Log in
MWELA THEATRE TAWI LA VUGA

MWELA THEATRE TAWI LA VUGA

WILAYA YA LUSHOTO KATA YA VUGA , Tanzania

UTANGULIZI

Mwela theatre group tawi la vuga ni kikundi cha vijana cha kujitolea kilichoanzishwa tarehe 28/1/2010.ni muunganiko wa vijana kutoka katika vijiji vya Kidundai, Kiluwai,Vuga Kishewa na Bazo wakaunda Dira ya pamoja ya kuwa na jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza bila kikomo.

Mwela theatre group ilipata mafunzo ya kujengewa uwezo toka mradi wa uimarishwaji wa asasi mradi uliofadhiliwa na The foundation for civil society na kuendeshwa na Chama cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii vuga (CHAMAKIVU) mradi ambao mwela uliweza kuwapa ujasiri na kuweza kujiimarisha zaidi katika masuala ya utendaji kazi wake katika shirika

 MALENGO YA SHIRIKA

  •  Kuinua vipaji vya vijana na watoto katika sanaa na michezo
  •  Kulinda na kutangaza utamaduni wa mtanzania ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia maadili na sheria za nchi
  • Kutete haki za vijana,wanawake na watoto katika mambo yanayowahusu   Kuwawezesha vijana na wanawake katika masuala ya ujasiliamali
  • Kutoa elimu kwa vijana juu ya kuzuia na kupunguza madhara kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya

MHUTASARI

Muhutasari wa mradi huu ni kuhakisha vijana wazee na wanawake wanashiriki katika kutoa maoni ya Katiba kwa kutumia haki zao za kimsingi za kikatiba ili kuleta mabadiliko yatakayokwenda sanjari na maendeleo kwa kupata mahitaji ya msingi ya vijana,wazee na wanawake.

Mradi uliwafikia watu 110 me 50 na ke 60 toka katika vijiji vya Kiluwai na Kidundai toka kata ya Vuga  wamefahamu faida za kushiriki katika utoaji wa maoni ya Katiba na kuchangia utoaji wa maoni hayo.

Mradi huu umesaidia kutoa dhana potofu kwa vijana,wazee kuwa Katiba ya Nchi imeshatengenezwa.

Shughuli za mradi huu zilikuwa kuendesha mikutano ya siku 3 kwa vijana wazee na wanawake

walitoa maoni yao na walifahamu faida za kutoa maoni kwa njia ya mijadala njia hii ilisaidia vijana,wazee na wanawake kutoa maoni yao na wameonesha maisha halisi ya jamii yetu na mitazamo hasi katika jamii yetu juu ya masuala ya kushiriki katika kutoa maoni ya katiba hivyo njia hii ilisaidia kuibua mijadala na iliwapa fursa kuchangia na kutoa maoni mazuri

 HISTORIA YA MRADI

Vijana wazee,na wanawake wa vijiji vya kiluwai na kidundai ambao walikosa utambuzi juu ya kutoa maoni yao na wengi hawakupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika kuchangia marekebisho ya katiba pya

Tulifanya mahojiano na baadhi ya vijana,wazee na wanawake

35% walikuwa hawafahamu lolote kuhusu masuala ya marekebisho ya katiba na kusema kwambao wao wamesahaulika katika mambo mengi ya maendeleo na kusema kuwa fursa nyingi zinapelekwa vuga bazo

25% walikuwa wanasikia tu kama kunamarekebisho ya katiba lakini walikuwa hawajui kuwa wao wana nafasi gani ya kushiriki na watashiriki vipi katika kutoa maoni ya katiba

20%walikuwa wanafahamu kama kunamarekebisho ya katiba lakini walikuwa hawana rasimu hiyo ya katiba hivyo walikuwa hawaelewi nini wachangie na nini wasichangie

15% walikukuwa hawana taarifa na hawakuhitaji kujisumbua na masuala marekebisho ya katiba kwa sababu waliamini kuwa katiba imeshatengenezwa hivyo ni janja tu ya kuweka mazingira ya kula pesa

