Ni kuwa chombo imara cha ushawishi na uteteziwa maslahi na maendeleo yavijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo ili kujenga mshikamano wa kimkoa na hatimaye kitaifa
1.0. JINA, ANUANI, HADHI, DIRA NA UTUME WA SHIRIKA.
1.1 Shirika litajulikana kwa jina la MSHIKAMANO wa VIJANA WAZALISHAJI WADOGO WAFANYABIASHARA WADOGO NA TANZANIA ambao kifupi chake kitakuwa MWAVIWAWATA.
1.2 Shirika litakuwa ni shirika lisilo la kiserikali, lisilolenga kugawana faida na pia lisilojihusisha au kushabikia itikadi za kidini na siasa.
1.3 Makao makuu ya shirika yatakuwa Mwanza na anuani yake itakuwa S.L.P. 1460 Mwanza Tanzania.
1.4 Shirika litafanya shughuli zake mkoa wa Mwanza na baadaye mikoa mingine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1.5 Dira ya shirika ni kuwa chombo imara cha ushawishi na utetezi wa maslahi na maendeleo ya vijana wazalishaji wadogo, wafanya biashara wadogo ili kujenga mshikamano wa kimkoa na hatimaye kitaifa, utakao hakikisha mawasiliano bora na uwakilishi wa ukweli wa mawazo yao ili kuwezesha ushawishi na utetezi wa maslahi ya vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo.
1.6 Utume wa shirika ni kuunganisha vijana na mshikamano wa vijana wazalishaji wadogo, wafanya biashara wadogo na utakao saidia kuhakikisha, ushiriki na uwakilishi wao katika michakato ya maamuzi kisera katika Nyanja za kiuchumi na kijamii hasa kwa kupitia mafunzo. Ufuatiliaji wa maendeleo yao kiuchumi na kijamii mkoani kote na hatimaye nchini kote.
1.7 Shirika litasajiliwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali 2002 (sheria namba 24 ya mwaka 2002) kama ulivyorekebishiwa mwaka 2005.
2.0 TAFSIRI.
Isipokuwa pale ambapo imeelezwa waziwazi vinginevyo maneno yaliyotumiwa ndani ya katiba hii yatakuwa na maana kama inavyoonyeshwa hapa chini:-
2.1 Bodi ya Wakurugenzi inamaanisha chombo kinachosimamia na kutoa mwelekeo wa kisera kwa menejimenti katika utekelezaji wa shughuli za shirika.
2.2 Halmashauri inamaanisha chombo kinachoundwa, na viongozi kutoka ngazi za wilaya na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
2.3 ‘Katibu’ ina maanisha Katibu wa Mwaviwawata katika ngazi ya wilaya na imeondoa utata katika ngazi ya mkoa, Katibu inamaanisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika.
2.4 Kiongozi inamaanisha mjumbe ama wa kamati ya uongozi katika ngazi husika na au mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika katika ngazi ya mkoa au mwakilishi katika kikao kilichoundwa kwa mujibu wa Katiba hii anayechaguliwa na kupigiwa kura na pia Mkurugenzi mtendaji anayeajiriwa na kufanya kazi kwa mujibu wa katiba hii.
2.5 Mjumbe ina maanisha mjumbe ama wa kamati ya uongozi katika ngazi husika au mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya shirika katika ngazi ya mkoa.
2.6 Mzalishaji mdogo , mfanyabiashara mdogo ina maanisha kijana na mwananchi yeyote aliyeajiriwa au asiyeajiriwa na ambaye kipato chake, kinategemea shughuli zake za uzalishaji, na ufanyabiashara.
2.7 Mkurugenzi Mtendaji, ina maanisha katibu wa shirika katika ngazi ya mkoa kwa mujibu wa katiba hii.
2.8 Mwanachama ina maanisha mwanachama wa MWAVIWAWATA kwa mujibu wa katiba .
2.9 Mweka hazina ina maanisha mwanachama aliyechaguliwa kutunza na kusimamia fedha na raslimali zingine za shirika katika ngazi husika.
2.10 Mwenyekiti ina maanisha mwenyekiti wa MWAVIWAWATA katika ngazi husika.
2.11 Ngazi ya mkoa inamaanisha shirika la MWAVIWAWATA shirika lisilo la kiserikali lililosajiriwa chini ya jina la MWAVIWAWATA kwa mkoa au wilaya husika linalofanya shughuli zake kama wakala wa MWAVIWAWATA na hii itaongozwa na makubaliano ya ndani.
2.12 Ngazi ya msingi ina maanisha mshikamano unaounganisha wanachama wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya Kata au Kijiji.
2.13 Shirika ina maanisha mshikamano wa vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo Tanzania.
2.14 Mfanyakazi au mtumishi ina maanisha mtu yeyote aliyeajiriwa na shirika au anaye jitolea kufanya kazi za shirika kwa hiari chini ya uongozi na maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji au mtumishi mwingine mwandamizi yeyote aliyeruhusiwa na anayejitolea kufanya kazi katika ngazi ya Mkoa, wilaya, kata, na kijiji. Hata hivyo neno mfanyakazi au mtumishi halitajumuisha kiongozi wa kuchaguliwa wa shirika, mtafiti au mshauri (mentor) au mtu mwingine yeyote anaye fanya kazi ya malipo au ya kujitolea kwa malipo ya mara moja au ya muda maalum kulingana na mkataba atakaokuwa ameingia kati yake na shirika.
1.0. LENGO NA MADHUMUNI YA SHIRIKA .
Shirika litakuwa na lengo la kuunganisha vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo wa Mwanza kwa kupitia mshikamano wao katika ngazi mbalimbali ili kuwa na sauti ya pamoja katika kutetea haki na maslahi yao kijamii na kiuchumi.
Katika kutekeleza lengo hili shirika litakuwa na madhumuni yafuatayo:-
1.1.1. kuboresha na kurahisisha mawasiliano kati ya wazalishaji wadogo, wafanya biashara wadogo na wakulima wadogo na wadau wa maendeleo ili kujenga kwa pamoja mbinu na mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maslahi vijana wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wadogo kijamii na kiuchumi.
1.1.2. Kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu juu ya shughuli mbalimbali zinazohusiana na uzalishaji, ufanyabiashara ili kuboresha maisha na kuinua maslahi ya vijana kijamii na kiuchumi.
1.1.3. Kuwakilisha vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo katika mashauriano na serikali juu ya maswala mbalimbali yanayohusu au yanayoathiri ufanisi na maslahi ya vijana wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wadogo wa Mwanza Tanzania kiuchumi na kijamii.
1.1.4. Kuunganisha vijana wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wadogo wa Mwanza Tanzania na mashirika, vyama na Taasisi mbalimbali za vijana ndani na nje ya nchi.
1.1.5. Kusaidia kuongeza ufanisi wa vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo wa Mwanza Tanzania katika kuboresha jitihada za kupambana na umasikini.
1.1.6. Kufanya jambo au mambo mengine yeyote halali ambayo yatapelekea kufanikisha utekelezaji na ufikiwaji wa malengo na madhumuni ya shirika.
3.2. Ili kutekeleza malengo na madhumuni ya shirika yaliyoainishwa katika katiba hii. Shirika litapanga na kutekeleza shughuli zifuatazo:-
3.2.1. Kuandaa, kubuni, kutathimini na kutekeleza miradi na mipango mbalimbali yenye kuwaendeleza na kuwajengea uwezo vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla kutetea maslahi yao.
3.2.2. Kuandaa mikutano na warsha kuhusiana na mada zinazowagusa au kuathiri maslahi ya wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo wa Mwanza.
3.2.3. Kuandaa au kuwezesha ziara za mafunzo ya vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo na ndani na nje ya Tanzania.
3.2.4. Kuandaa na kuwezesha mafunzo kwa vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo sambamba na kutoa ushauri elekezi kwa wanachama wa shirika.
3.2.5. Kuandaa na kuchapisha majarida kama chombo cha mawasiliano kwa lengo la kusambaza maarifa, ujuzi na uzoefu wa vijana wazalishji wadogo na wafanya biashara wadogo Tanzania.
