Log in
SHANGWE COUNSELING CENTRE

SHANGWE COUNSELING CENTRE

Mbeya Mjini, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

FCS Narrative Report

Introduction

SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Imarisha Utawala bora kwa wanawake Vijijini
FCS/MG/2/10/099
Dates: March 2012 - May 2012Quarter(s): 4
Samuel Philimon Ngwipa

Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu unalenga katika kuimarisha utawala bora kwa njia ya kutoa elimu ya haki za wanawake ambao ndio walengwa hasa wa mradi ikiwemo kuwashirikisha katika mipango mbalimbali ya maendeleo ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali za jamii zinazotolewa na serikali na wadau wengine waliokatika mapambano ya kupambana na umaskini katika jamii.


RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MbeyaRungweBujela, Bulyaga,Lufingo, Mpuguso, Kisondela, KyimoSimike, Kalalo, Kagwina,Itete,Lugombo,Ipongola,Igalabwe, Bulyaga juu, Igamba, Bulyaga kati,Mtindo,Bugoba,Lutete,Kisuba,Ndubi,Kibatata,Nampuga,Ilenge,Isyukula,Kibisi,Kyimo, Katabe,Mibula,Ipumbuli,Isaji,Bujela,Isongola,Ipombo,Kyamandege,Segela50
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female39(No Response)
Male11(No Response)
Total50(No Response)

Project Outputs and Activities

Mkutano wa pamoja wa tathmini kwa kushirikiana na wadau wengine umefanyika. Mtathimini kutoka nje ameweza kufanya tathmini kwa mradi husika.
Kufanya mkutano na wadau wengine wa Shangwe kwa ajili ya kutathmini shughuli za mradi zilizofanyika, wadau kama mashirika yasiyo ya kiserikali, jamii, walengwa na uongozi kutoka Wilayani walihudhulia mkutano huu.
- Kufanya tathmini kwa kupitia mtathmini wa nje ambaye ni Planet Vision
Mafanikio katika kipindi hiki ni kwamba jamii imeweza kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wanawake kabla ya kuyafikisha katika vyombo vya sheria na hivyo kuongezeka kwa amani na utulivu katika jamii,mfano katika kata ya Kisondela na Lufingo kesi 6 za wanawake walionyang`anywa mali zimeweza kutatuliwa na wao wenyewe baada ya kupata mafunzo
Hakuna
Kufanya Tathmini ya pamoja na wadau wengine - 5, 400,000/=

Kufanya tathmini na Mtathmini toka nje- 700,000

Project Outcomes and Impact

Kuongezeka kwa vikundi vya maendeleo vya wanawake toka 3 hadi 6 katika kata 3 za kisondela, Lufingo na Bulyaga na hivyo kupunguza umaskini kwa wanawake, Pia hali ya jamii kuweza kusimamia haki za wanawake bila gharama yoyote
Jamii kuweza kusimamia kesi zinazohusu haki za wanawake na kuweza kurahisisha na kupunguza gharama kama ilivyokuwa awali kwani ingemlazimu mlalamikaji kufuatilia hatua za kisheria ambazo zingeweza kumpa gharama yeye pamoja na asasi
Viongozi wa Vijiji kusimamia kwa umakini haki za wanawake na kuziweka kama agenda ya kudumu.
Hakuna

Lessons Learned

Explanation
Jamii inauwezo mkubwa wa kutatua matatizo ya wanawake na hivyo kumaliza changamoto nyingi zinazowakabili wanawa ke vijijini hasa wajane.
Viongozi wa Vijiji na kata na kata wanawajibu mkubwa wa kusimamia haki za wanawake na kuweza kutatua matatizo yao
Wanawake waliokatika vikundi mbalimbali vya maendeleo wameonyesha mfano mzuri katika jamii kuliko wasio katika vikundi kwani wamepeleka watoto wao shule kupitia mikopo midogomidogo wanayopata yenye riba nafuu
Wanaume wakizidi kuelimishwa kuhusu haki za binadamu na wanawake tatizo la unyanyasaji wa mwanamke litakuwa histioria.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Changamoto iliyopo ni kwa namna gani tunaweza kuzifikia kata zote za Wilaya ya Rungwe kwani kata za jirani ambazo ni karibu na kata tunazohudumia zimetoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya kwamba nao pia wanahitaji mafunzo hayoTuliweza kuwaomba wale wakufunzi waweze kuelimisha japo kwa kiwango kidogo mpaka tutakapofanya mawasiliano na mfadhili wa mradi huu ambaye ni FCS