Kutokana na hali hiyo vijana,wazee na wanawake hawa dhahili kabisa kulikuwana kunahitajika kuwawezesha kuwa na maeneo na nafasi huru za kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wao katika masuala muhimu ya marekebisho ya katiba .Lakini pia kupata nafasi ya kujadili changamoto za maisha na jinsi ya kukabilina na changamoto hizo.na ufumbuzi na majawabu ya maswali yao ni wao kushiriki katika kutoa maoni ya katiba

 LENGO KUU LA MRADI

Ushiriki mzuri wa vijana,wazee na wanawake katika marekebisho ya katiba

 LENGO MAHUSUSI

Kuongeza ushiriki wa vijana,wazee na wanawake katika marekebisho ya rasimu ya katiba

 MATOKEO YA AWARI

Vijana,wazee na wanawake walifahamu umuhimu wa kutoa maoni ya rasimu ya katiba

Vijana,wazee na wanawake walifahamu rasimu ya katiba na ibara zake

Vijana,wazee na wanawake walifahamu kutoa maoni ni haki yao ya kikatiba

 MATOKEO YA KATI

Vijana,wazee na wanawake walijua jinsi ya kujiunganisha na kujenga timu ya kuingia katika vijiji na kuchukua maoni na kuyatuma tume ya katiba

Waliweza kutoa hoja nzito zenye kujenga ushirikiano wa pamoja na mahitaji yao na kuyapendekeza katika rasimu ya katiba

 WALENGWA

Vijana wa mashule na nje ya shule

Watoto wa mashule na nje ya shule

wanawake

 NJIA TUNAZOTUMIA

Semina

Midahalo

Mikutano na mikutano ya hadhara

Matamasha

Kupitia vijiwe vya vijana

Nyumba hasi nyumba

Kutumia michezo

MAONI SIKU YA KWANZA

 UTANGULIZI

BARAZA LA MAJADILIANO YA RASIMU YA KATIBA MPYA

Mweyekiti wa Asasi ya MWELA Theater Group alifungua mkutano mnamo saa2:30 asubui kwa kuwakaribisha washiriki. Alifanya utambulisho wa wageni akiwemo MUWEZESHAJI, MCHUKUA DONDOO pamoja na washiriki wote wa baraza la majadiliano kutoka asasi ya MWELA ambao ndio walioshughulikia maombi ya Ruzuku kutoka The Foundation for Civil Society na kibali cha majadiliano haya toka Tume ya Katiba hii. Baada ya maelezo haya, alimkaribisha Muwezeshaji ili atoe maelezo mafupi yanayohusu majadiliano haya.

 MAELEZO YA MUWEZESHAJI

Muwezeshaji aliwafahamisha washiriki juu na umuhimu wa kuchangia katika Katiba hii na taratibu zinazotakiwa kufuatwa

  • kutochanganya siasa,dini na kabila katika majadiliano ya rasimu ya katiba
  • kuheshimu maoni yanayotolewa na mshiriki mwengine
  • kutoingiliwa katika utoaji wa maoni
  • kutoa hofu na kuwapa fursa ya kushiriki kikamilifu na bila woga katika kutoa maoni ya rasimu ya katiba mpya
  • kuwataka kila mshiriki kuzungumza ili kuweza kutumia haki yake ya kikatiba.

 Muwezeshaji aliweza kuwagawa washiriki katika makundi ambayo yalikuwa makundi matatu, washiriki waliweza kushiriki kikamilifu katika makundi yao na

Baada ya muda wa mijadala kumalizika, washiriki walirudi kwenye mjadala wa pamoja na kutoa hoja zao kama ifuatavyo;

 MADA; 1 Aina ya muungano(sura ya 6 ya rasimu)

               2 Mambo ya muungano(mambo saba ya muungano yaliopendekezwa)

1 AINA YA MUUNGANO:-

Mshiriki wa kwanza

-Amependekeza kuwa na serikali moja

Sababu: Inaleta amani kwani kila kitu kiko chini ya serikali moja

Pia gharama za serikali zitakuwa mahali pamoja

Wanakikundi walitoa ufafanuzi katika eneo la gharama kutokana na kuwa na serikali moja kutasaidia makusanyo ya pamoja na kugawa kwa pamoja tofauti na sasa ambapo tunagawana nchi mbili ambapo zanzibari ni ndogo sana tofauti na Tanzania bara

