Fungua
Newala Youth Network

Newala Youth Network

Newala, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

Ndugu msomaji, mnamo tarehe 31.11.2011, NEYONE ilipata fursa ya kutembelewa na Balozi wa Norway nchini Tanzania ambaye pamoja na kuonana na vijana wa Newala, alizindua rasmi kituo cha vijana (Newala Youth Resource centre). Kituo hiki kimeanzishwa kwa madhumuni ya kutoa elimu mbalimbali kwa vijana wa Newala hususani katika masuala ya elimu, afya, kilimo ,utawala bora na shughuli mbalimbali za maendeleo na ujasiriamali. Uongozi wa wilaya ya Newala walishiriki kikamilifu wakiongozwa na Mh. Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya.Picha za tukio hili zinafuata.

Ndugu msomaji , tafadhali pitia ukurasa wetu kwenye facebook  (http://www.facebook.com/?ref=home#!/pages/Newala-Youth-Network-NEYONE/106305629402359?v=wall )  na blog yetu  http://newalayouths.blogspot.com/ kwa taarifa zaidi kuhusu kazi zetu.