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Planet VisionKufanya tathmini ya mradi
Kihumbe OrganizationKushiriki katika mkutano wa pamoja wa tathmini
Viongozi wa kata na VijijiKushiriki katika mkutano wa pamoja wa tathmini

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Hakuna kwani Mradi umekamilika

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale1(No Response)
Male3(No Response)
Total4(No Response)
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale39(No Response)
Male11(No Response)
Total50(No Response)
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Hakuna kwa kota hii

Attachments

FCS Narrative Report

Introduction

SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Kuimarisha Utawala bora kwa wanawake Vijijini.
FCS/MG/2/10/099
Dates: 1Sept, 2011- 31Nov, 2011Quarter(s): 3
Samuel Philimon Ngwipa ( Meneja Mradi).
P.o. Box 3101
Mbeya

Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu unalenga utoaji elimu wa haki za wanawake ambao ndio walengwa hasa wa mradi ikiwemo kuwashirikisha katika mipango mbalimbali ya maendeleo
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MbeyaRungweMpuguso,Kyimo,Bujela,Bulyaga,Kisondela na LufingoSimike,Kalalo,Itete,Iponjola, Lugombo, Kagwina, Bulyaga kati,Bugoba,Mtindo,Lutete, Kisuba,Ndubi,Mpombo,Katabe, Mibula,Bujela,Isaji,Ipumbuli,Isongola.60
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female4511
Male159
Total6020

Project Outputs and Activities

Kufanyika kwa mkutano wa utetezi na uhamasishaji kwa wanawake 45 na wanaume 15 katika kata za Lufingo,Kyimo,Bujela,Kisondela,Mpuguso na Bulyaga
1.Mkutano wa uhamasishaji na utetezi juu ya haki za wanawake kwa wanawake na wanaume katika kata sita za Rungwe.
Mkutano wa utetezi na uhamasishaji juu ya haki za wanawake umeweza kufanyika tarehe 3Sept,2011.Jumla ya walengwa 60 wanawake 45 na wanaume 15 walishiriki katika mkutano huo. Masuala ya mila na desturi zinazowakandamiza wanawake yaliweza kushughulikiwa kwa kina mfano mgawanyo wa mali kwa mama Suzana wa Bulyaga ambaye kwa muda mrefu alikuwa akifuatilia sehemu yake ya urithi na hakuweza kupata uvumbuzi, katika mkutano huu alitoa hoja yake , kwakuwa Mkuu wa mila na desturi alihudhulia mkutano huu aliahidi kulishughulikia suala hili na kulipatia majibu
Hakuna Tofauti Yoyote.
Mkutano wa uhamasishaji juu ya haki za wanawake- 3,548,500/

Project Outcomes and Impact

Kiwango cha jamii kutambua haki za wanawake na kuheshimu mawazo ya mwanamke kuongezeka mfano katika kata ya Lufingo wanawake walipendekeza kuanzisha mradi wa ng,ombe wa maziwa kwa kusaidiwa na ofisi ya mifugo wilaya na mradi wa uanzishwaji wa mashamba ya chai, mawazo yao yalikubaliwa na viongozi wa vijiji na wilaya , na yanashughulikiwa ili kuanzisha miradi hiyo.
Vikundi vya maendeleo ya wanawake vimeweza kuanzishwa mfano kata ya Kisondela wanawake wameanzisha vikundi vya maendeleo (vicoba) kwa ajili ya kukabiliana na hali ngumu ya uchumi na kusaidiana wakati wa matatizo.
Wanawake wengi wamejitokeza katka kujiunga kwenye vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na maendeleo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.
Hakuna