 Mshiriki wa 2

Amependekeza muungano wa serikali moja

Sababu:mabalozi hawatakuwa watatu wala wawili bali mmoja

Muungano wa serikali nyingi ni gharama

Uraia utakuwa mmoja kwa pande zote

 Mshiriki wa 3

Amependekeza muungano wa serikali moja

Sababu:maliasili zilizipo zitatumika kwa pande zote

Watanzania bara hawatakuwa wageni Zanzibar bali watu wote watakuwa kitu kimoja

Mshiriki huyo alitaka kiboreshwe kipengele cha tatu ambacho kinaeleaea uraia na uhamiaji mchiriki alitoa hoja kuwa mpaka sasa Zanzibar wanavitambulisho vyao na Tanzania bara wanavitambulisho vyao kitu ambacho kikiachwa kinaleta mgawanyo katika muungano

 Mawazo ya washiriki wengine ya

meuwiana na mapendekezo ya hapo juu

 MAONI YA SIKU YA PILI NA YA TATU

 UTANGULIZI

Mwenyekiti aliwakaribisha washiriki ukumbini mnamo saa 3.12 na kuwashukuru wajumbe na kuwatakia majadiliano mema kisha alimkaribisha mwezeshaji.

 Mwezeshaji naye aliwakaribisha washiriki kwa kuwataarifu kuwa tunaandelea kuwasilisha maoni ya siku ya kwanza kutokana na aina ya muungano na mambo saba ya muungano.

 Mwezeshaji aliwapa washiriki fursa ya kujadili vipengele vilivyomo katika katiba ili baada ya majadiliano watoe maoni yao

 Washiriki walipata chai 4:00 baada ya chai washiriki walirudi ukumbini na mwezeshaji akaendelea kuwashirikisha wanavikundi kutoa maoni yao pia tulipata waandishi wa habari toka gazeti la Habari leo,Mwananchi,Tumaini.

 MAONI

Mshiriki:I, alipendekeza kuwa wananchi wawe na haki ya moja kwa kufanya uchaguzi wa kisheria kuhusu suala la madaraka ya ni yaani yani kuwe na ukomo

Sura ya saba, ibara ya 74

 Mshiriki:IIAlishauri kuwepo na katiba tatu yaani kuwe

Sura ya pili katiba ya serikali ya Zanzibar

Ibara ya II katiba ya Tanganyika na katiba ya Tanzania bara

Mshiriki III . Alipendekeza kuwa spika na naibu spika wasichaguliwe na bunge ila wateuliwe na Raisi na kuthibitishwa na bunge

Sura ya tisa ibara 128

 Mshiriki IV: alipendekeza kuwa wafanyakazi wa makampuni wapewe haki zao bila kujari umri wao wanapostaafu.

Sura ya 4 ibara 35

 Mshiriki V: alipendekeza kuwa vikwazo vya elimu viondolewe

-kuwajengea wanafunzi maabara

-kujenga hostori kwa serikali

-walimu wajengewe nyumba karibu na shule

-kuwajari walimu

-kuwaongezezea vifaa mashuleni

Sura ya kwanza ibara 41

Mshiriki VI:Alipendekeza kuwa katika elimu,elimu hisiyo rasmi ipewe kipaumbele ili kuboresha vipaji vya vijana na watu wazima hasa katika suala ubunifu ili elimu ya Tanzania iwe ina msaidia mtanzania.

Sura ya kwanza ibara ya 41

 Mshiriki VII:Alipendekeza kuwa vyanzo vya mapato viwe na ushuru wa pande zote mbili yaani kuwe na ushuru wa Tanzania bara na ushuru wa Tananzia wa Tanzania visiwani

Sura ya nne ibara 212

 Mshiriki,IX:Alipendekeza haki za wazee zitekelezwe na kupatiwa huduma nzuri wanazostahiri

Sura ya 1 ibara 47

 Mshiriki X: Alipendekeza kuwa ushiriki uzingatie uwiano wa washiriki wa muungano katika bunge la jamhuri wa muungano wa Tanzania kuwakilishwa na watu wenye ulemavu

Mambo ya muungano ibara 7

 Mshiriki XI:Alipendekeza kuwa endapo Raisi atakuwa amefanya kosa lolote ashtakiwe kama raia wengine

Sura ya 1, ibara 83

 Mshiriki XII: Alipendekeza kuwa madeni ya nchi yafahamike kwa wananchi kwa kupitia vyombo habari na mikataba iwekwe wazi

