Fungua
CHARITY ROVING ORGANIZATION

CHARITY ROVING ORGANIZATION

TUKUYU, Tanzania

        Charity Roving Organization ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na maendeleo ya jamii kwa ujumla,kifupi chake ni CHARIOT. Makao makuu ya shirika hili yapo katika kijiji cha Itete Kabembe katika wilaya Rungwe mkoa wa Mbeya nchini Tanzania. Kipaumbele cha shirika hili ni kuwasaidia watoto wanaosoma na wasiosoma. Pia shirika lina malengo mengine kama ifuatavyo;

  •          Kuondoa umaskini na ujinga kwenye jamii. Kuhakikisha rasilimali watu na zile za asili zinatumiwa na jamii kwa mgawanyo ulio sawa.

         Kuyafikia makundi mbalimbali  katika jamii yasiojiweza kama vile wajane,watoto yatima

  •          Kuendeleza afya ya jamii,afya ya uzazi na kupambana na ukimwi.
  •          Pia uangalizi wa watoto na vijana. Hii inajumuisha kuwasaidia watoto wale wanaosoma na wasiosoma. Kuwafundisha vijana shughuli mbalimbali za kisanii kama vile ngoma,maigizo ili waweze kukuza vipaji vyao na kujiongezea kipato. Shirika hili pia litafanya jitihada za kuwaunganisha vijana na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali.
  •          Kufungua vituo vya mafunzo ya kompyuta na mtandao (internet) katika maeneo ya vijijini, ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo kupata uelewa wa kompyuta jinsi ya kutumia ili ziwaletee maendeleo na kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu.
  •           Chariot pia itatoa elimu ya uraia. Shirika litatoa elimu kwa jamii kuhusu haki za binadamu, usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake na vijana kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile za kisiasa, kiuchumi. Pia kutoa elimu kuhusu katiba ya Tanzania.

 

           

Mabadiliko Mapya
CHARITY ROVING ORGANIZATION imeongeza Habari.
JENGO LA CHARIOT lilipofikia kwa sasa na ujenzi bado unaendelea,
9 Oktoba, 2012
CHARITY ROVING ORGANIZATION imeongeza Habari 4.
3 Oktoba, 2012
CHARITY ROVING ORGANIZATION imejiunga na Envaya.
2 Oktoba, 2012
Sekta
Sehemu