PROGRAMU YA YOUTH INFORMATION CENTRE YAJA TANZANIA,DAR-ES-SALAAM IKIWA SEHEMU YA MAJARIBIO.
Wizara ya habari,utamaduni,vijana na michezo imepokea na kukubali mpango wa taarifa na habari kwa vijana utakaojulikana kama Youth information Centre.Mpango huu uliasisiwa ama kupendekezwa na bi Joyce Shahidi mkurugenzi msaafu wa Idara ya vijana ya wizara hiyo kwa alipokuwa kwenye kikao cha wadau nchini kenya miaka kama miwili iliyopita.
Programu hii inalengo la kurahisisha upatikanaji wa habari zitakazohusu nyanja mbalimbali za ustawi wa vijana hasa ukizingatiwa kuwa vijana ndio wahanga wakubwa wa changamoto nyingi za maisha.Hivyo kituo cha habari cha vijana kitakuwa kinajibu maswali ya vijana katika changamoto mbalimbali watakazo kuwa wanakabiliana nazo.
Kituo katika hatua za awali kitakuwa ni cha mfano kwa kuanzia katika wilaya za Temeke,Ilala na Kinondoni na kutakuwa na kituo cha taifa cha habari kwa vijana vyote vitakuwa chini ya wizara na Manispaa husika.
Wizara imeunda timu ya watu 7 kushughulikia mchakato wa uundwaji wa kituo hicho na kwa pamoja na wadau walihojiwa imeundwa timu ya watu 14 itakayotoa maoni juu ya namna gani kituo hicho kitakavyochukua sura ya vijana wa kitanzania.
TEYODEN imetoa uwakilishi wa vijana wawili katika timu hiyo ya mchakato wa maoni na kuchagiza uundwaji wa kituo hicho.
Vijana tuamke na kufuatilia juu ya fulsa hii muhimu kwetu.
Wadau 12 wa timu ya Uundwaji wa kituo cha Habari cha vijana wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika Hotel ya Peacock tarehe 12/7/2012.
Wadau wa timu ya Uundwaji wa kituo cha Habari cha vijana wakiwa katika mjadala wa pamoja wa namna ya kuanzisha kituo cha habari cha vijana katika Hotel ya Peacock tarehe 13/7/2012.
Comments (2)