Sura ya 4 ibara ya 215

 Mashiriki XIII:Alipendekeza kuwa taifa liingilie kati suala la mavazi ili kulinda hadhi ya Taifa, kipengele cha utamaduni kifafanuliwe ili ziwabane vijana katika kudumisha utamaduni wao

Sura ya 1, ibara 43

 Mashiriki XIV: Anapendekeza kuwa watoto wazaliwapo wapate cheti cha kuzaliwa mahali alipozaliwa kuepuke usumbufu

Sura 2 ibara 42

Mshiriki XV: Alipendekeza limetolewa kuwa uhuru wa habari uwe na mipaka ili vyombo vya habari visitoa taarifa zinazopotosha wanachi.

Mashiriki XVI: Alipendekeza kuwa Mawaziri wachaguliwe kama wanavyochaguliwa wabunge na Raisi

Sura 4 ibara 30                                                                                                

Mashiriki VIII: Alipendekeza kuwa katika mfumo wa ajira usizingatie udhoefu bari mtu achaguliwe moja kwa moja kutoka chuoni bila kujari udhoefu

Sura ya 4 ibara ya 35

 Mshiriki XVIII: Alipendekeza serikali imarishe mazingira kuhusu watoto wa mitaani hadi hadi ngazi ya kijiji

Sura ya 4 ibara 42

 Mshiriki XIX:Alipendekeza kuwa wananchi washirikishwe katika kura za maoni kwa kupitia vyama vyao na matokeo yaishimiwe kikatiba kwa mgombea aliyepata kura nyingi

Sura ya saba ibara ya 74

 Mshiriki XXI:`Alitoa mapendekezo kuwa kiswahili kiwe lugha ya Taifa hata katika mikutano ya kimataifa na endapo kuna wasio kijua kuwa na wakalimani

Sura ya 1,ibara ya 4

 MshirikiXXII:Mahakama iwe na porisi jamii ili atoe elimu kwa wananchi juu ya haki zao na kuwepo na ukomo wa ajira katika majaji badala la miaka 70 iwe 60 kama wafanyakazi wengine

Sura ya 10 ibara ya 155

 Ibara ya 75 hadi 79

Madaraka ya Raisi

Sifa

Ukomo

Kwamba makamu wa raisi ndio atakaye chukua majukumu ya raisi

Kitu ambacho wananchi wananyimwa fursa ya kumchagua mtu wanaemtaka inawezekana kuwa raisi ameshirikiana na makamu wa raisi hivyo kuinasababisha ubovu kuendelea

Maswali

-Katiba ni nini

-Faida za kushiriki katika katiba

-Je rasimu hii ndio katiba

-Kuna tofauti gani kati ya katiba ya zamani na rasimu hii

-Je katiba hii ikikamilika mtatuletea kama mlivyotuletea wakati huu wa kuajadiri

-Kwa nini hamjatoa mafunzo ya kujua jinsi ya kusoma ibara katika katiba

-Wasiojua kusoma na kuandika watachangiaje

-Kwa nini hakuna rasimu iliyochapwa kwa lugha ya wasiona

CHANGAMOTO

Uelewa wa washiriki kuhusu rasimu ya katiba ni mdogo

Washiriki kutoudhuria katika muda muwafaka

washiriki wamedai posho kinyume na masharti ya mkataba     wetu na mfadhili

kutoamini kwamba kinachofanyika ndicho walichoelezwa

kudhani kuwa katiba ni mambo ya siasa na kusababisha ushiriki mdogo wa baadhi ya wananchi

 MAPENDEKEZO

Kufanya mafunzo uhamasishaji jamii juu ya kufahmu vifungu na ibara mbalimbali katika katiba

Mikutano na vikundi na mashirika yasio ya kiserikali na kutafuta wafadhili kwa mgongo wa tume

Ruzuku itolewe kwa wakati

Muda uongezwe katika majadiliano

Viongozi wa serikali wasiangalie mabaraza yao tu wawe na hali ya kuunga mkono shughuli za kitaifa kwa maslai ya Taifa

 