Lessons Learned

Explanation
Shughuli za utetezi na uhamasishaji ni shughuli muhimu sana katika kutatua matatizo ya wanawake vijijini kwani bila kufanyiwa utetezi sauti zao hazisikilizwi na viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na watunga sera mfano katika shughuli za utetezi tuliyoifanya kulikuwepo na watu maarufu ambao ni rahisi kusikilizwa katika jamii, hivyo watu hao waliweza kuona umuhimu wa mwanamke na kuhamasisha jamii kuheshimu utu wa mwanamke, hivyo wanawake kupata nafuu mbalimbali za kimaisha.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Kuhamahama kwa viongozi wa serikali za vijiji wanaoujua mradi na ambao walishiriki kikamilifu katika mafunzo ya haki za wanawake na kuja wapya ambao inabidi tuanzenao mwanzo kuwaelekeza yale tunayoyafanya na pale tulipofikia Kuwapatia muhtsari na ripoti mbalimbali inayohusu mradi unaoendelea ili waufahamu vema na kuendelea kutoa ushirikiano

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Vituo vya sheria za haki za wanawake na watotoKutoa rufaa ya walengwa wanaohitaji msaada wa kisheria
Idara ya ustawi wa jamiiKutoa rufaa kwa ajili ya wanawake wanaohitaji misaada ya kijamii katika ngazi ya familia.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kufanya tathmini na warsha itakayojumuisha wadau mbalimbali katika kutathmini mradi uliofanyikaXXX

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale3(No Response)
Male1(No Response)
Total4(No Response)
ElderlyFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale2(No Response)
Male2(No Response)
Total4(No Response)
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale4011
Male129
Total5220
Hawa ni wawakilishi wa wanawake na wanaume waliohudhulia mkutano wa utetezi na uhamasishaji

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Usimamizi wa ruzukuOctober ,2011Namna ya kubadilishana uzoefu wa masuala ya Usimamizi wa fedha.Mkutano wa pamoja na kamati tendaji pamoja na watendaji ili kutoa mrejesho wa maagizo na mafunzo yaliyotolewa.

Attachments

FCS Narrative Report

Introduction

SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Kuimarisha utawala bora kwa wanawake vijijini
FCS/MG/2/10/099
Dates: Tarehe; June 1,2011-31 Aug,2011 kipindi cha robo mwaka 2Quarter(s): Robo mwaka 2
Samuel Philimon Ngwipa (Meneja Mradi)
P.O.BOX 3101
Mbeya
















































Samuel Philimon Ngwipa
P.O.BOX 3101
Mbeya
Tel:0764047358



Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu inalenga utoaji elimu juu ya haki za kiraia hasa wanawake ambao ndio walengwa hasa wa mradi,uwajibikaji wa viongozi wa vjiji ,kata na wilaya ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wanawake katika mipango mbalimbali ya maendeleo
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MbeyaRungweKisondela,Mpuguso,Kyimo,Lufingo na BujelaSimike,Kalalo,Kagwina,Itete,Lugombo,Ipongola,Igalabwe,Bulyaga juu,Igamba,Bulyaga kati,Mtindo,Bugoba,Lutete,Kisuba,Ndubi,Kibatata,Nampuga,Ilenge,Isyukula,Kibisi,Kyimo,Katabe,Mibula,Ipummbuli,Isaji,Bujela,Isongola,Ipombo,Kyamandege,Segela60
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female1631
Male449
Total6040

Project Outputs and Activities

Mkutano juu ya utetezi wa haki za wanawake kwa viongozi 60 wa kata na vijiji umefanyika.

Kuendesha mkutano wa utetezi juu ya haki za wanawake kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata.













































































Kuendesha mkutano juu ya utetezi wa haki za wanawake kwa viongozi wa vijiji na kata

Kufanya zoezi la ufuatiliaji

Mafanikio tuliyoyapata katika kipindi hiki ni wanawake kupewa nafasi ya kusikilizwa mawazo na matatizo yao, na hivyo masuala ya wanawake kuendeshwa kiufanisi hadi kufikia suluhisho lenye kujenga.
Hakuna tofauti
Kuendesha mkutano na viongozi wa kata na vijiji- 1,251,000/=