3.2.6. Kufanya tafiti na kuweka kumbukumbu ya shughuli za vijanawazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo katika ngazi zote na yote yahusianayo.
3.2.7. Kushirikiana na mashirika, Taasisi, vikundi, mitandao ya Asasi, serikali na wadau wengine wa maendeleo ndani na nje ya Tanzania.
3.2.8. Kujihusisha na shughuli mbalimbali za ushawishi na utetezi kwa maslahi ya vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo Tanzania.
3.2.9. Kuingia ubia na kushirikiana na taasisi, mashirika au vikundi vingine vyenye malengo yanayofanana na ya shirika.
3.2.10. Kuhamasisha na kuwezesha uanzishwaji wa vyombo vya kiuchumi vitakavyojenga uwezo wa vijana wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wadogo kama vile vyama vya wazalishaji wa kila Nyanja, mitandao ya kuweka na kukopa , mitandao ya tovuti zenye habari za masoko ya bidhaa zinazozalishwa na wanachama , vituo vya kuongeza thamani bidhaa, mazao na miradi mingine ya kiuchumi.
3.2.11. Kufungua na kuendesha akaunti katika mabenki na Taasisi mbalimbali za fedha.
4.0. UANACHAMA NA JINSI YA KUJIUNGA NA SHIRIKA .
4.1. Shirika litakuwa na wanachama wa aina tatu (3)
a) Kikundi cha vijana wazalishaji wadogo, wafanya biashara wadogo ambao wamejiunga na umoja kwa lengo la kutekeleza shughuli zao.
b) Kijana mzalishaji mdogo , mfanya biashara mdogo aliye mwanachama au asiye mwanachama katika kikundi , mtandao, shirika , mwanachama wa MWAVIWAWATA kwa mujibu wa Ibara 4.1.1. ya katiba hii mwenye sifa zifuatazo:-
- Awe na umri usiopungua miaka kumi na tano (15).
Atakuwa mwanachama wa kawaida wa MWAVIWAWATA na mwenye haki sawa na mwanachama kikundi.
4.1.2. Wanachama vyama, mashirika na mitandao ya vijana wazalishaji wadogo, wafanyabiashara wadogo, wadogo vinavyojishughulisha na utetezi na ushawishi wa maslahi ya vijana wazalishaji wadogo na wafanya biashara wadogo vilivyosajiliwa chini ya sheria yeyote ya Tanzania katika ngazi za kata, wilaya, mkoa na Taifa vinaweza kuomba kuwa mwanachama wa shirika iwapo vinakubaliana kwa dhati na malengo na madhumuni ya shirika.
4.1.3. Wanachama washiriki.
Mtu yeyote au Taasisi au kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono malengo na madhumuni ya shirika anaweza kutamkwa na mkutano mkuu katika ngazi husika kuwa mwanachama mshiriki baada ya kushirikiana na ngazi ya mkoa.
4.2. UTARATIBU WA KUJIUNGA NA SHIRIKA.
4.2.1. Wanachama wa kawaida.
a) Kikundi kitaomba uanachama wa shirika kwa kujaza na kuwasilisha fomu za maombi kwa Katibu wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya kata , wilaya, mkoa kikionyesha idadi ya wanachama kilichonacho na mamlaka inayokitambua.
b) Maombi yote ya uanachama yatawasilishwa katika ngazi husika kupitia ngazi inayo husika.
c) Kijana mzalishaji mdogo, mfanyabiashara mdogo, mtu binafsi atapata uanachama wake moja kwa moja mara tu atakapojaza fomu na kukubaliwa kuwa mwanachama wa shirika.
d) Mkutano mkuu wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya mkoa utapokea orodha ya wanachama wapya kila unapokutana na unaweza ama kumkubalia au kumkatalia mwombaji yeyote kuwa mwanachama.
4.2.2. Wanachama vyama, mashirika na mitandao ya vijana na wazalishaji wadogo.
Vyama , mashirika na mitandao ya vijana wazalishaji wadogo, wafanya biashara wadogo, vinavyojishughulisha na ushawishi na utetezi kwa maslahi ya vijana vilivyosajiliwa kwa sheria yeyote Tanzania vitaomba uanachama kwa kujaza fomu za maombi kwa katibu wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya wilaya , na mkoa kupitia ngazi zote kikionyesha idadi ya wanachama na mamlaka inayokitambua.
4.2.3. wanachama washiriki.
a) Mkutano mkuu wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya mkoa utakuwa na mamlaka ya kuthibitisha au kukataa mapendekezo ya uteuzi wa mtu binafsi, taasisi au kikundi cha vijana kilichopendekezwa kuwa mwanachama mshiriki.
b) Bodi ya wakurugenzi baada ya kushauriana na ngazi ya wilaya husika itawasilisha mapendekezo ya uteuzi wa mwanachama au washiriki kwenye mkutano huu.
4.3. ADA NA KIINGILIO.
Kutakuwa na malipo ya ada na kiingilio yatakayolipwa na kila mwanachama wa shirika.
4.3.1. Wanachama waliokubaliwa kuwa wanachama watalipa kiingilio cha uanachama katika viwango vifuatavyo:-
a) Kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (Tshs. 2000.00) kwa kila mwanachama binafsi.
b) Kiingilio cha shilingi elfu tano tu ( Tshs. 5000.00) kwa kila mwanachama kikundi
c) Kiingilio cha shilingi elfu kumi na tano tu (Tshs. 15,000.00) kwa kila mwanachama wa shirika, chama cha uzalishaji , au wafanyabiashara vijana, au mtandao wa wazalishaji wadogo.
4.3.2. Kila mwanachama atalipa ada ya mwaka ya uanachama kila mwaka katika viwango vifuatavyo :-
a) Kila mwanachama atalipa ada ya mwaka ya uanachama kila mwaka ikiwa ni Tshs. 3000.00 (shilingi elfu tatu tu) kwa kila mwanachama binafsi .
b) Ada ya mwaka ya wanachama ya shilingi elfu kumi tu (Tshs.10,000.00) kwa kila mwanachama wa kikundi.
c) Ada ya mwaka ya wanachama ya shilingi elfu ishirini tu (Tshs. 20,000.00) kwa kila mwanachama shirika, chama cha uzalishaji, au wafanyabiashara vijana au mtandao wa wazalishaji wadogo.
4.3.3. Mkutano mkuu katika ngazi ya mkoa unaweza kubadilisha au kuongeza viwango vya kiingilio na ada ya mwaka vilivyoorodheshwa katika ibara hii kila inapoonekana inafaa.
4.4. HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA .
4.4.1. HAKI ZA WANACHAMA.
Kila mwanachama wa shirika atakuwa na haki zilizoainishwa katika ibara hii.
a) Mwanachama kikundi cha vijana
i. Kupata cheti cha uanachama.
ii. Kupiga au kupigiwa kura kupitia mwakilishi
iii. Kuhudhuria mkutano na mikusanyiko mingine ya shirika kupitia mwakilishi .
iv. Kupata taarifa mbalimbali za hali na maendeleo ya shirika kupitia mikutano mikuu ya ngazi husika.
v. Kutoa maoni kupitia mwakilishi
b) Mwanachama binafsi .
- Kupiga au kipigiwa kura kuchaguliwa kuwa kiongozi
c) Mwanachama shirika, chama au mtandao wa wazalishaji wadogo au wafanya biashara wadogo.
- Kupata taarifa mbalimbali za hali ya maendeleo ya shirika kupitia mikutano mikuu ya ngazi husika (wilaya na mkoa)
d) Mwanachama mshiriki.
- kupata cheti cha utambulisho wa uanachama .
4.4.2. WAJIBU WA MWANACHAMA.
Kila mwanachama washirika atakuwa na wajibu ulio ainishwa katika ibara hii.
a) Mwanachama kikundi .
b) Mwanachama binafsi .
c) Mwanachama shirika, chama au mtandao wa vijana wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wadogo.
- Kupiga au kupigiwa kura kupitia mwakilishi wake .
d) Mwanachama mshiriki.
