Envaya

large.jpg

KAMALINAVYO JIELEZA BANGOLETU HAPO

large.jpg

PICHA YA WANA-NURUHALISI KABLA YA KUPOKEA KIKOMBE

large.jpg

WADAU WAKIJADILIANA KABLA YA KUPOKEA TUZO

large.jpg

kikombe hiki ni mali ya WANAMAZINGIRA ambacho tulikabidhiwa kwa utendaji mzuri hasa katika nyanja ya usafi.NAMBA MOJA KI-WILAYA YA ILALA KATIKA SWALA LA UTUNZAJI MAZINGIRA NA USIMAMIZI WA USAFI

NURU HARISI WAENDELEA KUTOA ELIMU KWA MAMA NA BABA LISHE

DIRA YETU NI KUWAWEZESHA WAUZA VYAKULA NA MATUNDA WAZINGATIE YAFUATAYO ILI KUEPUKA KUENEA KWA KIPINDUPINDU KWA WATEJA

  • Osha vyombo kwa maji safi na sabuni
  • Kufunika vyombo vyote vizuri na kwa usafi
  • chemsha au tibu maji yote ya kunywa na kutengenezea juisi ya wateja na yafunikwe wakati wote
  • Mpe mteja wako chakula kikiwa cha moto
  • Weka chombo chenye maji na sabuni kwa kunawia mikono kwa wateja wako
  • Nawa mikono kwa maji yanayo tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni na kabla ya kuandaa chakula
  • Tayalisha chakula katika mazingira safi
  • Osha matunda na mbogamboga zisizo chemshwa kwa maji salama

Epuka na pia usichangie kuenea kwa kipindupindu mteja wako akifa kesho utamuuzia nani?

TUNZA AFYA YA MTEJA WAKO.

 

 

Mwezi August na september Nuru Halisi imetoa mafunzo kwa mama na baba lishe katika maeneo ya mazizini-Ukonga, Mafunzo hayo yalihudhuriwa na watu 32 na yalihusisha viongozi wa Kata ya Ukonga kitengo cha afya. Pamoja na kutoa elimu hiyo ya namna ya kutunza vyakula katika hali ya usafi, pia walipatiwa elimu ya namna ya kutunza taka zitokanazo na vyakula katika hali isiyokua na madhara kwa binadamu. Vilevile baada ya kmaliza mafunzo hayo,wameaswa kuwa na umoja wao ili waweze kujikwamua na kukuza biashara zao kwa kushirikiana. Wameona ni vyema wakawa na sare za pamoja.

Katibu wa Nuru Halisi akiwa na viongozi wa kikundi cha Nuru Development Group(KIMANU) katika moja ya vikao vyake. Kikundi hiki tayari kimeanzisha mradi wa uyoga na kinaendelea kuandaa miradi mingine ya maendeleo.

NURU DEVELOPMENT GROUP tayari wameshafanikisha kupanda uyoga, wanakikundi wamepeana majukumu ya kuutunza na viongozi kuendelea kutoa elimu pamoja na kutafuta fursa nyingine, Kikundi bado kinakaribisha wanachama ili kuwa na wigo mkubwa zaidi. Pia tunakaribisha wajasiriamali wadogo wagogo ili tuungane na kupanuka zaidi na hatimaye kuifikia jamii nchi nzima. Wanachama sio lazima watoke Dar es salaam na Dodoma tu, tunakaribisha wanachama toka pande zote za Tanzania bara. Katibu wa Nuru Halisi akizungumza na wana Kikundi katika picha.

large.jpg

Ni usiku,baadhi ya wanachama walikua wakiendelea na zoezi la kuzibua mitaro bila kujali muda