Envaya

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UIMARISHAJI WA ASASI ULIOTEKELEZWA NA YOFSAO

UTANGULIZI.

YOUTH FIGHTY FOR SOCIAL AWARENESS ORGANIZATION (YOFSAO) ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka 2009 na kusajiliwa mwaka 2011 chini ya sheria ya NGOs ya mwaka 2002.Shirika lina wanachama 25 kati yao 7 wanaume na 18 wanawake.Makao makuu ya shirika yapo Mlamleni kata ya Tambani Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.Lengo kuu la shirika likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kupunguza vifo vitonanavyo na maambukizi ya vvu huku shirika likidhamiria kupunguza maambukizi ya vvu na athari zitokanazo.Msingi mkuu wa ufanikishaji wa malengo wa YOFSAO ni kujitolea sambamba na matumizi ya rasilimali zinazo tuzunguka.

SHUGHULI ZA SASA ZA SHIRIKA.

  • Kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya maambukizi ya vvu, athari za Dawa za kulevya,stadi za maisha , afya ya uzazi ,elimu rika ,ujasiliamali na Mazingira.
  • Kutembelea na kutoa misaada kwa makundi yaliyoathirika na dawa za kulevya na vvu.
  • Kuhamasisha uundaji na uendelezaji wa mitandao ya kijamii.

 

WALENGWA

  • Vijana ndani na nje ya shule
  • Watoto
  • Wazee wasiojiweza.

MAENEO YA KAZI

  • Mashuleni
  • Vijiweni
  • Majumbani

HAJA YA MRADI HUU.

Kutokana na uwepo wa maambukizi ya vvu katika kata yetu hususani katika kijiji cha Mlamleni kumepelekea vifo vingi vilivyotokana na ukimwi huku vikiacha watoto yatima wasio na msaada wowote,sambamba na kuporomoka kwa uzalishaji mali hususani katika shughuli uzalishaji mali mashambani (kilimo).

katika kupunguza tatizo lililopo kwa kukusanya nguvu za pamoja na kuweka malengo yatakayotuwezesha kupunguza tatizo hilo.Ndipo mwaka 2009 YOFSAO ilianzishwa.

Kutokana na utekelezaji wa shughuli za kila siku za YOFSAO ilibaini mapungufu kadha wa kadha ambayo yaliainishwa na wanachama kuwa ni

  • Ukosefu wa vitabu vya kumbukumbu za mahesabu na taarifa za mahesabu.
  • Kukosekana kwa malengo yaliyowazi kwa wanachama na yenye mwelekeo maalum.
  • Kukosekana kwa mifumo na miundo iliyowazi ya uongozi na ya kiutendaji.
  • Kushindwa kubuni na kuaandaa miradi shirikishi ya kijamii.

Baada ya kubaini mapungufu hayo wanachama kwa pamoja tulikubaliana kuomba ufadhili toka katika mashirika ambayo yanatoa ruzuku katika maeneo hayo.Shirika tuliliona kuwa tunaweza kukidhi vigezo vyake ni FCS (Foundation for civil society) ambapo tulikaa kikao na kuunda kamati ya maandalizi ambayo ilifuatilia fomu za maombi na kuzijaza na kisha kuzituma .FCS walikubaliana na wazo letu na kisha kuamua kutupatia ruzuku ya T-sh 7,480,430/= (Milioni saba ,laki nne ,themanini elfu na mia nne therathini tu),ambazo zimetuwezesha kuendesha shughuli zifuatazo ;-

1)      Mafunzo juu ya uandaaji wa miradi shirikishi.

Mambo ambayo yamejadiliwa katika mafunzo haya nipamoja na

  • Uibuaji wa matatizo katika jamii
  • Ushirikishaji wa wadau
  • Jinsi ya kubuni mradi
  • Kuandaa viashiria
  • Namna ya kuhakiki viashiria
  • Dhahania
  • Na namna ya kuandaa mpango wa kazi
  • Namna ya kuandaa mpango wa ufuatiliaji na tathimini.
  • Namna ya kuandaa taarifa ya utekelezaji wa mradi.

 

SEHEMU YA 1: UTANGULIZI

A: JINA KAMILI LA ASASI

YOUTH FIGHTY FOR SOCIAL AWARENESS ORGANIZATION (YOFSAO)

                                           

C: KUHUSU BARAZA LA KATIBA

  1. BARAZA LILIFANYIKA WAPI: MKURANGA KATA YA KITOMONDO
  2. Washiriki : Me   50_ KE_80_Jumla 130

                        

SEHEMU YA PILI: YATOKANAYO NA BARAZA

D: MAREKEBESHO/ MAPENDEKEZO KATIKA SURA NA IBARA MBALIMBALI ZILIZOMO KATIKA RASIMU

 

SURA (ibara, kifungu)

INAVYOSOMEKA               SASA

MAPENDEKEZO/MAREKEBISHO

MAELEZO/ SABABU

1

Sura 4

44(1)

(a)Kuheshimiwa, kutambuliwa na kutendewa kwanamna ambayo haishushi utu wake.

