Log in
MWELA THEATRE GROUP DAR-ES-SALAAM

MWELA THEATRE GROUP DAR-ES-SALAAM

TEMEKE,DSM,Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

KUHUSU MIGOGO MASHIRIKA YA KIRAI TUPO WAPI?

FIKIRI S MVUGARO (DSM)
May 22, 2012 at 7:33 PM EAT

Napata taabu sana kwa kuona mashirika mengi ya Tanzania ukiacha yale yanayotetea haki za wanawake na walemavu ndio wanakuwa kipaumbele linapotokea tatazo ndio ulifatilia lakini baadhi ya mashirika mengi inapotokea matatizo mbalimbali katika jamii uwa hayajitokezi kuzungumzia swala lolote au tunasubiri hadi tuingiziwe Ruzuku ndio tunafanya kazi.

ukiangalia baadhi ya mashirika mengi yamekuwa kama vile baadhi ya vyama vya siasa kipindi cha uchaguzi uwa motomoto kikiisha tu basi.

na ndio sawa na baadhi ya mashirika hapa nchi kipindi cha Ruzuku uwa moto Ruzuku ikimalizika basi hakuna tena utetezi,

ukiangalia sasa migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa ni tatizo kubwa sehemu nyingi za Tanzania kwa mfano morogoro,kisarawe na wiki hii pwani wilaya ya Rufiji

katika hizi wilaya sasa kumekuwa ni tatizo kubwa sana lakini cha kushangaza kuna Asasi nyingi sana katika hizi wilaya na nje ya wilaya lakini wana asasi tumekaa kimya

na wakati mwengine baadhi ya Asasi hizi ukosa ujasili wakukabiliana na baadhi ya viongozi wa kijiji na porisi kipindi cha kukabili matatizo.

sio kwamba nabuni swala ili  nina uhakika kuna baadhi ya mashirika ambayo niliofanya nayo kazi  baadhi ya maeneo yao wanakutaka usizungumze ukwele kwa sababu tu wanamauhusiano nae mazuri huyo kiongozi mbovu ambae hafuati sera,sheria na miongozo iliyowekwa.

hivi hatuoni matatizo haya ya baadhi ya viongozi wabovu wanavyosababisha. na hivi kweli tunawapa miongozo mizuri jamii inapotokea matatizo kama haya.mpaka inafikia jamii moja ina kuishambulia jamii nyingine.

mashirika tupo wapi mpaka athari  zinatokea na kushindwa kutoa mwelekeo kwa jamii

na mashirika tuna tunaifahamu mitandao mbalimbali inayofanya kazi mbalimbali za kuidumia jamii kwa mfano msaada wa kisheria n.k

lakini pia tunaufahamu juu ya kama wananchi maenda kupeleka malalamiko sehemu fulani na hayajasikilizwa basi wachukue hatua ya kwenda wapi na kwa muda gani? lakini hata kama shirika lako halina hufahamu na jambo hilo unaweza kutafuta shirika ambalo linaweza kutoa muongozo wa ilo swala

naileta kwenu wadau na mashirika mbalimbali, kwanini inapotokea migogoro baadhi ya mashirika mengi uwa kimya?


Add New Message

Invite people to participate