Ufuatiliaji - 3,132,000/=

Project Outcomes and Impact

Wanawake wameweza kupata uwakilishi katika ngazi mbalimbali ya vyama vya maendeleo na uzalishaji kwenye vijiji mfano mwanamke mmoja ameweza kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa wakulima wa chai katika kata ya Lufingo ambapo kwa miaka mingi walikuwa ni wanaume tu. Vilevile kuna wajumbe 3 wanawake kwenye chama hicho chenye wanachama 20.
Viongozi wa vijiji/kata wamekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia masuala ya wanawake hasa baada ya kufanya mkutano na kutambua kwa dhati haki za wanawake kuliko hapo mwanzo ambapo nao walishiriki katika kumkandamiza mwanamke kwa kutosikiliza malalamiko yao na hivyo kuwafanya wanwake kukata tamaa na kubaki na shida zao huku wakiteseka.
Badiliko jingine kubwa ni wanawake kuwa na umoja katika kudai haki zao na kutokuwa na woga kwani vikundi mbalimbali vya kiuchumi vimeanzishwa kwa lengo la kumkwamua mwanamke kiuchumi na kusaidiana hasa pale ambapo kuna aina yoyote ya ukandamizaji juu ya wanawake katika maeneo yao.
Hakuna.

Lessons Learned

Explanation
Mambo muhimu tuliyojifunza ni kwamba viongozi wa vijiji hawana miongozo iliyowazi katika kuongoza makundi yao na inaonyesha madaraka waliyopewa ni nusunusu kwani wengi wao wamekiri kwamba wanashindwa hata kutatua migogoro mbalimbali ya vijiji ikiwemo matatizo ya wanawake na hivyo kutumia miongozo ya kimila na desturi ambazo zina mapungufu katika kutatua matatizo na hivyo kuendelea kumkandamiza mwanamke.
Jambo la pili tulilojifunza ni matarajio ya unafuu kwa mwanamke katika Wilaya ya Rungwe, Viongozi wa vijiji na kata ndio wenye dhamana kubwa katika kutatua migogoro ya wanawake, lakini dhamana hiyo haikutumika vema hapo awali, baada ya viongozi hawa kupata mafunzo wamekiri kwamba kutokana na uelewa mdogo katika kutatua shida za wanawake na kutokujua sheria, hali ya wanawake ilikuwa mbaya sana kwani mashtaka yote yaliyopelekwa kwao yaliishia kuendelea kumkandamiza mwanamke.
Wazo jingine tulilolipata ni juu ya kuendelea kuwapatia mafunzo ya utawala bora viongozi wa vijiji na kata kwani wengi wao wamekiri kubeba majukumu wasiyoyajua mfano kiongozi mmoja wa kijiji cha itete alikiri kwamba hajawahi hata kuona katiba ya nchi na wala hajui kama kunakitu kinaitwa utawala bora, kwake ni mara ya kwanza kusikia kwenye mafunzo haya. Viongozi hawa wa vijiji ni wengi na ndio waliokaribu zaidi na wananchi, hivyo wanatakiwa kujengewa uwezo zaidi juu ya masuala ya uongozi , utawala na utawala bora.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Changamoto ambayo bado tunapambana nayo ni kuhusu mifumo ya kiutawala vijijini, bado hawaamini kama mwanamke anaweza kuwaongoza mfano kwenye mkutano uliofanyika idadi ya wanaume viongozi waliohudhulia walikuwa wengi kuliko viongozi wanawake.Hii inaonyesha kuwa viongozi wanawake bado hawajapewa nafasi zaidi za kuongoza.Tulichokifanya katika mkutano huo ni kuendelea kufanya utetezi juu ya umuhimu wa mwanamke katika maendeleo, na wao walikiri kwamba wamewanyima wanawake nafasi nyingi za kiutawala kwenye maeneo yao na hivyo kuuhakikishia mkutano kubadili mifumo inayomkandamiza mwanamke
Changamoto nyingine ni kuhusu posho, kwakweli ukiwaita viongozi wa serikali katika mkutano au semina wanataka kupewa kiwango cha serikali ambayo ni 65,000/= kwa siku kwa kweli jambo hili lilileta hadithi nyingi.Tuliendelea kuwaelimisha tofauti zetu na serikali kwa nia njema na kuwaomba waangalie zaidi umuhimu wa mkutano kwa faida ya maendeleo ya vijiji/kata zao
Kuongezeka kwa wanawake wanaohitaji msaada wa kisheria Tumejaribu kufanya rufaa mbalimbali mfano kwenye ofisi za ustawi, mahakama ya mwanzo na wote waliozingatia na kufatilia rufaa hizo wamepata msaada.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya RungweKufungua mafunzo na kutoa kibali kwa watendaji wa kata kuhudhulia mkutano tuliokuwa tumeuandaa na kuendesha.
Asasi zisizo za kiserikali mfano AFNET TanzaniaWameweza kutusaidia kuwaelimisha zaidi viongozi wa kata na vijiji juu ya elimu ya kiraia kwani AFNET wanauzoefu mkubwa juu ya utoaji wa elimu ya kiraia kwa ufadhili toka UNDP.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Mpango uliopo ni kufanya mkutano wa pamoja wa tathmini ambao utajumuisha wadau mbalimbali katika wilaya ya Rungwe ili kutahmini mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza katika mradi na kwamba tufanyeje.XXX
Kutoa ripoti ya utekelezaji kwa wadau mbalimbali wa shangwex