SHUKRANI

Mwela theatre group makao makuu DSM tunawashukura kwa kutupatia msaada wa kitaalamu tangia uandishi wa mradi,utekeleza na uandishi wa taarifa kwa kuhakisha tunatekeleza mradi kwa ufasaha kama mkataba unavyosema

 

Tunawashukuru The foundation for civil society kwa kutupaitia Ruzuku na kuonesha uaminifu kwetu kuwa tunaweza kutekeleza mradi huu na tumeitumia vizuri fursa hiyo

 

Tunawashukuru waandishi wa habari wa gazeti la habari leo,mwananchi,gazeti tumaini na Redio huruma

 

Tunawashukuru viongozi wa vijiji na kata kwa kutuhakikishia usalama na kutupatia maeneo ya kufanyia shughuli zetu bila bughudha yoyote

 

Tunawashukuru walimu na wanafunzi wa shule ya kiluwai kwa kushirikiana na sisi muda wote na kutuvumilia kutokana na mijadala iliyokuwa ikifanyaka shuleni hapo

 

Tunawashukuru wananchi na washiriki wote wa kijiji cha kiluwai na kidundai kwa kuonesha moyo wa kuwa nasi bega kwa bega mwanzo mwa uandishi wa mradi huu utekelezaji wake mpaka tulipofikia

 

HITIMISHO

Serikali itoe fungu na kuwashirikisha vikundi na asasi za kiraia katika masuala makubwa kama haya ya kitaifa tangia mwanzoni ili kuongeza tija na ufanisi katika jamii na kuleta maendeleo ya Taifa letu

 

UTANGULIZI

Mwela theatre group vuga ni shirika lisilo la kiserikali lenye nia ya kuikomboa jamii kwa njia ujasiliamali ili waweze kujikomboa katika suala la uchumi na kuweza kutatua matatizo yoa yenyewe                    katika kujua na kuifahamisha jamii dhana ya ujasiriamali                                                                 ujasiliamali kama somo limetokea kupendwa sana katika eneo la mradi na kuwa kivutio kwa washiriki na hata wale ambao wamesikia mafunzo hayo yakiendeshwa lakini hawakupata fursa ya kushiriki lakini pia nao wamevutiwa kwa kiasi kikubwa ila kutokana na mradi huu wa ujasiriamali kukosa mfadhili na mwela kuamua kuendesha wao wenyewe kwa michango yao bila ufadhili umeona kuchukua watu wa chache na hivyo kuacha malalamiko kwa baadhi ya watu                                                                                                 

kutokana na utafiti mdogo tuliofanya tumegundua kuwa faida za kiufundi  za ujasiriamali kwa wananchi kunaumuhimu mkubwa kwani ujasiriamali unaweza leta mabadiliko wa ukuwaji wa kiuchumi katika jamii kwani utawawezesha hata wale ambao wamekosa elimu ya msingi,sekondari na vyuo wanaweza wakajikwamua kiuchumi.                                                                                                                            

Inakadiliwa mnamo mwaka 1700 ndio zana ya ujasiriamali ilipogunduliwa lakini mpaka leo bado sehemu nyingi hasa za vijiji bado kunachangamoto nyingi kutokana na watu wengi hawajajua somo ili la ujasirimali

Mwela vuga inaamini ujasirimali ni zaidi ya dhana ya biashara tunaamini mjasirimali ni mtu ambaye anaweza kutoa jambo/wazo jipya ambalo litaweza kumpa faida

Masoma haya ya ujasiriamali yamewafanya kinamama hawa kuwa:

  • Kuwa wathubutu
  • Kuwafanya wasiogope kufeli/kushindwa
  • Kuwafanya waweze kutafuta njia/mbinu mpya za kuzalisha na kuleta mabadiliko
  • Kuwafanya wawe wavumilivu
  • Kuwafanya wawe viongozi wazuri
  • Kuwafanya wawe washindani
  • Kuwafanya wasikate tamaa
  • Kuwafa nya wawe wawajibikaji wazuri katika shughuli zao
  • Wawe wenye mtazamo chanya wa kusonga mbele
  • Wenye uwezo wa kutumia fursa

 walengwa wa mradi                                                                                                          wanawake 60 toka katika vijiji  vya Bazo,Vuga,Kiluwai na Kidundai toka Kata ya Vuga Jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto

 