- Kujitolea kutekeleza shughuli maalum za shirika kila inapohitajika
4.4.3. Kwa ujumla, kila mwanachama wa shirika atakuwa na wajibu wa kulinda na kutetea malengo na madhumuni ya shirika, katiba ya shirika na siri na maslahi ya shirika wakati wa uanachama wake na hata baada ya kukoma uanachama.
4.5. KUKOMA UANACHAMA
4.5.1. Uanachama wa shirika utakoma iwapo moja kati ya matukio yaliyoainishwa katika ibara hii yatatokea:-
a) Mwanachama kikundi.
- Kusambaratika au kufa kwa kikundi
b). Mwanachama binafsi .
- Kupatwa na ugonjwa wa akili na kutopona katika muda unaozidi miezi mitatu (3).
c). Mwanachama shirika , chama au mtandao wa vijana wazalishaji wadogo, na wafanyabiashara wadogo
- Kutolipa ada ya mwaka na michango mingine kwa kipindi cha miaka mitatu (3) mfululizo .
d). Mwanachama mshiriki.
- Kuondolewa uanachama na mkutano mkuu katika ngazi ya wilaya na mkoa .
4.5.2. Kwa ujumla, mwanachama ambaye uanachama wake utakoma kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichotoa , ada ya mwaka aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa kwa shirika.
5.0. MUUNDO WA SHIRIKA.
5.1. Muundo wa shirika utakuwa na ngazi tatu kama ifuatavyo;-
5.1.1. Ngazi ya mkoa
5.1.2. Ngazi ya wilaya
5.1.3. Ngazi ya Kata (msingi)
5.2. Ngazi ya wilaya zinaweza kusajiliwa chini ya sheria za Tanzania kuwa shirika lisilo la kiserikali au kuwa tawi la MWAVIWAWATA katika eneo la ngazi husika ambalo linaendesha shughuli zake lenyewe kwa kuingia makubaliano na ngazi ya mkoa na kufuata katiba, kanuni na miongozo mbalimbali ya shirika. Hata hivyo usajiri huo hautofanya ngazi ya wilaya husika kukoma kuwa sehemu ya MWAVIWAWATA.
5.3. Kwa ujumla shughuli na mamlaka ya shirika zitatekelezwa na wanachama au wawakilishi wao kupitia mikutano, vikao na vyombo vilivyoundwa na katiba hii ili kusimamiwa na kutekeleza shughuli za shirika katika ngazi husika.
5.4. Kwa ajili ya kuhakikisha uwiano mwafaka kijinsia. Kila chombo au mkutano au kikao kilichoundwa kwa mujibu wa katiba hii, kitakuwa na wajumbe wasiopungua theluthi moja yakila jinsia katika ngazi zote za shirika.
5.5. MUUNDO WA UONGOZI NGAZI YA MKOA.
Kutakuwa na vyombo na vikao vifuatavyo katika kutekeleza mamlaka na shughuli za shirika katika ngazi ya mkoa.
- Mkutano mkuu
- Halmashauri
- Bodi ya wakurugenzi
5.51. MKUTANO MKUU.
a) Kutakuwa na mkutano mkuu utakaofanyika mara moja kwa mwaka.
b) Mkutano mkuu utakuwa ndicho chombo cha juu zaidi na cha mwisho katika kufanya maamuzi juu ya maswala mbalimbali ya shirika.
c) Mkutano mkuu utafanya shughuli zifuatazo:-
- Kupitisha mpango kazi na bajetikwa mwaka unaofuata katika ngazi ya Mkoa
- Kufanya uchaguzi wa wajumbe kutoka katika ngazi ya mkoa watakaokuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaviwawata katika ngazi ya Mkoa
- Kuwajibisha wajumbe wa kamati ya uongozi katika ngazi ya mkoa
- Kupokea na kuthibitisha wan
- Kufanya uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya uongozi
- Kufanya jambo jingine lolote ambalo kwa kawaida hufanywa na mkutano mkuu wa
7.0. VYANZO VYA MAPATO , UTUNZAJI NA MATUMIZI YA FEDHA NA RASILIMALI ZA SHIRIKA.
7.1. Shirika litakuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato vifuatavyo:_
7.1.1. Kiingilio na ada ya mwaka ya uanachama.
7.1.2. Michango ya hiari ya wanachama.
7.1.3. Mauzo ya mazalisho , machapisho na huduma mbalimbali zitolewazo na shirika.
7.1.4. Mauzo ya vitu chakavu vya shirika.
7.1.5. Ruzuku kutoka ndani na nje ya nchi.
7.1.6. Vitega uchumi, uwekezaji, hisa na mapato mengine yahusianayo.
7.1.7. Mapato mengine yeyote yaliyo halali.
7.2. Fedha na rasilimali za shirika zitatumika tu kwa ajili ya kutekeleza malengo na madhumuni ya shirika yaliyoainishwa katika katiba hii.
7.3. Shirika litafungua na kuendesha akaunti za fedha katika benki na taasisi nyingine za kifedha.
7.4. Akaunti zote za shirika zitakuwa na jina la shirika . Mshikamano wa vijana wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wadogo na wafanyabiashara wadogo.
7.5. Katika ngazi ya mkoa akaunti za shirika zitaendeshwa na bodi ya wakurugenzi.
7.5.1 Fedha zote zitawekwa Benki , isipokuwa kiasi kidogo kitakachoamuiwa na bodi ya wakurugenzi kugharamia malipo madogo madogo ya kila siku.
7.5.2. Fedha zitakazowekwa Benki zitatolewa kwa hundi tu katika ngazi zote za shirika.
7.5.3. Hundi zote za malipo zitawekwa saini na watia saini wawili mmoja mmoja kutoka makundi mawili yaliyoainishwa hapo chini.
a) Kundi ‘A’ litaundwa na Mkurugenzi Mtendaji.
b) Kundi ‘B’ litaundwa na Afisa Tawala na Fedha, Afisa Mwandamizi yeyote atakayependekezwa na Mkurugenzi Mtendaji na kuthibitishwa kwa Azimio la Bodi ya Wakurugenzi.
7.5.4. Katika ngazi za wilaya za shirika akaunti za shirika zitaendeshwa na kamati ya uongozi ambapo Mratibu atakuwa mtia saini katika kundi ‘A’ na Mweka Hazina na mjumbe mmoja wa Kamati ya uongozi watakuwa watia saini katika kundi ‘B’ Hundi zote za malipo zitawekwa saini na watia saini wawili mmoja kutoka makundi mawili yaliyoainishwa hapo juu.
7.5.5. Iwapo katika ngazi husika atakuwa mtia saini katika Kundi ‘A’ badala ya Mratibu.
7.5.6. Katika ngazi za msingi, akaunti za shirika zitafunguliwa na kuendeshwa na kamati ya uongozi katika ngazi husika. Mwenyekiti na Katibu watakuwa watia saini katika Kundi ‘A’ na Mweka Hazina na mjumbe mmoja wa Kamati ya Uongozi watakuwa watia saini katika Kundi ‘B’ Hundi zote za malipo zitawekwa saini na watia saini wawili mmoja mmoja kutoka makundi mawili yaliyoainishwa hapo juu.
7.5.7. Raslimali zote za shirika zinazohamishika au kutohamishika zitamilikiwa na shirika kwa jina lake na kutumiwa tu kwa ajili ya kazi na shughuli za shirika kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na Bodi ya Wakurugenzi.
c) Kutohudhuria mitatu (3) mfululizo ya chombo ambacho yeye ni kiongozi wa shirika hata baada ya kutakiwa kufanya hivyo isipokuwa tu kama atakuwa ameshindwa kuhudhuria kutokana ama na kuruhusiwa na chombo hicho au sababu za kushindwa kuhudhuria kwake kikao hicho zinakubaliwa na chombo hicho chenyewe baada ya kujieleza au kutoa taarifa ya maneno au maandishi.
d) Kutolipa ada ya mwaka na michango mingine kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
e) Kufariki dunia.
f) Kupatwa na ugonjwa wa akili na kutopona katika muda unaozidi miezi sita (6).
g) Kuwa na mwenendo wa kitabia, kijinai na kimaadili ambao unalidhalilisha shirika mbele ya macho jamii.
Kujaza nafasi za uongozi zilizowazi.