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
Moja kwa moja ke 16, me 44, Wasio wa moja kwa moja ke 51, me 9

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
----
----
----

Attachments

FCS Narrative Report

Introduction

SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Kuimarisha utawala bora kwa wanawake Vijijini.
FCS/MG/2/10/099
Dates: 23March,2011-23May,2011Quarter(s): 1
Samuel Philimon Ngwipa
P.o.Box 3101
Mbeya
Tel: 0764047354

Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu inalenga vipengele muhimu vya utawala bora kama vile utoaji elimu juu ya haki za wanawake katika jamii na uwajibikaji wa viongozi wa ngazi mbalimbali za vijiji na wilaya kwa ujumla katika kuwashirikisha wanawake kwenye masuala ya maendeleo yao.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MbeyaRungweMpuguso, Kisondela,Bulyaga,Bujela,Lufingo,KyimoSimike, Kalalo, Kagwina,Itete,Lugombo,Ipongola,Igalabwe, Bulyaga juu, Igamba, Bulyaga kati,Mtindo,Bugoba,Lutete,Kisuba,Ndubi,Kibatata,Nampuga,Ilenge,Isyukula,Kibisi,Kyimo, Katabe,Mibula,Ipumbuli,Isaji,Bujela,Isongola,Ipombo,Kyamandege,Segela150
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female93682
Male57368
Total1501050

Project Outputs and Activities

Wanawake 93 na wanaume 57 wameweza kupata elimu juu ya utawala bora na haki za wanawake katika nyanja mbalimbali, na baada ya mafunzo hayo wanawake na wanaume hao wameanza kutoa elimu waliyoipata kwa jamii katika maeneo yao vijijini kwa kuzingatia mpango kazi walioupanga baada ya semina.
1. Kuendesha mafunzo juu ya haki za wanawake na utawala bora
2. Waliopata mafunzo yaani wakufunzi kutoa mafunzo katika vikundi mbalimbali vya kijamii
kilichofanyika ni utoaji wa mafunzo juu ya utawala bora na haki za wanawake, ambayao yalitolewa kwa awamu tatu tofauti tarehe 4 April - 8April 2011, 11 April - 15 April 2011, 19 April - 23 April 2011 katika kata sita za wilaya ya Rungwe ambazo ni Mpuguso, Lufingo, Kyimo, Bujela, Bulyaga na Kisondela. Washiriki waliopata mafunzo haya ni wanawake .93 na wanaume 57 amabao waliandaa mpango kazi kwa ajili ya kutekeleza mradi..Baada ya Mafunzo wakufunzi mia moja walipewa vitini ili kuweza kuendesha mafunzo juu ya haki za wanawake katika vijiji vyao.Mafunzo hayo yalianza tarehe 10/5/2011 Masuala yaliyoshughulikiwa ni Wanawake 3 walionyang,anywa Mali baada ya waume zao kufariki Dunia, Msaada wa rufaa ya kwenda kituo cha sheria kwa Mwanamke mmoja toka Lufingo anayepigwa mara kwa mara na mumewe, Wanawake 2 katika kata ya Mpuguso waliobakwa na kushindwa kutoa taarifa popote kwa kuogopa kutengwa na wanajamii.Maelezo ya wanawake hao ya awali yamechukuliwa na kuwasilishwa kwenye kituo cha msaada wa kisheria Mbeya Mjini.
Hakuna Tofauti
mafunzo zilitumika 16,200,000/=
Wakufunzi kuendesha mafunzo katika vijiji vyao 3,600,000/=
Uandaaji wa vitini 750,000/=
Uandaaji wa washiriki 200,000/=
Manunuzi ya Pikipiki 1,850,000/=

