Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

VIJANA (MDAHALO WA VIJANA)WATOA MAPENDEKEZO YA KUBORESHA SHUGHULI ZA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE.

Vijana kutoka wastani wa kata 10 walikutana katika kikao cha vijana katika ofisi ya Mtandao wa vijana manispaa ya Temeke kujadili namna ya kuendeleza shughuli ya mijadala ya vijana ambayo hufanywa 2 kila mwezi ili vijana kubadilishana uzoefu na ujuzi juu ya masuala yanayohusu vijana.

Katika kikao tarehe hicho cha tarehe 21/7/2012 vijana walitoa mapendekezo juu ya namna ambavyo  changamoto na zinazokabili vituo zinavyodhoofisha utendaji wa kila siku wa vituo vya vijana.

1. Ukosefu wa uelewa kwa viongozi waliochaguliwa ngazi ya kata juu ya stadi za uongozi na kuhusu mwelekeo wa utendaji kazi wa mtandao wenyewe.Jambo hili limeonekana kudhoofisha kata zote.

2.Ukosefu wa ofisi kwa vijana ngazi ya kata hali inayowafanya kukaa kwenye baa na ofisi za CCM jambo linalowanyima fulsa ya ushiriki vijana wa vyama vingine.Mfano kat ya Buza

3.Viongozi wa juu wa mtandao kuto tembelea vituo imeonekana pia kuwa moja ya changamoto hizo.

4.Vituo vya kata kutokuwa na tija kwa vijana kwa kuwa kila wanapokuja hakuna kitu kinachoshikika.

Mapendekezo juu ya nini kifanyike.

  • Kutolewa kwa mafunzo kwa viongozi na wanachama wa vituo vya kata.mfano mafunzo ya ujasiriamali na stadi za maisha ambapo mkazo zaidi uwepo kwa vijana kujifunza kazi za mikono,ubunifu na ujuzi wa kazi za kuingiza kopato kwa vijana.
  • Stadi za uongozi na wajibu wa viongozi katika kusimamia vituo.
  • Mafunzo juu ya dira.madhumuni na na shughuli za TEYODEN ili kuwezesha viongozi na wanachama wa vituo kujua shughuli za mtandao kwa undani
  • Kuboresha mfumo wa mawasiliano kwa kutuma msg na kupiga simu kwa viongozi na wanachama wa vituo ili kuwapa taarifa kwa kila shughuli inayoendelea katika Mtandao.
  • Kuanzisha group ya mtandao kwenye face book ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa vijan a wanaoweza kupata taarifa hizi kwa haraka kupitia mtandao.

Programu ambazo zinatarajiwa kufanyiwa kazi kwa kipindi kijacho.

Uendeshaji wa mafunzo kwa vijana hasa katika maeneo ambayo wameyapendekeza lakini pia kwe ye eneo zima la utendaji na uboreshaji wa kituo cha vijana  ngazi ya kata.

Utoaji wa taarifa za kazi kwa kila mwezi ili kusaidia kubuni mipango na miradi ya TEYODEN kwa kipindi kijacho.

Vijana wawakilishi wa vijana kutoka kata za Manispaa ya Temeke wakiwa katika mjadala wa pamoja katika ofisi za TEYODEN.

Vijana wakifuatilia kwa makini maelezo ya mratibu wa mdahalo wakati wa kikao cha vijana cha kituo cha vijana ofisi ya makao makuu ya TEYODEN.

21 Julai, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

Maulid Issa Mziwanda (Azimio) alisema:
Muda mwingine Mtandao wa vijana Temeke unafanya kazi kwa mazoea bila kuangalia mahitaji ya vijana wa Temeke kiujumla. Mtandao ni baba na mama mzazi wa vituo 30 vya vijana Manispaa ya Temeke inabidi iangalie mazingira ya ufanyaji wa shughuri zao. Ingekuwa vituo vijitegemee ya nini kipindi cha uchaguzi wagombeea wapigane vibega kwenye kutafuta kura? si wagombea wangeacha mpaka siku ya uchaguzi ili vijana waamue hatma yao? Vituo vya vijana vimedolola kabisa hii ni kwa Teyoden kupoteza mvuto, hebu vuta taswira miaka kazaa iliyopita jinsi gani mtandao ulivokuwa na mvuto wa kipekee vijana mbalimbali wanajumuika katika centre na kuafanya mijadara mbalimbali. Hebu jiulize kwenye kata 30 ziulidhulie kata 10.. Kuonyesha kama Teyoden inafanya kazi kwa mazoea kulikuwa na mipango ya kuzindua centre zenye maeneo 3 {1} CHANG'OMBE {2} TOANGOMA {3} KIGAMBONI, sielewi mipango hii imekufa vipi. hiki ni kipindi cha kufanya kazi za kweli kama hayo mafunzo wapewe ili siku wasiwe na la kusema, kama ushirikiano basi wapeni ili yasiwe midomoni. Namaliza kwa kusema mabadiliko ya ukweli hayaendi kimyakimya bali yanaenda kwa kutoa mapungufu yanayotokea' Tcha
25 Julai, 2012

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.