6.4.5. Wakati wowote kutakapotokea nafasi ya uongozi kuwa wazi katika chombo chochote cha shirika katika ngazi yeyote; nafasi hiyo itabaki wazi hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika wakati wa mkutano mkuu uliomchagua /kumteua kiongozi husika.
6.4.6. Ibara hii haitahusu uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji ambapo kama nafasi yake itakuwa wazi Bodi ya wakurugenzi itamteua Mfanyakazi Mwandamizi wa shirika au mtu mwingine yeyote ambaye inaona ana sifa, kukaimu hiyo kwa muda usiozidi miezi sita (6).
6.5. Ieleweke wazi kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika itakuwa na mamlaka na wajibu wa kumwajibisha mkurugenzi yeyote ambaye ni mjumbe wa Bodi hiyo na kiongozi mwingine yeyote katika ngazi ya Kata iwapo itabainika kuwa amevunja Katiba, kukiuka maadili au taratibu za shirika.
6.6. Halmashauri itakuwa na mamlaka na wajibu wa kupokea na kujadili rufani juu ya maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya kumwajibisha kiongozi yeyote wa ngazi ya Mkoa na inapolazimu inaweza kuwa chombo cha kusikiliza na kutolea uamuzi wa rufaa wa maamuzi yeyote yaliyochukuliwa na Bodi ya wakurungenzi katika kumwajibisha kiongozi yeyote wa shirika katika ngazi ya mkoa katika kutekeleza jukumu hili Halmashauri inaweza ama kuthibitisha au kutengua au kuiagiza Bodi kulijadili na kulitolea uamuzi tena swala husika.
6.7. Iwapo kiongozi hataridhishwa na uamuzi wa Halmashauri anaweza kukata rufaa katika kikao cha Mkutano Mkuu ngazi ya Mkoa .
6.8. Katika ngazi ya wilaya na mkoa kamati ya uongozi itakuwa na mamlaka na wajibu wa kumwajibisha kiongozi yeyote katika ngazi hiyo na rufani inaweza kukatwa kwenye mkutano mkuu wa ngazi husika. Wakurugenzi au kamati ya uongozi kwa ujumla wake katika ngazi husika.
(g). Kufuatilia na kupitia mlinganyo wa mahesabu ya fedha na mali zingine za shirika kila mara.
(h). Kufanya kazi nyingine yeyote atakayoagizwa na Bodi ya Wakurugenzi. Halmashauri au Mkutano mkuu katika ngazi ya Mkoa au kamati ya uongozi katika ngazi za wilaya.
SIFA ZA WAGOMBEA UONGOZI.
6.2. Viongozi wa kuchaguliwa wa shirika watakuwa na walau na sifa zifuatazo ili waweze kugombea uongozi katika ngazi yeyote ya shirika.
6.2.1. Awe mwanachama hai wa shirika aliyelipa michango yake yote.
6.2.2. Awe amekuwa mwanachama wa shirika kwa muda usioungua miaka
miwili (2).
6.2.3. Awe mzalishaji mdogo au mfanya biashara mdogo ambaye ni mwanachama au anatoka katika kikundi au mtandao mwanachama.
6.3. Mwanachama wa shirika atakayekuwa amewajibishwa kwa mujibu wa Ibara ya 6.4 ya Katiba hii, hataruhusiwa tena kugombea nafasi yeyote ya uongozi katika ngazi yeyote ile ya shirika.
6.4. MUDA , UKOMO WA UONGOZI NA UWAJIBISHWAJI WA VIONGOZI.
6.4.1 Muda wa uongozi utakuwa ni miaka mitatu (3) katika nafasi zote za kuchaguliwa katika ngazi zote za shirika.
6.4.2. Kiongozi anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kimoja zaidi na baada yakutumikia shirika kwa vipindi viwili zaidi na baada ya kutumikia shirika kwa vipindi viwili, hataruhusiwa tena kugombea nafasi hiyo aliyokuwa akiishikilia katika ngazi husika ya shirika. Ieleweke wazi kuwa kiongozi aliyemaliza vipindi viwili katika nafasi ya uongozi katika ngazi yeyote anaweza kugombea nafasi ya ngazi ya juu au ya chini katika shirika iwapo anazo sifa zinazotakiwa.
6.4.3. Kiongozi wa MWAVIWAWATA hataruhusiwa kushika nafasi mbili za uongozi katika ngazi tofauti za shirika. Ieleweke wazi kuwa iwapo kiongozi wa ngazi ya wilaya atachaguliwa kushika madaraka katika ngazi ya mkoa isipokuwa tu katika Halmashauri, atalazimika kujiuzulu mara moja katika ngazi ya wilaya mara tu atakapochaguliwa katika uongozi wa ngazi ya mkoa, ibara hii itatumika katika ngazi za wilaya na za kata.
6.4.4. Kiongozi yeyote wa shirika katika ngazi yeyote atakoma kuwa kiongozi iwapo mojawapo ya matukio yaliyoorodheshwa katika Ibara hii litatokea.
(a). Kujiuzulu au kujitoa uanachama mwenyewe kwa kuandika barua na kuwasilisha kwa katibu wa kikao kilichomchagua kuwa kiongozi.
(b). Kuondolewa uongozi au kufukuzwa uanachama na mkutano mkuu katika ngazi husika kutokana na sababu zifuatazo;-
6.1.3. KATIBU.
Katibu atatekeleza kazi na majukumu yafuatayo katika ngazi husika.
a) Mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za shirika katika ngazi husika
b) Ataandaa sera, mipango mkakati, mpango wa utekelezaji kazi bajeti na maandiko ya miradi katika ngazi husika.
c) Ataandaa taarifa ya fedha na kuziwasilisha katika kikao kinachohusika katika ngazi husika.
d) Kuongoza ama menejimenti katika ngazi ya mkoa au ofisi ya uratibu na ufuatiliaji katika ngazi ya wilaya.
e) Kusimamia uundaji wa bajeti, mapato, matumizi na taarifa za maswala yote ya fedha katika ngazi husika kwa kushirikiana na mtunza hazina.
f) Kufanya mawasiliano yote ya kiofisi ndani na nje ya shirika katika ngazi husika.
g) Ataandaa na kuongoza mchakato wa kuajiri na kuwajibisha wafanyakazi wa shirika chini ya usimamizi wa Bodi ya wakurugenzi na au kamati ya uongozi kulingana na mahitaji halisi ya shirika katika ngazi husika.
h) Kuitisha mikutano na vikao vya vyombo mbalimbali katika ngazi husika, kuweka kumbukumbu ya vikao vyote vya kikatiba ambavyo yeye ni mwandishi na mtunza kumbukumbu wa vikao hivyo.
i) Katika ngazi ya mkoa katibu ataweka na kutunza kumbukumbu za vikao vya mkutano mkuu, Halmashauri na Bodi ya wakurugenzi.
j) Katika ngazi ya wilaya Katibu ataweka na kutunza kumbukumbu za vikao vya mkutano mkuu wa ngazi ya wilaya na kamati ya uongozi.
k) Katika ngazi ya Kata Katibu ataweka na kutunza kumbukumbu za vikao vya mkutano mkuu na kamati ya uongozi katika ngazi husika.
l) Kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili kugharamia shughuli zote za shirika kwa kushirikiana na Mweka Hazina na Bodi ya Wakurugenzi au kamati ya uongozi katika ngazi husika.
m) Kufanya kazi nyingine yeyote atakayoagizwa na Bodi ya Wakurugenzi , Halmashauri au Mkutano mkuu katika ngazi ya Mkoa au Kamati ya uongozi katika ngazi za wilaya.