Malengo ya mafunzo

  • Ni kuwasaidia kinamama watokanae na dhana ya utegemezi kwa kuboresha hali yao ya kipato kwa kuchochea maendeleo yao
  • Ni kutoa dhana potofu katika jamii juu ya ujasiriamali ni kipaji cha kuzaliwa nacho na kuwapa uelewa kuwa ujasiriamali ni ubunifu na kutumia fursa zilizopo
  • Kuwajengea uwezo wajasiriamali Kuyabadili matatizo na kuwa fursa
  • Kuwawezesha wajasirimali kuanzinsha na kumiliki vitega uchumi
  • Kuwawezesha wajasiriamali Kubadili utashi wa kimaisha ndani ya kazi na ajira
  • Kuwawezesha wajasiriamali kuwa na usimamizi mzuri wa biashara
  • Kuwawezesha wajasiriamali dhana ya biashara na namna ya kutafuta masoko
  • Kuwawezesha wajasiriamali kujua dhana ya kununua,kuuza, kazalisha mali utaalamu na kuwa wito kwa wateja
  • Kuwawezesha wajasirimali kujua namna upatikanaji wa bidhaa na huduma inayotarajiwa kutolewa,idadi ya washindani wanaouza na kutoa bidhaa hiyo,matakwa ya wateja katika eneo hilo na gharama za uendeshaji wa biashara hiyo

 

matokeo

  • Washiriki wamefahamu kuwa si kila anayeuza au mfanyabiashara ndogo ndogo ni mjasiriamali. Kwa ufupi wamegundua kuwa mjasiriamali ni mtu yeyote ambaye haogopi kuweka mipango na kushindwa, tofauti na mfanyabiashara yeye huwa na mtazamo wa kuwekeza kwa ajili ya faida pekee. Wamegundua kuwa Mjasiriamali mhimili wake mkuu ni ubunifu,uzalishwaji wa bidhaa mpya, na kujua njia mpya za uzalishaji kutafuta masoko mapya na utumiaji wa rasilimali zinazomzunguka.                                                                                                                              Wamelewa Ubunifu na uvumbuzi ni suala muhimu kwa Mjasiramali haswa ni yule anaeyekuwa na kubuni vyanzo na mbinu mbalimbali za kuboresha utendaji wake wa kazi
  • Wamefahamu kuwa Kukua na kupanuka kwa mjasiriamali ni      muhimu mjasiriamali akue na kutanuka kimaslahi na si kuwa katika hali moja      tu kila mara, anapaswa kutanuka kimtaji,kiutendaji na kimahusiano, hili      huboresha huduma na uwanda wake wa malengo. Hivyo ni muhimu pia      majaisiriamali kuwa mtu wa mipango na kuwa na uelekeo Fulani anaotaka      kufikia Kujaribu na kudhamiria:      Mjasiiramali si mtu wakuaogopa kutenda pindi aionapoa fursa na kuitathmini      kuwa inapaswa kuendewa. Hivyo si muoga katika kujaribu
  • Wamefahamu kuwa       mjasiriamali lazima hawatambue Washindani wake na kuelewa ushindani si uadui.Kama unataka kuwa      mjasiriamali mwenye mafanikio ni vizuri sana ukawajua washindani wako wa      kibiashara. Na Mshindani wako anaweza kukufaa katika kazi zako Anaweza kuzidiwa na kazi na akaweza      kukupa kazi nyengine ni vyema      .kujitambulisha,na kujenga uhusiano mzuri wa wajasiriamali wengingine

 