Project Outcomes and Impact

Wanawake walio katika mazingira duni na migogoro mbalimbali wamepata fursa ya kushiriki katika kutoa maamuzi kwa kuzingatia haki zao mfano wanawake 7 katika kata ya Bujela, Kisondela na Lufingo wamejiunga kwenye mabalaza ya ardhi ili kuhakikisha maslahi yao katika ardhi yanaangaliwa ipasavyo.
Wanaume wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kutambua na kuheshimu wanawake na haki zao kwani wao wenyewe wamekuwa hodari katika kuendesha mafunzo vijijini juu ya kuheshimu wanawake na haki zao, wameonyesha dhamira njema katika kutetea haki za wanawake ,badiliko hili si la kawaida kwa wanaume wa kabila la kinyakyusa ambalo kiwango cha mfumo dume ni kikubwa.
Badiliko jingine kubwa ni upande wa wanawake kuonyesha kujitambua wao wenyewe mfano mmoja ni kwa upande wa wanawake 3 wa kata ya Kyimo walioonyesha dhamira kubwa ya kuchukua hatua katika kudai ushiriki wao kwenye mabalaza ya kata na mabalaza ya ardhi, na kupewa nafasi hiyo.
HAKUNA

Lessons Learned

Explanation
Wazo jipya tulilolipata katika kutekeleza mradi huu ni kwamba wanaume wakipata elimu ya kweli na ya kutosha juu ya haki za wanawake wanabadilika na wanapata mwitikio mkubwa pindi wanapoelimisha jamii juu ya haki za wanawake, kwani hata wanaume wenzao huwasikiliza kuliko mwanamke kusikilizwa kutokana na hali ya dharau iliyojengeka katika jamii kwamba mwanamke hapaswi kusikilizwa, kwa hiyo wanapoelimisha jamii juu ya haki za wanawake, kwa mwanamke ni faida kubwa.
Wazo jingine ni kwamba pamoja na harakati nyingi za ukombozi kwa mwanamke zinazoendeshwa na asasi mbalimbali Tanzania, bado hali ya mateso kwa mwanamke wa kijijini ni kubwa, wanawake bado wanabakwa, wanapigwa, wananyimwa nafasi za ushiriki katika mipango ya maendeleo, kiujumla hawasikilizwi, hivyo bado tunakazi kubwa ya kufikia Wilaya yote ya Rungwe hasa tukilenga kuelimisha wanaume na viongozi wa vijiji.
Bado viongozi wengi wa vijiji ni madikteta, wananchi wananyanyaswa na kupewa adhabu na faini zisizo na msingi, mfano washiriki wawili waliochelewa mafunzo tuliyokuwa tukiendesha kwa sababu za kufiwa , Mtendaji aliposikia hawajafika kwenye mafunzo kesho yake walipokuja aliweza kuwapigisha magoti kwa muda mrefu na kuwaamuru warudishe posho walizopewa kwenye mafunzo na faini ya elfu kumi kila mmoja kwa ajili ya mgambo aliyewafuata, kwakweli kama shangwe tulikataa wale akinamama kuturudishia posho, lakini ile faini ya mgambo aliwaamuru watoe, kwa kweli wenzetu vijijini wanateseka na hawa viongozi wa kata na vijiji. Yaani viongozi hao wanaabudiwa ni mungu watu.
Katika kutekeleza miradi mingine inayokuja , kama tutaendelea kuwa pamoja, tumegundua ni vema kutenga fungu la msaada wa kisheria kwa wanawake, kwani tumekutana na kesi nyingi za uonevu na manyanyaso juu ya wanawake zinazohitaji fedha kwa ajili ya msaada wa kisheria lakini tumekwama, japo kesi zingine zilizokuwa ni mbaya sana ilibidi tuchangie kutoka mifukoni mwetu ili kuweza kunusuru hali zilizokuwa zikiendelea.
Jambo jingine muhimu tulilojifunza ni kuhamasisha wanasheria sasa kufungua matawi yao vijijini hasa wanasheria wanawake kwani mateso ya wanawake vijijini ni makubwa sana kuliko mjini ambako wanawake wengi mjini wanatambua haki zao, katika miradi ijayo tumeona vema kutenga fungu kwa ajili ya kuhamasisha wanasheria na watetezi wa haki waliopo mjini wakitafuta ajira wafungue matawi vijijini kazi zipo nyingi.
