Chavita imetoa mafunzo ya Lugha ya Alama kwa Taasisi za serikali na Wazazi wanaoishi na
Watoto Viziwi katika kata 5,ambazo ni Bereko,Kondoa mjini,Pahi,Kilimani na Chemchem
katika Wilaya ya Kondoa.
Mafunzo ya lugha ya alama kwa Taasisi za serikali wameliona kama Lugha ya Ajabu aidha
jamii bado wanaona lugha ya alama ni ngeni kwao walikuwa Hawajui kama Viziwi wana
lugha maalum ya Mawasiliano .
Sasa wamepata mwamko wa Lugha ya alama ya Viziwi kwasasa wameona umuhimu wa
kuwa nayo na kujifunza lugha ya alama ya ishara kwa bidii sana ili waongeze tija na uelewa
kwa Viziwi.
Upande wa wazazi nao walikuwa wanaona kama Lugha ya Vichaa kwasasa wamepata
mafunzo haya wanaona ni Lugha sawa mtu anaeongea na mtu wa kawaida.
Wamehamasika sana na lugha hii walikuwa wanatamani iwe hata siku 20 kwa mafunzo haya
ya viziwi.
Wazazi wenyewe wameweza kufungua kikundi chao ambacho inaitwa (UWAVIKO) yaani
Umoja wa Wazazi wa Viziwi wilaya ya Kondoa.
Kikundi hiki cha wazazi lengo lake ni kusaidiana na CHAVITA ili kufikisha ujumbe kwa
wazazi wote.
CHANGAMOTO
Kulikuwa ma vikwazo vya mawasiliano hasa katika lugha ya Alama ya viziwi
Ujumbe ulikuwa unachelewa kufika kwanza ipitie kwa mkalimani ndio watu wapata ujumbe
huu wa mafunzo ya Lugha ya Alama ya viziwi.
Kutokujua lugha ya Alama ni nini? Ukiziwi na ububu kuna tofauti gani katika mawasiliano
jambo la ajabu Viziwi hawataki kuitwa neno Bubu haina maana yoyote usipokuwa hakuna
mawasiliano. Viziwi si mabubu bali Walemavu wa kutosikia au Kiziwi/Viziwi
Mtu anasikia vizuri ila hawezi kuongea tutamwiitaje jibu limeshindwa kupatiwa ufumbuzi
MAFANIKIO
• Taasisi za serikali wamehamasika na Lugha ya Alama ya Viziwi
• Kufunguliwa kwa Kikundi cha Umoja wa Wazazi wanaoishi na Viziwi Wilaya ya kondoa
(uwaviko)
• Kupata uzoefu wa kuendelesha mradi wa mafunzo ya Lugha ya Alama
• Wamehamasika na Lugha ya Alama kwa Jamii katika kata 5 zilizopitiwa Mradi wa mafunzo ya
Alama ya Viziwi katika wilaya ya kondoa