(b)Kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika shughuli za kijamii

(c)Kuwekewa mioundombinu na mazingira yatakayoyowezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata habari

(d) Kutumia lugha za alama, maandishi ya nukuta nundu au njia nyingine zinazofaa.

(f) Haki ya kupata ajira na kugombea nafasi ya uongozi katika nyazifa mbalimbali kwa usawa.

Wanapendekeza kuwa na Mbunge wao atakayewawakilisha Bungeni ili kukidhi matakwa yao.

-

-Watoto walemavu ambao wazazi wao ni walemavu wapewe elimu bure kuanzia ngazi za awali hadi ngazi za chuo kikuu

-Selikari iwapatie matibabu bure,

-Walemavu wasishitakiwe,

-Wapewe fursa ya ajira,

-Wawekewe vyombo vya babari vyenye utafsiri wa lugha yao,

-Kuwa na mfuko maalum wa walemavu

-Kuchagua wenyewe wawakilishi wetu bungeni,

 

Kama kutakuwa na Mbunge mwenye ulemavu basi atawakilisha vizuri xana wananchi wengine ambao ni walemavu

 

-Hi ni kutokana na walemavu kukosa ajira na kunyanyapaliwa kwa kwani hata kama ana elimu ya kutosha kuajiriwa kwake kutakuwa kugumu sana kwani waajiri wengi wanaohisi kuwa watu hawa hawawezi kufanya kazi ipasavyo.

2

23

Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka katika serikali na jamii kwa mujibu wa sheria.

Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka katika serikali na jamii kwa mujibu wa sheria na hakutakuwa na namna yoyote ya kutoa uhai wa mtu.

Mungu peke yake ndiya mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa mtu.

3

105(2)(b)

Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia   uwiano wa washirika wa Muungano.

Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia   uwiano wa washirika wa Muungano.

Ili waweza kuwatetea walemavu wenzao ipasavyo.

4

1 (2)( 2)

Eneo la Jamahuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya Bahari.

Eneo la jamuhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari na anga

Hakuna Tanzania bara unapoitaja Zanzibar bali kuna Tanganyika

5

 

11(2)(1)

Lengo kuu la Katiba hii ni kulinda, Kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wa wananchi wa JAMHURI YA Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.

Lengo kuu la Katiba hii ni kulinda, Kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na mshikamano   wa wananchi wa JAMHURI YA Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, uongozi bora na kujitegemea.

 

Utengeno utatufanya tugawanyike na mneno utawala linafanya viongozi watutawale na sio kuongoza kwa yale tuliowatuma .

 

 

 

 

 

6

Ibara 22(1)

Binaadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa tangu kutungwa kwa   mimba.

Binaadamu wote huzaliwa huru na wote ni swawa tangu kutungwa kwa mimba.

(a)Kutokana na tamko hilo haliko kwenye katiba haki ya huduma ya mama na mtoto haikuwa halali kwenye katiba.

(b)Kutokana na tamko hilo haliko kwenye katiba litapeleka uharibuji wa mimba.

(c) Haki za walemavu hazitakuwepo kwa wale   walio tumboni kwa sababu ya technologia inayoonyesha mtoto mlemavu na kuitoa mimba hiyo.

(d) Haki za watu hazitakuwa na maana yoyote.

7

45(1)(c)

Kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi hayo kuitumia kama eneo la kuishi na kupata riziki ya chakula.

Kutengenezwa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi hayo kuitumia kama eneo la kuishi na kupata riziki ya chakula wakiwemo walemavu

Maana kamili ya neno kamili maana limetumika kama msamiati na walemavu watapata nafasi ya umiliki halali

 

E: MAMBO MAKUBWA MAPYA YANAYOPENDEKEZWA KUINGIZWA KATIKA RASIMU YA KATIBA

NA.

MAPENDEKEZO

YAENDE SURA YA

IBARA

KAMA KUNA PENDEKEZO LA NYONGEZA SURA/IBARA /KIFUNGU MPYA

 

 

Kuwepo na mbunge wakuchaguliwa na walemavu wenyewe

6

105 (C)

 

 

 

Raisi apunguziwe madaraka

7

69(a)-(f)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

F: MAMBO MAKUBWA YALIYOJITOKEZA KATIKA MAJADILIANO

1. Kukubaliana kuwa na serikali mbili

2.Walemavu wengine kukosa wakalimani wa luga zao

3.Washiriki wengi kutojua kusoma na kuandika

 

 

 

 

 

Sahihi na Mhuri wa Asasi :______________________________

                                JINA :HASSANI NDONDI

Tarehe 28-30/08/2012