6.1.4. MWEKA HAZINA.
Mweka Hazina atatekeleza kazi na majukumu yafuatayo katika ngazi husika
a) Msimamizi mkuu wa maswala yote ya fedha , uchumi, uwekezaji na mali ya shirika kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji. Katika ngazi ya Mkoa atawajibika kwa Bodi ya Wakurugenzi.
b) Ata andaa na kubuni mikakati ya kuboresha vyanzo mbalimbali vya mapato ya shirika.
c) Ataratibu matumizi yote ya shirika katika ngazi husika.
d) Atapokea kiingilio na ada ya uanachama ruzuku misaada na mapato mengine yeyote yale halali ya shirika katika ngazi husika.
e) Kuandaa na kutunza taarifa zote za fedha za shirika kwa kuweka sahihi kwa mujibu wa taratibu za utunzaji fedha na au kuhakikisha jukumu hili linatekelezwa kikamilifu na menejimenti.
f) Kuandaa na kuwasilisha taarifa mbalimbali za fedha katika vikao na mikutano ya Bodi ya Wakurugenzi au Kamati ya uongozi na au mkutano Mkuu kwa kushirikiana na Mkurugenzi mtendaji na Bodi ya viongozi wote walau siku tatu (3) kabla ya kikao au mkutano.
g) Kiwango cha mahudhurio yanayowezesha kukutana kwa mkutano au kikao cha kamati ya uongozi ni asilimia hamsini (50%) ya wajumbe walioalikwa walio na haki ya kuhudhuria na kupiga kura kwa mujibu wa katiba hii.
h) Iwapo itahitajika kupiga kura za siri ili kufikia uamuzi wa jambo lolote katika kikao au mkutano kila mjumbe atakuwa na kura moja. Iwapo kura zitafungana kati ya makundi mawili, Mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi.
i) Kamati ya uongozi inaweza kukasimu baadhi ya mamlaka yake kwa Mwenyekiti na au katibu kwa jambo ambalo imeanza kulifanyia kazi lakini haijalitolea maamuzi pale itakapo ona sio busara kusubiri hadi kikao kingine.
6.0. VIONGOZI WA SHIRIKA.
6.1. Shirika litakuwa na viongozi wakuu wafuatao katika kila ngazi :-
- Mwenyekiti
- Makamu Mwenyekiti
- Mweka Hazina
6.1.1. VIONGOZI WA SHIRIKA.
Mwenyekiti atatekeleza kazi na majukumu yafuatayo katika ngazi husika.
a) Atakuwa ni msemaji mkuu wa shirika.
b) Ataongoza mikutano na vikao vyote vya shirika katika ngazi husika
Katika ngazi ya Mkoa Mwenyekiti atafanya yafuatayo:-
c) Atasimamia shughuli zote za shirika katika ngazi husika.
d) Atawasilisha na au kutoa ufafanuzi wa taarifa mbalimbali za shirika mbele ya Bodi ya Wakurugenzi , Halmashauri na au Mkutano mkuu ngazi ya mkoa.
e) Atawajibika kwa bodi ya Wakurugenzi na mkutano mkuu ngazi ya Mkoa.
6.1.2. MAKAMU MWENYEKITI.
Makamu Mwenyekiti atatekeleza kazi na majukumu yafuatayo katika ngazi husika:-
a) Shughuli zote za Mwenyekiti iwapo Mwenyekiti hataweza kutekeleza majukumu yake kutokana na kutokuwepo; nafasi ya uenyekiti kuwa wazi au sababu nyingine yeyote ile.
b) Shughuli yeyote ile atakayoagizwa na Mwenyekiti inayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya Mwenyekiti yaliyoainishwa katika Katiba hii.
c) Kufanya kazi nyingine yoyote atakayoagizwa na Bodi ya Wakurugenzi. Halmashauri au Mkutano Mkuu katika ngazi ya Taifa au Kamati ya uongozi katika ngazi za wilaya.
572. KAMATI YA UONGOZI KATIKA NGAZI YA KATA.
a) Kutakuwa na Kamati ya uongozi katika ngazi ya kata husika itakayokutana kila baada ya miezi mitatu (3) yaani mara nne (4) kwa mwaka au kila itapoonekana inahitajika.
b) Kamati ya uongozi katika ngazi ya Kata husika itafanya shughuli zifuatazo;-
c) Kamati ya uongozi itaundwa na wajumbe wasiopungua watano (5) na wasioizidi tisa (9) watakaochaguliwa na mkutano mkuu katika ngazi ya Kata husika kuondoa utata. Wajumbe wa mkutano mkuu watachagua viongozi wafuatao ili waunde Kamati ya uongozi katika ngazi ya Kata (msingi) husika:-
- Mwenyekiti
- Makamu Mwenyekiti
- Katibu
- Mweka Hazina na
d) Utaratibu wa uchaguzi wa viongozi wa Kamati ya Uongozi katika ngazi ya Kata husika utakuwa kama ulivyoainishwa na Ibara ya 5.53 (m) ya Katiba hii na au kulingana na taratibu, miongozo na kanuni itakayowekwa na ngazi ya Kata husika.
e) Katibu atakuwa ndiye mtendaji katika ngazi ya Kata na hata ajiriwa bali atatekeleza majukumu, kazi na mamlaka yake kwa kujitolea.
f) Kikao au mkutano wa kamati ya uongozi utaitishwa na Katibu kwa taarifa ya maandishi inayoonyesha siku. Mahali na ajenda za kikao itakayotolewa na kusambazwa.
g) Taarifa ya kuitisha kikao cha Mkutano mkuu itatolewa na katibu na kuwasilishwa kwa makatibu wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya Kata husika.
h) Katibu wa MWAVIWAWATA katika ngazi ya Kata husika atasambaza Taarifa ya Mkutano mkuu katika ngazi ya kata katika eneo lake.
i) Kila mjumbe wa mkutano anayehudhuria kikao halali atakuwa na kura moja ya siri. Iwapo kura zitafungana katu ya makundi mawili ; mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi.
j) Mkutano mkuu wa dharura wa shirika katika ngazi ya Kata (msingi) husika utaitishwa wakati wowote kunapotokea jambo la dharura ambalo linahitaji kufanyiwa maamuzi ya haraka na Mkutano katika ngazi ya Kata husika .
k) Katibu kwa azimio la kamati m ya uongozi ataitisha kikao cha mkutano mkuu wa dharula katika ngazi ya Kata husika.
l) Vilevile mkutano mkuu wa dharula katika ngazi ya Kata husika utaitishwa na wanachama wa MWAVIWAWATA theluthi mbili ya wajumbe halali wa mkutano mkuu kwa mujibu wa Katiba hii kutoka walau vikundi au mitandao mitatu katika ngazi ya Kata husika wataafiki kwa kuwasilisha azimio la maandishi lenye majina, anwani na saini zao na lenye kutaja ajenda za mkutano mkuu wa dharura.
m) Kufanya jambo jingine lolote ambalo kwa kawaida hufanywa na mkutano mkuu wa shirika katika ngazi nyingine.
5.6 MUUNDO WA SHIRIKA KATIKA NGAZI YA WILAYA
Kutakuwa na vyombo na vikao vifuatavyo katika kutekeleza mamlaka na shughuli za Shirika katika Ngazi za wilaya:
- Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wilaya husika
- Kamati ya Uongozi
- Kamati ya Uratibu
(b) kwa kuondoa utata ielewekewazi kuwa Bodi ya wakurugenzi wafuatao
- Wajumbe tisa(9) watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu kutoka kila wilaya
Leleweke wazi kuwa wajumbe wa Bodi watakaoteuliwa kwa mujibu wa Ibara 5.5.3(b)ii, hawatakuwa na haki ya kuchaguliwa kushika au kujaza au kukaimu nafasi za uongozi wa kuchaguliwa za Mwenyekiti. Makamu Mwnyekiti na Mweka Hazina.
(c) Bodi ya Wakurugenzi itafanya shughuli zifuatazo:-
- Kupanga na kutekeleza mikakati na shughuli mbali mbali za kutunisha mfuko wa Shirika
Vi Kuajiri na kuwajibika mkurugenzi Mtendaji na watumishi wengine wa Shirika na kuingia mikataba ya ajira hizo kulingana na mahitaji halisi ya Shirika
Vii Kuandaa taarifa mbali mbali za kuwasilishwa mbele ya Mkutano
Viii Kuandaa Mkutano Mkuu wa Shirika .
Ix Kupendekeza kwenye Mkutano Mkuu uteuzi wa Mkaguzi wa Mahesabu ya fedha za Shirika kila mwaka.
X Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote anayetuhumiwa kukiuka Katiba na maadili ya Shirika na baada ya kupitia kwa kina tuhuma hizo na kumpa mtuhumiwa haki ya kusikilizwa kuwasilisha mapendekezo mbele ya mkutano Mkuu ama umfukuze uongozi au imrejeshee uongozi mtuhumiwa.
Xi Kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote anayetuhumiwa kukiuka Katiba na maadili ya Shirika na baada ya kupitia kwa kina tuhuma hizo na kumpa mtuhumiwa haki ya kusikilizwa kuwasilisha mapendekezo mbele ya Mkutano Mkuu katika Ngazi husika ya Shirika ama umfukuze uanachama au imrejeshee uanachama mtuhumiwa.
Xii Kufanya jambo jingine lolote ambalo kwa kawaida hufanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika na au kufanya jambo jingine lolote kama itakavyoagizwa na Mkutano Mkuu au Halmashauri ya Shirika.
(d) Kikao au Mkutano wa Bodi ya wakurugenzi utaitishwa na Mkurugenzi Mtendaji baada ya kushauriana na Mwenyekiti kwa taarifa ya maandishi inayooyesha siku. Mahali na ajenda za kikao itakayotolewa na kusambazwa kwa Wakurugenzi wote walau siku tatu(3) kabla ya Kikao au mkutano.
(e) Uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi utafanyika katika Mkutano Mkuu kila baada ya miaka mitatu(3)
(f) Uchaguzi utafanyika kwa mtindo wa kura ya siri na ni mwanachama Yule tu ambaye atakuwa amelipa ada na michango mingine yote walau siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa uchaguzi ndiye atakayekuwa na haki ya kupiga au kupigiwa kura.
(g) Utawala wa uchaguzi wa viongozi wa kuchaguliwa wa Bodi ya Wakurugenzi utakuwa kama ifuatavyo:-
I Uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi utafanyika katika awamu tatu(3)
Ii Awamu ya kwanza itahusika kupata wagombea kumi na nane(18) ambao watakuwa wamepata kura nyingi zaidi ya wagombea wenzao wakiwa ni washindi wawili tu kutoka kila kanda leleweke wazi kuwa wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi kila kanda itakaa peke yake na kupiga kura za kuchagua wagombea washindi wawili kwa utaratibu wa kura ya siri.
Iii Katika awamu ya pili ya uchaguzi wajumbe wote wa Mkutano Mkuu watakusanyika pamoja na kuchagua wagombea washindi tisa(9) kutoka miongoni mwa kundi la wagombea washindi kumi na nane(18) kwa kuzingatia kuwa kila wilaya ipate kiti kimoja cha uwakilishi katika Bodi ya Wakurugenzi.
Iv Katika awamu ya tatu ya uchaguzi wa viongozi , wajumbe wateule wa Bodi ya Wakurugenzi wa kuchaguliwa kuwasilisha kila wilaya watakutana na kufanya Kikao cha kwanza cha Bodi ya Wakurugenzi siku hiyo hiyo ambacho miongoni mwa ajenda yake itakuwa ni kuchagua miongoni mwa ajenda yake itakuwa ni kuchagua miongoni mwao Mwenyekiti makamu Mwenyekiti na Mweka Hazina.
V lli kuondoa utata ieleweke wazi kuwa Kikao cha Kwanza cha Bodi ya Wakurugenzi kitafanyika siku hiyo hiyo ya uchaguzi na matokeo ya washindi wa uongozi katika nafasi ya Mwenyekiti makamu Mwenyekiti yatatangazwa siku hiyo hiyo kwenye Mkutano Mkuu.
Vi Iwapo kura za kuchagua viongozi katika nafasi yeyote zitafungana kura zitarudiwa hadi mshindi apatikane kwa wingi wa kura.
Vii Kigezo pekee cha kutangazwa mshindi katika nafasi yeyote ya kuchaguliwa katika uongozi wa Shirika itakuwa ni kupata kura nyingi zaidi ya mgombea au wagombea wengine.
(h) Wajumbe wa kuteuliwa wa Bodi ya Wakurugenzi watateuliwa na Mkutano Mkuu mara tu baada ya uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kuchaguliwa kupatikana. Bodi ya Wakurugenzi itachagua na kuwasilisha mapendekezo yenye majina sita ya wanachama wenye sifa kwa Halmashauri ambayo itayachuja majina hayo na kuwasilisha majina yasiyozidi matatu(3) kwa ajili ya uteuzi mbele ya Mkutano mkuu.
(i) Katibu wa vikao na mikutano ya Bodi ya Wakurugenzi atakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji
(i) Kiwango cha mahudhurio yanayowezesha kukutana kwa mkutano au kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ni asilimia hamsini (50%) ya wajumbe walioalikwa walio na haki ya kuhudhuria na kupiga kura kwa mujibu wa Katiba hii kwa vyovyote vile idadi ya wajumbe wa Mkutano au Kikao cha Bodi ya wakurugenzi isipungue wajumbe saba(7) kila kikao.
(k) Iwapo itahitajika kupiga kura za siri ili kufikia uamuzi wa jambo lolote katika kikao au Mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi kila mjumbe atakuwa na kura moja iwapo kura zitafungana kati ya makundi mawili Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi atakuwa na kura ya uamuzi.
(i) Bodi ya Wakurugenzi inaweza kukasimu baadhi ya mamlaka yake kwa Mwnyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi au Mkurugenzi Mtendaji kwa jambo ambalo imeanza kulifanyia kazi lakini haijalitolea maamuzi pale itakapoona sio busara kusubiri hadi kikao kingine cha Bodi ya Wakurugenzi.
(m) Utaratibu wa uchaguzi ulioainishwa katika Ibara hii utatumika katika chaguzi zote za Shirika kutoka Ngazi ya kata hadi Ngazi ya mkoa isipokuwa tu pale ambapo itakuwa imeelekezwa vinginevyo na Mkutano Mkuu kwa kupitisha Azimio Maalum kuhusu uendeshaji wa uchaguzi wa Ngazi yeyote ile ya Shirika.
(ii) Bodi ya Wakurugenzi itawajibika kwa mkutano mkuu wa mwaviwawata Ngazi ya mkoa kwa ujumla wake.
5.5.3
BODI YA WAKURUGENZI
Kutakuwa na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika itakayoundwa na wajumbe wasiopungua tisa (9) wasiozidi kumi na mbili (12) ambao watachaguliwa na kuteuliwa na mkutano mkuu kwa kuzingatia yafuatayo.
i Uwakilisshi wa wajumbe tisa (9) wa kuchaguliwa kutoka wilaya utakaohakikisha kuwa kila wilaya ya Mwaviwawata kama zilivyoainishwa katika Nyongeza ya 1 ya katiba hii, zimeundwa kwa madhumuni ya uchaguzi tu ili kupata uwakilishi katika Bodi ya Wakurugenzi katika Ngazi ya kutoka kila wilaya
ii Uwakilishi wa wanachama wasiozidi watatu (3) watakaoteuliwa na
mkutano mkuu kutokana na hadhi, ujuzi, busara
5.5.4 MENEJIMENTI
(a) Kutakuwa na menejimenti ya Shirika itakayoundwa na:-
I Mkurugenzi Mtendaji ambaye ataongoza shughuli zote za utendaji wa kila siku.
Ii Watendaji waandamizi wa Shirika watakaoajiriwa kwa mujibu katiba hii
Iii Wafanyakazi wengine wa Shirika watakaoajiriwa kwa masharti mbali mbali ya ajira kadiri itakavyoamua kulingana na mahitaji halisi ya Shirika.
(b) Menejimenti itafanya shughuli zifuatazo ;-
I Kuandaa na kutekeleza shuguli za kila siku za Shirika
Ii Kubuni kuandaa kuitekeleza na kuitathmini mipango mbali mbali ya maendeleo ya Shirika kulingana na malengo na madhumuni ya Shirika kama yalivyohainishwa katika Katiba hii.
Iii Kufuatilia kukagua na kutathmini utekelezaji wa shughuli mipango na miradi yote ya Shirika mkoa.
Iv Kuandaa vikao na mikutano yote ya Shirika katika Ngazi ya Mkoa kwa maagizo na Bodi ya Wakurugenzi.
