wa Tanzania wanajulikana sana kwa ukarimu na upole.
Kuna uelewa ambao unaendelea kukua nchini Tanzania wa madhara yanayosababishwa na tamaduni si tu kwa ajili ya watoto na vijana bali pia kwa wanawake. Uelewa huu umesababishwa kwa kuibuka asasi mbalimbali za kiraia ambazo zimekuwa zikifanya kampeni kwa ajili ya kukomesha tamaduni mbaya katika jamii.Asasi hizi ni pamoja na TAMWA, WAMA, AFRICAN Upendo GROUP, TAWA na TUNAWEZA WOMEN GROUP ambazo zinapinga unyanyasaji dhidi ya wanawake. TGNT na SWAAT hupambana na ubaguzi wa kijinsia na wanawake walio katika hatari ya kuambukizwa VVU / UKIMWI. KULEANA ambayo inakabiliana na kukomesha adhabu ya viboko kwa watoto na TANZANIA ALBINO SOCIETY ambayo inatetea mauaji dhidi ya binadamu wenye ulemevu wa ngozi (albino).
Sehemu kubwa ya jamii za kitanzania wana utaratibu wa kurithi wajane, mwanaume aliyefiwa na mke wake anaweza "kuoa" ndugu wa marehemu mke wake kwa lengo la kutunza watoto wa dada yake ambao pia huonekana kama watoto wake. Familia ya mwanamke aliyefariki huwa ni jukumu lao kumpatia mkwe wao mbadala wa kumrithi mke wake aliyefariki, na familia inaweza kumchagua binti yeyote kutoka kwenye familia bila hata makubaliano kati ya mume na binti anayemrithi dada yake. Utamaduni huu ni wa hatari sana maana unaweza kuleta maambukizi ya ukimwi kwa mwanamke anayerithiwa na mume aliyefiwa na mke, inawezekana dada yake alikufa na VVU naye pia atapata maambukizo hayo.
Ukeketaji-Katika mikoa kadhaa nchini Tanzania jambo hili limekuwa ni la kawaida, ambapo jamii hizo zinaelezea kwamba ukeketaji unadhibiti kujamiiana kwa mwanamke na kwa hivyo inapunguza nafasi ya mwanamke kuwa na wapenzi wengi. Ukeketaji ni hatari katika afya ya uzazi kwa sababu huathiri haki ya mwanamke kufurahia tendo la ndoa na zaidi inaweza kumsababishia ugonjwa wa fistula wakati wa kujifungua endapo makovu ya kidonda kitakapochanika na kusababisha kutokwa na damu nyingi ambayo pia inaweza kuwa mbaya. Nchini Tanzania vitendo hivi vinafanywa na baadhi ya makabila machache, hivyo hata kampeni ya kukomesha vitendo hivi inaonekana kufanikiwa sana.
Mauaji ya Albino. Mauaji ya albino yanasababishwa na fikra potufu katika jamii kama vile (uchawi, mali, siasa nk) na ubaguzi wa rangi.Utokomezaji wa mauaji haya umekuwa ni mgumu sana, hii inatokana na kukosekana kwa sheria ya uchawi, ukosefu wa utayari wa serikali, na kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi katika nyanja ya utamaduni. Kwa kutaja baadhi ya hayo machache hufanya mbinu za kuzuia mauaji kushindwa na hatimaye kuongezaka kwa mauaji hayo. Ni mpaka matatizo haya yote yashughulikiwe haraka ndipo wenzetu albino nchini Tanzania watakuwa salama.
Ndoa za mapema. Wasichana bado wanabaguliwa katika jamii nyingi za kitanzania, kwasababu wasichana wadogo wenye umri kuanzia miaka 11 wanaachishwa shule na wazazi wao ili waolewe. Kwa upande wa afya jambo hili ni ni hatari, kwa sababu viungo vya msichana huyu havijakomaa kwa hivyo wengi viungo vyao hupasuka wakati wa kujamiiana, na hivyo kusababisha maambukizi ya VVU au mimba za mapema. Utafiti unaonyesha wasichana wengi wameachishwa shule ili kuolewa au kujiingiza mapema katika vitendo vya ngono ili kujitegemea kifedha hasa ukosefu wa ajira na umaskini miongoni mwa wasichana, ukosefu wa taarifa kuhusu masuala ya ngono na ujinga na ukosefu wa elimu miongoni mwa wasichana.
Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na kumtolea matusi mwanamke, kumshika na kumgusa mwili wake bila ridhaa mfano kwenye nywele, makalio, au matiti. Kuonyesha picha za utupu za wanawake, kumwonyesha mwanamke picha za ngono bila ridhaa yake na kumwongelesha maneno ya kashifa mwanamke wakati anapopita mbele ya wanaume, kumbaka na kumpiga mke wako kama ishara ya upendo katika baadhi ya makabila.
Mahudhurio ya Mwanaume kliniki. Katika jamii nyingi za kitanzania kina mama tu ndio huwa wenye jukumu la kuhudhuria kliniki. Wakati pia ni jambo la muhimu sana kwa kina baba kuwasindikiza wake zao kliniki ili kupata ushauri na nasaha mbalimbali, pia kupata elimu juu ya masuala muhimu sana yahusuyo uzazi wa mpango na VVU. Pamoja na hayo yote serikali inapaswa kujaribu kuzifanya kliniki ziwe rafiki kwa wanaume kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake ambao wanahudhuria kliniki na waume/wapenzi zao na pia wanaume ambao huleta watoto wao.
Mauaji ya wanawake wenye macho mekundu. Cha kushangaza mamia ya wanawake wazee wanauawa kila mwaka kwa tuhuma za uchawi baada ya kupata wao wanachokiita ukweli kutoka kwa baadhi ya waganga wa jadi.Wengi wa wanawake wazee wenye macho mekundu wanauawa hasa katika ukanda wa ziwa victoria, watu hushindwa kuelewa kwamba wanawake wenye macho mekundu wameathiriwa na moshi wakati wa kupika. Wanapopika kila siku kwa kutumia majiko ya kuni wanavuta hewa yenye kiasi cha gesi ya sumu. Kutokana na uhaba wa kuni, wakati mwingine mavi ya ng'ombe hutumika kama mbadala kwa kuni. Hivyo kwa kutumia nishati za kupikia ambazo hazina ubora husababisha macho kuwa mekundu.
a
Kujitolea katika Afrika Mashariki
Neno Kujitolea si geni kwa mtu yeyote, ni kutoa muda wako, uwezo, maarifa na huduma mbalimbali kwa manufaa ya jamii kwa ujumla, bila kutarajia malipo yoyote au fidia. Kujitolea ni moja ya njia kuu ambayo raia wa kawaida wanaweza kuitumia katika kuendeleza Jamii zao..
Kumekuwa na juhudi za muda miaka mingi sasa jinsi Waafrika wanavyopaswa kujipatia maendeleo yao wenyewe kwa kupunguza utegemezi kutoka nchi zilizoendelea kiuchumi.Katika ngazi kuu ya kiuchumi hii inamaanisha kukata utegemezi wa misaada ya nje au bidhaa kutoka nje, lakini katika ngazi ya kiuchumi hii ina maana kuwa Waafrika wenyewe lazima kushiriki na kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya mataifa yao. Kujitolea katika mipango ya kijamii ni njia kubwa ya kuwa sehemu ndogo lakini kubwa ya maendeleo ya taifa. mfano mkubwa na maarufu ni kutoka kwa Wangari Maathai, ambaye alianza kujitolea na baadhi ya wanawake katika kupanda miti maeneo ya vijijini nchini Kenya, ambayo sasa imekuwa ni moja ya harakati kubwa ya kuokoa mazingira yetu ya Afrika.
Mbali na hisia binafsi za kuridhika na kutimiza haja katika kuhudumia mataifa yao, Kujitolea kunamuwezesha mtu kupata ujuzi na uzoefu ambao utakuwa na manufaa hapo baadaye katika kupata ajira. Ni kawaida kwa waajiri kuangalia watu wenye uwezo na uzoefu wa kazi. vijana wengi wasiokuwa na ajira wamekuwa wakilalamika kuwa hawana uzoefu lakini kujitolea ni njia nzuri na rahisi ya kutatua tatizo hili.
Nchini Tanzania, utamaduni wa kujitolea si sana, ni nadra sana kumkuta mtu akijitolea muda wake wote na rasilimali zake, bali labda kuwe na sababu mbalimbali za msingi. Hii inatokana na mfumo wa elimu inayotolewa hapa nchini, mitaala ya elimu ya Tanzania haiongelei wanafunzi kujitolea katika huduma za jamii kama ilivyo kwa wenzetu katika nchi za magharibi.katika nchi zilizoendelea ili mwanafunzi afaulu mtihani lazima afanye pia huduma za jamii kuna baadhi ya masaa kwa wanafunzi ni kuhudumia shughuri za jamiii. Elimu ya Tanzania iko kinadharia zaidi na si kivitendo.
