-kuhuwisha takwimu za awali za watoto walio katika mazingira hatarishi
-kufanya usajili wa familia zinazolea watoto wenye uhitaji
-kutambulisha mradi wa pamoja tuwalee kutoka jali watoto
c)posho ya kujikimu wakati tunapokuwa field haitoshi
-usafiri haukidhi viwango kulingana na eneo husika la mradi
d)posho iongezwe kwa kufuata uahalisia wa eneo husika
-usafiri uboreshwe ili kuepuka usumbufu unasababisha kuchelewa kumaliza shughuli (kazi) kutokana na matatizo ya gari kama kuharibika tukiwa safarini kuelekea au wakati wa kurudi kutoka katika eneo la mradi
e)kutokana na kukutana na watu tofauti tofauti wenye mila na desturi tofauti nimeweza kujifunza namna ya kuishi au kufanya kazi na jamii moja au nyingine kwa kuendana na mazingira yao, mila na desturi zao. hii itanipa urahisi wa kufanya kazi zangu kwa kubadilika kulingana na eneo husika
f)posho
-usafiri
g)kwa upande wa posho tungependa iongezwe kwa kuangalia geografia ya wilaya yetu na ugumu wa kufikika..posho iliyopo sasa inatufanya tushindwe kufanya kazi vizuri kutokana na umbali wa maeneo yetu ya kazi, hivyo wakati mwingine tunalazimika kutumia siku nyingi katika eneo la mradi na kujikuta tunaishiwa fedha za kujikimu kabla ya kumaliza kazi (shughuli)
-usafiri-tungependa kuboreshewa chombo cha usafiri au kubadilishiwa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kama gari kuharibika katikati ya safari, hii inachelewesha muda na pia kushindwa kumaliza kazi mapema kwa sababu zinazoweza kushughulikiwa.
h)kulingana na ukubwa wa shughuli ya kuhuwisha takwimu, usajili na utambulisho wa mradi wa pamoja tuwalee katika wilaya ya sikonge na kata zake, tumefanikiwa kutekeleza shughuli zote kana ilivyoainishwa pasipo kikwazo kikubwa chenye madhara kuacha matatizo madogo madogo yanayoweza kushughulikiwa.
katika shughuli zote zilizopangwa kutekelezwa kwa kipindi hiki hakukuwa na ugumu uliojitokeza ambao ungeweza kuleta kukwazo kwa namna moja au nyingine jambo hili ni la kuleta faraja kwangu mimi katika utendaji wangu wa kazi za kila siku, kwa shirika, lakini pia kwa uongozi wa vijiji tulivyovitembelea na kamati za watoto walio katika mazingira hatarishi.
Aidha kwa kuonesha kuwa wapo mstari wa mbele katika kupiga vita umasikini kwa kukubali kwamba watoto wote ni wetu hivyo kwa pamoja tuwalee viongozi wa vijiji ameahidi kuwa pamoja na TYNF katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi wa Pamoja atauwalee wakiwa kama wadau ngazi za jamii.
Jambo hili ni ishara ya kwamba jamii sasa imeelewa kwamba mtoto ni wa kila mwanajamii na kwamba wanapaswa kusimamia haki za mtoto ikiwa ni pamoja na kumlinda. Haya ni mafanikio na dalili njema katiak juhudi za kutimiza malengo yetu ya kuona yale makundi yaliyosahaulika haswa watoto walio katika mazingira hatarishi wanapata elimu na wanakuwa na maisha bora.
-