V Kuandaa kalenda ya Mikutano Mikuu ya Shirika katika Ngazi mbali mbali na vikao vingine kila mwaka kwa maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi kwa kushauriana na Ngazi husika
Vi Kutoka huduma mbali mbali za kitaalamu na za kiutawala kwa Ngazi zote za Shirika kadri itakavyohitajika katika kupanga na kutekeleza shughuli za Shirika.
Vii Kuandaa vikao vya Menejimenti na vya wafanyakazi wote.
Viii Kufanya shughuli yeyote itakayoagizwa na Bodi ya Wkurugenzi
(c) Menejimenti itakutana walau mara moja kila mwezi
(d) Kikao au Mkutano wa Menejimenti utaitishwa na Katibu baada ya kushauriana na Mkurugenzi Mtendaji kwa taarifa ya maandishi inayoonyesha siku mahali na ajenda za kikao itakayotolewa na kusambazwa kwa wajumbe wote wa Menejimenti walau siku moja(1) kabla ya Kikao au Mkutano.
(e) Nafasi ya Katibu wa Menejimenti itakuwa kwa mzunguko kila mwaka ambapo Katibu atachaguliwa katika kila kikao au mkutano wa kwanza wa kila mwaka.
(f) Mzunguko wa uchaguzi wa Katibu wa Menejimenti utazingatia mfuatano wa uandamizi katika utumishi wa Shirika na au uwakilishi wa kila Idara na pia muda wa utumishi uliopo wa mfanyakazi husika kwa mujibu wa mkataba wake wa ajira.
(g) Katibu wa Menejimenti atafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja hadi pale Katibu mwingine atakapochaguliwa.
(h) Kiwango cha mahudhurio yanayowezesha kukutana kwa mkutano au kikao cha Menejimenti ni asilimia hamsini (50%) ya wajumbe walioalikwa walio na haki ya kuhudhuria kwa mujibu wa Katiba hii.
(i) Iwapo itahitajika kura za siri ili kufikia uamuzi wa jambo lolote katika kikao au Mkutano wa menejimenti kila mjumbe atakuwa na kura moja Iwapo kura zitafungana kati ya makundi mawili, Mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi.
(ii) Menejimenti inaweza kukasimu baadhi ya mamlaka yake kwa Mkurugenzi mtendaji au katibu kwa jambo ambalo imeanza kulifanyia kazi lakini haijalitolea maamuzi pale itapoona sio busara kusubiri hadi kikao kingine cha Menejimenti.
(k) Katibu ataweka kumbu kumbu zote za vikao vya Menejimenti.
(i) Iwapo Mkurugenzi mtendaji au Katibu atakuwa hayupo menejimenti itamchagua mfanyakazi yeyote mwaandamizi miongoni mwao kuikaimu nafasi hiyo kwa ajili ya uendeshaji wa kikao hicho tu.
(ii) Kutakuwa na vikao au mikutano ya wafanyakazi wote ambayo itahudhuriwa na wafanyakazi wote wa Shirika itakayokutana walau mara moja kila mwishoni mwa miezi miwili.
(iii) Mkutano wa wafanyakazi wote utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kama Mwenyekiti na Katibu wake atakuwa Katibu wa Menejimenti. Iwapo Mwnyekiti na Katibu hawapo wafanyakazi watateuwa miongoni mwao Mwenyekiti na Katibu wa muda kwa ajili ya kuendesha kikao hicho tu.
(iv) Mkutano wa wafanyakazi utajadili na kushauri juu ya mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Shirika mazingira ya kufanyia kazi na maslahi ya wafanyakazi au jambo jingine lolote linalohusu maslahi ya wafanyakazi au ya Shirika.
(v) Kikao au Mkutano wa Wafanyakazi wote utaitishwa na Katibu baada ya kushauriana na Mkurugenzi Mtendaji kwa taarifa ya maandishi inayoonyesha siku mahali na ajenda za kikao itakayotolewa na kusambazwa kwa wafanyakazi wote wa Shirika walau siku saba(7) kabla ya Kikao au Mkutano.
(vi) Kiwango cha mahudhurio yanayoweza kukutana na kufanyika kwa mkutano au kikao cha wafanyakazi ni asilimia hamsini (50%) ya wafanyakazi wote.
(vii) Menejimenti kwa ujumla wake itafanya kazi na kuwajibika kwa Bodi ya Wakurugenzi.
OFISI YA URATIBU KATIKA NGAZI YA WILAYA
Kutakuwa na Ofisi ya uratibu katika ngazi ya wilaya ya shirika itakayoundwa na :-
I Mratibu ambaye ataongoza shughuli zote za Ofisi ya uratibu kiutendaji
II Watumishi wengine wa shirika watakaoajiliwa kwa masharti mbalimbali ya ajira kadiri itakavyoamuliwa kulingana na mahitaji halisi ya shirika katika ngazi ya wilaya husika.
Ofisi ya uratibu itafanya shughuli zifuatazo:-
I Kuandaa na kutekeleza shughuli za kila siku za shirika
II Kubuni ,kuandaa ,kuitekeeza na kuithamin mipango mbalimbali ya maendeleo ya shirika
Kulingana na malengo na madhumuni ya shirika katika ngazi ya wiaya husika kama yalivyoanishwa katika katiba hii.
III Kufuatilia , kukagua na kutathmini utekelezaji wa shughuli ,mipanngo na miradi yote ya shirika katika ngazi ya wilaya
IV Kuandaa vikao na mikutano yote ya shirika katika ngazi ya wilaya husika
V Kutoa huduma mbalimbali za kitaalamu na za kiutawala kwa ngazi zote za shirika kadri itakavyohitajika katika kupanga na kutekeleleza shughuli za shirika kadri itakavyohitajika katika kupanga na kutekeleza shughuli za shirika
VI Kuandaa vikao vya wafanyakazi wote katika ngazi ya wilaya pale itakapoonekana kuna wafanyakazi zaidi ya watatu (3)
VII Kufanya shughuli yoyote itakayoagizwa na kamati ya uongozi ya ngazi ya wilaya husika na au menejimenti ya shirika katika ngazi ya mkoa.