  • Washiriki wamefahamu kuwa ili wateja wengi husikia kwanza jina la biashara au shughuli yako kabla hawajapata habari kamili kuhusu biashara huduma au biashara hiyo hivyo tumefahamu kuwa unapotaka kuanza bishara lazima uanze na taswira nzuri pia wamefahamu jinsi ya kutafuta jina la biashara na kujua kuwa jina la linatakiwa kuwa fupi,la kipekee na jepesi kukumbuka kuwa na wepesi kwa wateja wapya unaotaka kuwapa habari ya biashara yako ili uwateke hisia za wateja wako
  • Washiriki wamefahamu dhana ya ujasirimali na kufahamu kuwa mjasirimali ni mtu yeyote ambaye ana hamasa ya kuleta mabadiliko chanya katika hali yake ya kiuchumi na anatabia za kipekee ili kufanikisha azma yake kwa kujishughulisha yani kujiajiri, wamefahamu kuwa neno ujasiriamali linatokana na neno la kifaransa “Entreprendre” sawa na kutekeleza/kufanya shughuli Fulani mwenyewe katika uwanja wa biashra katika maana rahisi ni sawa na kuanzisha bishara /shughuli ya kujiajiari.     Kwa mitazamo ya mbalimbali ya wasomi wana muelezea Mjasiriamali kama mtu anayeongoza,anayepanga na aliye na utayari juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara/shughuli yake husika .                                                               Mchimi Kiaustrian Joseph Schumpeter amelezea kuwa ujasirimali kwa kuegemea mihimili ya ugunduzi na ubunifu katika Nyanja hizi za kugundua na kubuni
  1. Bidhaa mpya
  2. Njia za udhalishaji /uendeshaji
  3. Masoko mapya
  4. Mifumo mipya ya vikundi na mashirikisho

 

  • Washiriki wamefahamu kuwa neno ujasiriamali linatokana na maneno ya Kiswahili ambayo ni UJASIRI na MALI hivyo ujasiriamali ni ujasiri au mashawasha wa kutafuta na kupata mali na uwezo wa kutambua fursa za biashra kwa haraka na uthubutu wa kuziendea na kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza na uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzui utekelezaji wa fursa za bishara            

 

  • Washiriki wamefahmu kuwa ujasiriamali ni utashi wa kitu na njia ya kufikiria ,kufikia na kufanya jambo au kitu fulani pia wamefahamu ujasiriamali ni mchakato ambapo mtu anachukua hatua ya kutumia fursa bila kujali hali ya rasirimali alizonazo. Ni mchakato ambapo mtu anafanisi,kusimamia ,kuandaa na kuratibu ubunifu,uboreshaji na uvumbuzi,kujenga thamani na uthamini kwa jamii inayomzunguka wamefahamu kuwa mchakato upelekea mjasiriamali kuwa na ubunifu na kukua,kujenga,kuunda kundi/faida taasisi kujenga thamani

 

 

  • Washiriki wamefahamu kuwa Mjasiriamali ni Mtu ambaye “anathubutu kufanya,” Jambo, vitendo au mradi wenye manufaa”.• “Aliyechochewa au mwenye vichocheo vya kuendelea kiuchumi kwa kutafuta na kubuni njia mpya za kujikwamua na kufanya mambo”. “Mjasiriamali kwa tafsiri ya Drucker, ni ahamishae rasilimali kutoka eneo lenye uzalishaji mdogo na kupeleka katika eneo lenye uzalishaji mkubwa na mavuno mengi na ili ufanikiwe katika shughuri au biashara unayofanya au unayotarajia kufanya ni lazima uwe na mtazamo sahihi na mtazamo chanya. ujasiriamali una kanuni zake amboazo ni muhimu sana ili mtu afikie mafanikio aliyoyapanga,kama mtu akishindwa kufuata kanuni hizo basi anakuwa na nafasi ndogo ya kupata mafanikio katika shughuri yake. Pia washiriki wamefahamu Tabia za ujasiriamali zinaweza kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na kuzifuata,lakini  tabia  zingine  hazifundishiki hizi ni zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti katika kufikili,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo ambazo haziwezi kufundishika. tabia ambazo zinafundishika ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika biashara. Zifuatazo ni tabia za ujasiriamali.

 

MAONI

Ujasiriamali ni kiungo muhimu katika kukuza,kuendeleza ni njia mbadala ambayo inaweza kuongeza nafasi za ajira na kipato na kuongeza uchumi na kupunguza umaskini ni wajibu wa serikali,asasi na tasisi mbalimbali kujitolea katika kuwasaidia watu maskini ambao wengi wao tunaishi vijijini