Wanawake wa vijijini ni waelewa sana na wanakiu ya kujifunza na kutafiti mambo muhimu yanayoendelea katika Nchi yetu.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Changamoto ya kwanza ni kwa ajili ya wanawake 30 waliokuwa wakihitaji msaada wa kisheria, ilikuja kugundulika kwamba ni kweli msaada wa kisheria ni bure kwa wanawake katika vituo kadhaa, lakini kuna mambo mengi yanayohitaji fedha, mfano nauli ya nenda rudi, malazi, chakula nk., mahitaji hayo hayakuwekwa kwenye bajetiTuliweza kuwasaidia wanawake wawili ambao kesi zao zilikuwa mbaya za kubakwa tulichangisha kiasi cha shilingi laki 340,000/=, kwani mmoja wao aliyebakwa alizaa mtoto ambaye pia alikuwa anahitaji huduma za matibabu, mpaka sasa kesi zao zinasimamiwa vema na mwansheria husika, japo mbakaji mmoja amekimbia mji.
Kuchelewa kwa ruzuku kutoka FCS ambapo wanajamii waliona kwamba tunawadanganya na hivyo kutaka kuharibu kusudio zima la mradi.Ruzuku ilifika na tulitekeleza mradi kama inavyotakiwa na hivyo tulimaliza changamoto hiyo na jamii ikafurahi.
Wanawake vijijini kuwa na hofu pindi wanapofanyiwa ukatili hawawezi kusema , wakisema hutengwa hata na wanawake wenzaoMafunzo yaliyoendeshwa yameweza kuwabadilisha na sasa wanaweza hata kujieleza mbele ya jamii.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Vyombo vya habari mfano ITV, NIPASHE NA MWANANCHIVyombo vya habali viliweza kurusha shughuli zetu hewani na kuufanya mradi kutambulika na jamii kubwa
Serikali ya TanzaniaMkuu wa Wilaya ya Rungwe ndiye aliyefungua mafunzo tuliyokuwa tukiendesha. Watendaji wa kata na vijiji waliweza kutoa ushirikiano mzuri katika kuwatambua washiriki waliopata mafunzo
Vituo vya sheriaTumeweza kushirikiana na kituo cha sheria Mbeya hasa katika kutoa rufaa ya kesi zinazohitaji msaada wa kisheria.
Asasi zisizo za kiserikali mfano Planet Vision, Walter reedTumeweza kushirikiana nao katika kuchangia mawazo ya kuboresha shughuli mbalimbali za mradi unaoendelea.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuendesha mkutano na viongozi wa vijiji na kata (60) ili kuhamasisha utetezi juu ya mwanamke hasa katika kuwasikiliza pindi wanapoleta malalamiko yanayohusisha uonevu na ukatili.X
Kufanya mchakato mzima wa ufuatiliajiXXX

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale(No Response)23
Male(No Response)11
Total034
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale93682
Male57368
Total1501050
NIL

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mafunzo ya Usimamizi wa RuzukuDecember 2010Maana ya bajeti na umuhimu wake, uchambuzi wa bajeti, uandishi wa taarifa,Usimamizi wa fedha,Mpango kazi wa mradi, uandaaji wa taarifa za fedha, uandaaji na uhifadhi wa vitabu vya fedhaKuboresha taarifa za fedha na taarifa za shughuri za mradi.
Tamasha la asasi za kiraia2007Kuheshimiwa kwa matakwa na sauti za wananchi ili kuepusha kuvunjika kwa jumuiya ya afrika masharikiKuelimisha wafanyakazi wa asasi na jamii juu ya umuhimu wa jumiya ya afrika mashariki

Attachments