Tunaishukuru serikali na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja wameweza kufanikisha zoezi la ujenzi wa maema ya familia takribani 289 katika eneo la Mabwepande lilotengwa kwa ajili ya wahanga wa mafuriko na kugawa viwanja kwa familia zilizokuwa hazijapatiwa ,hii imekamilishwa tarehe 6 februari 2012 . Vile vile kukamilisha ujenzi wa ghala la kuhifadhia chakula na misaada pia ujenzi wa shule kuendelea kwa kasi.
Wakati zoezi hili likiendeshwa kwa ufanisi ,bado tumeshuhudia familia nyingine zilizopata matatizo sawa na zile zilizopo Mabwepande ziikitelekezwa katika maeneo yake ya athari. Hii ni kutokana na kasumba iliyojengeka kuwa wilaya ya Kinondoni ni ya watu wa hali ya juu kuliko wilaya zingine ikifuatiwa na Ilala. Wilaya ya Temeke ikiwa ni ya mwisho katika mkoa wa Dar es salaam.Dhana hiyo imesababishia wahanga wa Keko, Mission Mbagala ambao ni wakazi wa wilaya ya Temeke kutofikiwa na vyombo vya habari ,hivyo kusahaulika katika zoezi hili ,na kubakia wakiendelea kuteseka katika maeneo yao. Kutokana na tatizo hili tunaomba serikali na wadau mbalimbali , mashirika ya kimataifa ,watu binafsi, makampuni na wasamalia wema kuingilia kati suala hili ili kunusuru maisha ya wananchi hao.
Maoni (2)