Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MRADI WA MABINTI WALIOPEMBEZONI WATEMBELEWA NA MGENI KUTOKA MADAGASKA.

Mgeni wa kutoka Nchini Madagaska, Bi. Marium Toure ambaye ni Ofisa kutoka UNICEF Madagaska ametembelea mabinti ambao ni walengwa wa mradi wa kujenga uwezo wa mabinti waliozaa katika umri mdogo  na kutulekezwa na wenzi/familia  zao.

Mradi huu unatekelezwa  katika kata 4 za Manispaa ye Temeke, kwa ushirikiano kati ya TEYODEN watekelezaji,TAMASHA wasimamizi na POPULATION COUNCIL wafadhili.Lengo hasa ni kuwezesha wasichana hawa kupunguza changamoto za maisha walizonazo na kuwaepusha na maambukizi ya V.V.U imeelezwa sana katika taharifa,magazeti na tafiti kwamba wasichana hawa wapo katika hatari ya kupata mimba nyingine na hata maambuziki ya ukimwi kwa kuwa katika mazingira hatarishi.

Katika mazungumzo ya kubadilishana mawazo na wasichana mgeni huyu ambae aliambatana na Richard Mabala ambae ni mkurugenzi wa TAMASHA aliwataka wasichana kutohuzunika kwa kuwa wapo katika maisha yenye changamoto nyingi.

"kuzaa sio kosa,ila tatizo ni umri wenu kuwa mdogo pamoja na hayo mlipaswa kuwa katika uangalizi wa familia na waliowapa  mimba"alisema Bi. Marium.

Kwa mujibu wa Bi. Marium alieleza kuwa wasichana wa nchini ,Madagaska hawana programu kama hii zaidi ya progammu za kusaidia vijana hasa eneo la stadi za maisha na stadi za ujasiriamali.

Tatizo la wanajamii hasa vijana wa Madagaska ni kudai pesa kwa kila shughuli inayofanyika hata kama ina lengo la kuwasaidia wao wenyewe dhana ambayo anaishangaa sana kutoikuta kwa vijana wa Tanzania.

Marium alipongeza sana juhudi za TEYODEN na kusema kuwa wasichana wanatakiwa kutokata tamaa na kujichanganya kufanya hata kazi za kiume kama kuendesha bodaboda,kuosha magari na kazi nyingine ambazo zitawafanya kujipatia kipato na kupunguza umasikini.

Mwisho alimpongeza Bw. Mabara kwa kazi zake nzuri ambazo pia zimewasaidia vijana wa Madagaska.

 

June 5, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.