Pia tatizo lingine linaweza kuwa ni ukosefu wa upatikanaji wa taarifa kwa urahisi kutoka kwa asasi zetu kwa wenye nia ya kujitolea. Ni vigumu kwa wanaotaka kufanya huduma hii kama hawana taarifa ya uhitaji huu.kuna mashirika mengi ya kimataifa yanayohitaji watu wa kujitolea, mashirika haya yamefanikiwa kufahamika duniani kote kwa sababu ya urahisi wa taarifa zao,taarifa zao wamezisambaza kwa njia ya mtandao. Fursa ya kujitolea kwa Tanzania ni dogo sana na kivitendo haupo kwa sababu mashirika yetu ya kiraia hayana uwezo wa kutangaza fursa hii kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.
Lengo la Envaya limekuwa daima katika kutatua tatizo la usambazaji wa habari kwa ajili ya asasi ndogo, na katika hili envaya sasa imezindua kipengere kipya katika tovuti yake cha Kujitolea ambapo asasi zinaweza kuweka tangazo kama wanahitaji watu wa kujitolea. Ukurasa huu utawafikia vijana, wanafunzi wa vyuo vikuu, wasiokuwa na ajira na wale walio tayari kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu. Tunataka kuongoza harakati ya kupata Watanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kushiriki katika mipango ya maendeleo yaowenyewe, hii ni pamoja na kujenga nafasi kwa ajili ya mipango ya kijamii na kujitolea kiutendaji.
Je! Unafikiri nini juu ya dhana hii ya kujitolea na changamoto zake? Je posted up kujitolea nafasi yako bado? Jisikie huru kutupa majibu juu ya kipengere cha kujitolea ambacho kimewekwa na envaya - http://envaya.org/pg/volunteer. Tafadhari andika maoni yako hapo chini- asante sana.
Wiki ya Chanjo nchini Tanzania
Wiki hii ni wiki ya chanjo nchini Tanzania. Tukio hili limeanza rasmi tarehe 23 na litamalizika tarehe 28 ya mwezi huu wa nne. Kitaifa Tukio hili linafanyika Mkoani Mwanza lenye kauli mbiu “ Watoto wasiochanjwa ni wengi. Tokomeza ugonjwa wa Polio” Maudhui ya kauli mbiu hii ni kuchukua hatua za haraka katika kuokoa maisha ya watoto kutokana na magonjwa yanayozuilika kwa njia ya chanzo.
Hii ni fursa pekee kwa asasi za kiraia katika kusambaza habari na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hii. Asasi kama ANPPCAN, AACD na Children Care Development Organizations ni asasi zinazofanya kazi moja kwa moja na kaya, kwahiyo asasi hizi zinaweza kufanya mambo mengi katika kuongeza uelewa juu ya thamani na umuhimu wa chanjo kwa watoto.
Pia ni changamoto kwa Serikali kuweka nguvu zake na kuhimiza jambo hili kwa kuzitumia asasi za kijamii ili kufikisha ujumbe katika jamii,hii ni pamoja serikali kutoa rasilimali za kifedha na kiufundi ili kuokoa maisha ya watoto na surua , polio na magonjwa mengine yanayozuiwa kwa njia ya chanjo. Timu ya Envaya inatoa shukrani zake za dhati kwa asasi za kijamii, mashirika ya maendeleo na nchi wanachama kwa juhudi zao za pamoja katika suala hili.
Hata hivyo, licha ya mafanikio ambayo serikali ya Tanzania imeyapata, mengi bado hayajafanyika hasa katika baadhi ya mikoa ambayo bado iko nyuma kimaendeleo.Bado kuna watoto wengi sana ambao hawajapata chanjo kwahiyo wako katika hatari ya maambukizo,kwahiyo serikali tunaomba ichukue hatua za haraka katika kuokoa janga hili, hii ni pamoja na kuzishirikisha asasi hizi za kiraia katika kutoa elimu ya afya hasa kwenye maeneo ya vijijini.
Je! Asasi yako imeshiriki au kuhusika kwa namna yoyote katika kusaidia suala hili?
Karibu ujadili au toa maoni yako kuhusiana na hili...

The 2012 Echoing Green Semifinalists | Echoing Green
www.echoinggreen.org
There are 3,508 reasons why we have great hope for a better world. This is the number of applications Echoing Green received for our 2012 Fellowships. We congratulate every single applicant for taking on the world's biggest problems with their bold, innovative solutions.

@envaya is a Semifinalist for the 2012 Echoing Green Fellowship! Very excited and honored: http://t.co/0HPCUqWz #EG2012Fellowship