Coast Region Poverty Reduction Initiatives (COREPRI)
P.O.BOX 30080, Kibaha, Coast Region.
Email: corepri@yahoo.com
Phone: 0754572160 /0787557924,
Website: http://www.envaya.org/corepri
===============================================================
Kumb. COREPRI/ GN/11/10 09TH March 2011
Kwa Wadau wetu…………
YAH: MWALIKO WA KUSHIRIKI SEMINA YA WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA (VOLUNTEERS) NA WANACHAMA WA COREPRI KUHUSU KUJADILI SHUGHULI ZILIZOFANYIKA, KUIBUA MIRADI NA MIPANGO KAZI WA COREPRI KWA KIPINDI CHA JANUARI – DESEMBA 2011.
Ndugu, tafadhali rejea somo lililotajwa hapo juu,
COREPRI ni Asasi ya kiraia iliyoanzishwa mwaka 2007 na kupata usajili mwaka 2009. Lengo kuu la Asasi hii ni kushirikiana na Serikali katika vita vya kupambana na umaskini kwa kutumia fursa zilizopo ili kuleta maendeleo endelevu. Kwa mantiki hiyo Ofisi ya COREPRI ikishirikiana na shirika la Foundation for Civil Societies (FSC) wameandaa semina itakayosaidia katika kupanga na kutekeleza shughuli za Asasi.
Kwa niaba ya kamati ya maandalizi napenda kutumia fursa hii kukualika kushiriki katika semina itakayofanyika Countryside Motel, Mailimoja – Kibaha siku ya Jumanne, tarehe 15.03.2011, semina itaanza saa 2.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.Tafadhali zingatia muda. COREPRI na FCS watagharamia ukumbi, vifaa vya mafunzo, posho ya kikao na nauli ya basi kwa wanaotoka mbali tu.
Ni matumaini yangu kwamba utashiriki katika semina hii muhimu.
Ahsante.
R.M. Wanjara
Katibu - COREPRI