Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Tawa kwa kushirikiana na TGNP na Inernational Human Rights Watch leo tarehe 24 julai tumeanza kutekeleza lengo letu la kufanya utafiti katika makundi ya wanawake yaliyoko pembezoni yaani wanawake wanaofanya biashara ya ngono (  commercial sex workers CSW),wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (women who have sex with women WSW),na wanawake wenye jinsia mbili (Intersex),ambapo tumeweza kuwafikia walengwa wapatao 20.(Intersex 3, CSW 12,WSW 5).Kwa mwanzo huu tumepata mwitikio mkubwa ambao umeweza kuibua masuala mbali mbali yanayowakabili wanawake hawa katika jamii wanayoishi. Utafiti huu umeanzia Dar es salaam ambapo tumewashirikisha walengwa kutoka katika wilaya zote tatu ,Temeke, Kinondoni na Ilala.Tunategemea kuendelea na zoezi hili wiki ijayo na mwisho wa zoezi hili tutatoa taarifa kamili ya utafiti wetu.

24 Julai, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (2)

Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) alisema:
Wanawake tushikamane tusibaguane kutokana na kazi zetu au ujinsi wetu(sexual orientation and identities)
24 Julai, 2012
(Afahamiki) alisema:
good job.......big up!
26 Julai, 2012

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.