Fungua
Tanzania Women of Action(Tawa)

Tanzania Women of Action(Tawa)

Dar es salaam, Tanzania

IDARA YA HALI YA HEWA YATAHADHALISHA WAKAZI WA MABONDENI

Wakati matatizo ya awali yaliyowapata wananchi waishio mabondeni kutokana na mafuriko hayajapatiwa ufumbuzi , hasa wakazi wa Keko mwanga  Magulumbasi A na B ,Mission kizinga msikitini ,Tabata Kisukuru na wengineo ,tahadhali imetoka katika idara ya hali ya hewa kwamba kutakuwepo na madhala makubwa kutokana na mvua za vuli zitakazonyesha kwa muda mfupi.Hii ni pamoja na kuwepo kwa  magonjwa ya mlipuko kama maralia, kipindupindu na magonwa mengineyo,hivyo tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili familia hizo ziweze kunusurika na janga lililoko mbele yetu.

6 Machi, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (3)

Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) alisema:
Tunasikitika kuona familia hizo ambazo serikali haijazishugulikia wakati wenzao waliopata tatizo kama la kwao wakiwa Mabwepande ,bado wanategemea kupatwa na maafa zaidi ya yale ya mwanzo.Hivyo asasi za kitaifa na kimataifa tunawaomba waingilie kati suala hili watu hawa wanusurike.
6 Machi, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) alisema:
Ni bora kuziba ufa kuliko kujenga ukuta ,kwa hali yoyote familia hizo zipate wanaharakati watakao jitolea kupaza sauti ili kupatikane ufumbuzi wa haraka na wakudumu ili tusiwe kila siku tunarudia suala hilo hilo .
6 Machi, 2012
Tanzania Women of Action(Tawa) (Hananasifu Kinondoni) alisema:
Katika janga hili tunajua kabisa waathirika wakubwa ni wanawake ,watoto , wazee pamoja .na walemavu.
6 Machi, 2012

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.