Fungua
Save Lives Organization Trust Fund

Save Lives Organization Trust Fund

Manispaa Morogoro, Tanzania

Save lives organization Trust Fund Tanzania ni taasisi isiyo ya kiserikali, kidini wala si ya mtu binafsi. Ni taasisi ya kiraia ambayo ilianzishwa kwa ajili ya jamii nzima.

Kama lilivyo jina lake, taasisi hii ilianzishwa mwaka 2005 na waanzilishi wa taasisi hii ambao ni Mchungaji Jubeck T. Mapassa wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini pamoja na Mama Victoria Mbembela kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania maskini walio wengi.

waanzilishi wa taasisi hii waliona haja ya kuwa na chombo kama hiki ambacho kitahudimia wahitaji wa namna mbalimbali wakiwemo wajane, watoto waishio katika mazingira hatarishi (MVC), yatima, Vijana na wazee.

Kuanzisha kwa taasisi hii ni matokeo ya safari iliyofanywa na waasisi hao wawili wa shirika walipokuwa na ziara ya kutembelea makanisa mbalimbali katika wilaya ya Kilombero kwa shughuli za injili.

Katika safari yao hiyo walikutana na kisa cha mtoto mmoja ambaye alikuwa ni yatima Dada Anthonia Mbangule (Ambaye kwa sasa ni marehemu "Mungu ailaze Roho yake mahali pema Peponi"). Kisa hicho kilichokuwa kikihusu maisha ya binti huyo kiliwasikitisha sana waanzilishi hao na kupata msukumo wa kuanzisha taasisi hii ilikuwa chombo cha ukombozi wa maisha na mtetezi wa wanyonge.....

Kwa sasa Taasisi ina makao yake makuu katika Manispaa ya Morogoro, Kata ya Kiwanja cha Ndege , Mtaa wa Azimio, Kitalu Na. 1062.

Tunatoa Huduma za Upimaji VVU kwa Hiari, Utetezi wa Kisheria, Missada ya Kibinadamu kwa wahitaji wa namna mbalimbali, Mikopo midogo midogo kwa jasiliamali wadogo pamoja na kuandaa makongamano na warsha mbalimmbali za kiuchumi na kijamii.

Kauli mbiu yetu ni " AMUHURUMIAYE MASKINI HUMKOPESHA MUNGU......" Mithali 19:17

Wote Mnakaribishwa kushirikiana nasi katika kufanya kazi hii ngumu ya mapambano dhidi ya Umaskini, Ujinga na maradhi.

Taasisi yetu haina Ubaguzi wa dini, Kabila, Rangi, Jinsia wala Utaifa.