Napongeza sana juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na jumuia ya kukuza na kuendeleza elimu kisiwani Pemba. Jumuia hii inajaribu kutanuwa wigo kwa kuwahusisha wadau mbalimbali wa elimu katika kisiwa cha Pemba. Aidha wananchi wamefarajika kwa kiasi kikubwa kuona mabadiliko yaliyopatikana toka kuanzishwa kwa jumuia hii.
16 Ugushyingo, 2011
SAID KHAMIS JUMA (CHAKE-CHAKE PEMBA) bavuzeko
Ipo haja ya kujikita zaidi katika alimu ya stadi za maisha kama vile elimu ya ukimwi, mazingira, ujasiriamali, uvuvi nakadhalika.
Kufanya hivyo ni kuwajengea wananchi njia sahihi ya kujikwamua kutokana na umaskini unaoendelea kulitesa taifa letu la Tanzania
16 Ugushyingo, 2011
Ali Shaaban Mtwana (Pemba) bavuzeko
Uendelezaji huu wa elimu unaofanywa na Jumuia ya PEDO katika kisiwa cha Pemba kwa kuwasaidia wanafunzi katika masomo ya ziada ni wa umuhimu sana kulingana na mazingira yalivyo. Nimegundua kwa ufuatiliaji wangu kwamba yanapatikana manufaa makubwa na mabadiliko kwa wanafunzi waliobahatika kusaidiwa masomo kwa muda wa ziada na Jumuia ya Kukuza na Kuendeleza Elimu Pemba (PEDO).
Jamii inaridhia mchakato huu na wanatoa baraka kwa wanajumuia kuendeleza kuwasaidia vijana.
Ibitekerezo (3)