Changamoto za wajasiriamali

  • Mtaji
  • Utumiaji wa fursa
  • Ubunifu
  • mawasiliano

Jinsi tulivyokabiliana nazo

mtaji

tuliweza kuwafahamisha kuwa mtaji ni kitu chochote ambacho mjasiriamali anawezatumia katika kuzalishia au kufanyia jambo Fulani kwa ,lengo la kupata faida kuondoa mtazamo wao wa mwanzo wa kuwa mtaji ni fedha tu na kuwaelewesha kuwa mtaji umegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo fedha,nguvu kazi,elimu na utaalamu                                                               

fursa                                                                                                                              wajasiriamali wengi hawatambui fursa zilizopo na ivyo kuwajengea uwezo wa kutambua fursa au kugundua fursa na uwezo wa kuchambua na kuchanganua fursa zilizopo

ubunifu

tuliwajengea uwezo wajasiriamali kuwa na ubunifu na ndio hasa dhana ya mjasiriamali unatofautisha mtu mmoja na mwengine hata kama wote wanafanya jambo linalofanana  na kuwajengea uwezo wa kufikiri ya jinsi gani watafanya jambo jipya tofauti na linalofanywa na watu wengine lakini wao wafanye tofauti                                                                    

mawasiliano                                                                                                                 wajasiriamali wengi uwa wanashindwa kuendelea kutokana na kuwa na mawasiliano mazuri na wateja wao                                                                                                                mawasiliano huunganisha watu pamoja na usaidia kupata taarifa mbalimbali     muhimu katika biashara                                                                                            mawasiliano uboresha biashara na kumfanya mjasiriamali afanikiwe katika ujasiriamali wake

 MAHITAJI  

  • Machine ya kutengeneza sabuni –Ploder
  • Mashine ya kukata chips    
  • clutcher ya kupikia sabuni ni around
  • around equipment  
  • mafuta ya kupikia sabuni
  • mashine ya kutengenezea chaki
  • kuongezea ufahamu juu kutengeneza batiki,chaki na sabuni za miche na za unga
  • kusaidiwa vifungashio vya sabuni ya maji,sabuni ya usafi wa mikono na dawa ya usafi wa vyoo    
  • kupatiwa Sulphonics acid, Soda ash,Sless,Perfume,Rangi,Ghloride acid/ya unga,Caustic soda,mafuta (ambosa,mawese,nazi,nyonyo),Grycelin,Hydrogen Peroxide,Paraffin wax,Mould,Stearine au mixtire,Boric acid,Hydrochloric acid,Soda ash,Vinegar,Cmc,Grycelin, Sodium hydroxide na formalin                                                                              

 

SHUKRANI

  • Wanachama wa mwela theatre group vuga kwa kukubali kuchangia pesa zao kwa ajiri ya kuisaidia jamii juu ya uandaaji wa mafunzo haya na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mafunzo haya
  • Muweshimiwa Diwani wa kata ya vuga kwa kutufungia mafunzo yetu
  • Mama Diwani kwa kutupatia ukumbi wa kufanyia mafunzo yetu
  • Wanachama wa Chama cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii vuga kushirikiana nasi kwa karibu
  • Mtendaji wa kata ya vuga kwa kushirikiana nasi wakati wote wa mafunzo
  • Jumaa dhahabu kwa ushauri wa mara kwa mara kipindi cha utekelezaji wa mradi huu
  • Vikundi vya kinamama vya ujasiriamali kwa kuutunga mkono na kujigharamia wenyewe chakula na nauli
  • Jamii inayotuzunguka kufurahia mradi huu na kutaka kuufanyia muendelezo kwa kuona umuhimu wa mradi huu
  • Hassani sheshe kwa kutoa ushauri wa kihasibu kwa mwela theatre group vuga wakati wote wa utekeleza wa shughuli za mwela vuga

 

ITIMISHO

  • Utengenezaji wa sabuni unatoa ajira hivyo kuongeza kipato katika familia.
  • Sabuni zinaweza kutengenezwa bila kuwa na mitambo mikubwa sana
  • Mtu anahitaji sabuni kwa shunguli zote za usafi ili kutunza afya yake .
  • Itakuwaje sabuni ya kutumia inapatikana kwa gaharama kubwa wakati familia nyingi ni masikini.
  • Usafi na elimu nzuri ya afya ni muhimu na nafuu kuliko aina nyingine za madawa.

                                  

 tunaomba wadau wa maendeleo tunawaomba muje Vuga tushirikiane juu ya miradi mbalimbali ya kijamii kwani kunachangamoto nyingi na wafadhili wengi hawajafika hivyo tunashindwa kukabiliana navyo kutokana na kukosa rasimarimali za kutosha