Ofisi ya uratibu itakutana walau mara moja kila mwezi
Kikao au mkutano wa Ofisi ya uratibu utaitishwa na katibu baada ya kushauriana na mratibu kwa taarifa ya maandishi inayoonyesha siku , mahali na ajenda za kikao itakayotoewa na kusambazwa kwa wajumbe wote wa menejimenti walau siku moja (1) kabla ya kikao au mkutano
Katibu atachaguliwa katika kila kikao au mkutano wa kwanza wa kila mwaka
Mzunguko wa uchaguzi wa katibu wa menejimenti utazingatia mfuatano wa uandamizi katika utumishi wa shirika na au uwakilishi wa kila idara katika ngazi ya wilaya husika
Katibu wa menejimenti atafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja hadi pale katibu mwingine atakapochaguliwa
Kiwango cha mahudhurio yanayowezesha kukutana kwa mkutano au kikao cha Ofisi ya uratibu ni asilimia hamsini (50%) ya wafanyakazi wote katika ngazi ya wilaya husika
Iwapo itahitajika kupiga kura za siri ili kufikia uamuzi wa jambo lolote katika kikao kila mjumbe atakuwa na kura moja iwapo kura zitafungana kati ya makundi mawili mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi
KAMATI YA UONGOZI KATIKA NGAZI YA WIAYA
Kutakuwa na kamati ya uongzi katika ngazi ya wilaya husika itakayokutana kila baada ya miezi mitatu (3) yaani ara nne (4) kwa mwaka au kila itapoonekana inahitajika
Kamati ya uongozi katika ngazi ya wilaya ya husika itafanya shughuli zifuatazo :-
- Kupanga na kusimamia bajeti na mpango kaz wa shirika katika ngazi ya wilaya
- Kupanga na kutekeleza mikakati na shughuli mbalimbali za kutunisha mfuko wa shrike katika ngazi ya wilaya husika
- Kufungua na kuendesha akaunti za shirika katika mabenki na aasisi mbalimbali za fedha katika ngazi ya wilaya husika
- Kuajiri na kuwajibisha mratibu na watumishi wengine wa shirika na kuingia mikataba ya ajira hizo kulingana na mahitaji halisi ya shirika kwa kushauriana na kushirikiana na mkurugenz tendaji
- Kuandaa taarifa mbalimbali za kuwasilishwa mbele ya mkutano mkuu katika ngazi ya wilaya huska au katika ngazi ya mkoa
- Kuandaa mkutano mkuu wa shirika katika ngazi ya wilaya husika
viii. Kufanya jambo jingine lolote ambalo kwa kawaida hufanya na kamati ya uongozi na au kufanya jambo jingine lolote kama utakavyoagizwa na mkutano mkuu au halmashauri ya shirika au bodi ya wakurugenzi katika ngazi ya mkoa
(c) Kamati ya uongozi itaundwa na wajumbe wasiopungua saba (7) na wasiozidi tisa (9) watakaochaguliwa na mkutano mkuu katika ngazi ya wilaya husika kuondoa utata wajumbe wa mkytano mkuu watachagua viongozi wafuatao ili waunde kamati yta uongozi katika ngazi ya wiaya husika
I Mwenyekiti
II Makamu mwenyekiti
III Mweka hazina na
IV Wajumbe wasiozidi watano (5) watakaoteuliwa na mkutano mkuu katika ngazi husika
V Katibu atakuwa ni mratibu ambaye kwa nafasi yake pia atakuwa mtendaji mkuu katika ngazi ya wilaya husika mratibu ataajiliwa na Kuwajibika na kamati ya uongozi wa ngazi ya wilaya husika
(d) Utaratibu wa uchaguzi wa viongozi wa kamati ya viongozi wa kamati ya uongozi katika ngazi ya wilaya husika atakuwa kama uivyoainishwa na ibara ya 5.5.3 (m)ya katiba hii
(e) Uchaguzi utazingatia uwakilishi wa ngazi ya wilaya au ngazi za msingi yaani kata
(f) Kikao au mkutano wa kamati ya uongozi utaitishwa na mratibu baada ya kushauriana na mwenyekiti kwa taarifa ya maandishi inayonyesha siku mahali na ajenda za kikao itakayotolewa na kusambazwa kwa wakurugenzi wote walau siku tatu (3) kabla ya kikao au mkutano
(g) Kiwango cha mahudhurio yanayoweza kukutana na kufanya kazi kwa mkutano au kikao cha kamati ya uongozi ni asilimia hamsini (50%) ya wajumbe walioalikwa walio na haki ya kuhudhuria kwa mujibu wa katiba hii kwa vyovyote vile ,idadi ya waumbe isipungue wajumbe watano (5) kila kikao
(h) Iwapo itahitajika kupiga kura za siri ili kufikia uamuzi wa jambo lolote katika kikao au mkutano wa kamati ya uongozi kila mjumbe atakuwa na kura moja iwapo kura zitafungana kati ya makundi mawili mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi
(i) Kaati ya uongozi inaweza kukasimu baadhi ya mamaka yake kwa mwenyekiti na au mratibu kwa jambo ambalo imeanza kulifanyia lakini haijaitolea maamuzi pale itakapoona sio busara kusubiri hadi kikao kingine
(j) Kamati ya uongozi katika ngazi ya kati itafanya kazi na Kuwajibika na mkutano mkuu wa ngazi ya kata husika.
(d) kikao au mkutano wa Halmashauri utaitishwa na Mkurugenzi Mtendaji kwa taarifa ya maandishi inayoonyesha siku ,mahali na ajenda za kikao itakayotolewa na kusambazwa katika ngazi zote za kati walau siku saba (7) kabla ya kikao au mkutano
(e) Nafasi ya uenyekiti wa halmashauri itakuwa kwa mzunguko kwa kila ngazi ya wlaya na Mwenyekiti wa kila kikao au mkutano atachaguliwa katika kila kikao au mkutano wa halmashauri.
(f) Mzunguko wa uchaguzi wa uenyekiti wa Halmashauri utazingatia mfuatano wa kiwilaya kama ulivyoainishwa katika Nyongeza ya katiba hii
(g) Katibu wa vikao na mikutano ya Halmashauri atakuwa ni mkurgenzi mtendaji.
(h) Kiwanngo cha mahudhurio yanayowezesha kukutana kwa mkutano mkutano au kiko cha halmashauri ni asilimia hamsini (50%) ya wajumbe waloalikwa walio na haki ya kuhudhuria na kupiga kura halali kwa mujibu wa katiba hiikwa vyovyote vile, idadi ya wajumbe wa mkutano au kikao cha Halmashauri isipungue wajumbe thelathini (30)kila kikao
(i) Iwapo itahitajika kupiga kura za siri ili kufika uamuzi wa jambo lolote katika kikao au mkutano wa Halmashauri kila mjumbe atakuwanakura moja .Iwapo kura zitafungana kati ya makundi mawili ,Mwenyekiti wa Halmashauri atakuwa na kura ya uamuzi.
(j) Halmashauri inaweza kukasimu baadhi ya Mamlaka yake kwa bodi ya wakurugenzi kwa jambo ambalo imeanza kulifanyia kazi lakini haijalitolea maamuzi pale itakapoona sio busara kusubiri hadi kikao kingine cha Halmashauri
MKUTANO MKUU WA WILAYA.
(a) Kutakuwa na mkutano mkuu wa wilaya husika utakaofanyika mara moja kwa mwaka
(b) Mkutano mkuu utakuwa ndicho chombo cha juu zaidi na cha mwisho katika kufanya maamuzi ya juuya maswala mbalimbali ya shirika katika ngazi ya wilaya
(c) Mkutano mkuu wa ngazi ya wilaya utafanya shughuli zifuatazo:-
Kupokea , kujadili ,kukubali au kukataa taarifa ya maendeleo na utekelezaji wa shughuli za shirika katika ngazi ya wilaya husika kila mwaka
- Kupitisha mpango kazi na bajetikwa mwaka unaofuata katika ngazi ya wilaya
- Kupokea taarifa ya mkaguzi wa hesabu za shirika katika ngazi ya wilaya
- Kufanya uchaguzi wa wajumbe kutoka katika ngazi ya wilayawatakaokuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaviwawata
katika ngazi ya Mkoa
- Kuwajibisha wajumbe wa kamati ya uongozi katika ngazi ya wilaya
- Kupitisha marekebisho au mabadiliko ya katiba katika ngazi ya wiaya iwapo itakuwa imesajiliwa
- Kupokea na kuthibitisha wanachama wapya katika ngazi ya wilaya
- Kuwajibisha wanachama waokiuka malengo ,madhumuni ,katiba na maadili ya shirika katika ngazi ya wilaya
- Kutoa maelezo juu ya mipango ,mikakati na utekelezaji wa Mamlaka na shughuli za shirika katika ngazi ya wilaya
- Kufanya uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya uongozi
- Kufanya jambo jingine lolote ambalo kwa kawaida hufanywa na mkutano mkuu wa Shirika katika ngazi ya wilaya
(d) Mkutano mkuu utahudhuriwa na wajumbe wafuatao:-
- Wajumbe wote wa kamati ya uongozi atika ngazi ya wilaya husika
- Wawakilishi wa wa ngazi za kata kwa ngazi ya wiaya uwakilishi utakuwa kwa uwiano uliosawa utakaoamuliwa na kamati ya uongozi baada ya kujadiliana na kuafikiana na Ngazi husika.
iii. Wanachama washiriki wote katika ngazi ya wilaya husika
iv. Wajumbe mmoja mmoja kutoka wanachama mashirika vyama au mitandao midogo ya Vijana katika ngazi ya kata na wilaya husika
v. Wanachama ,wafanyakazi au waalikwa wengine wowote watakaoamuliwa na kamati ya ungozi kwa kushauriana na kuafikiana na ngazi husika.
MKUTANO WA DHARULA / MIKUTANO MINGINE.
Mkurugenzi mtendaji wajumbe waalikwa wa kutano mkuu hawatakuwa na haki ya kupiga kura au kuchangia mchakato wa majadiliano na ufanyaji maamuzi ya mkutano mkuu wa shirika katika ngazi ya wilaya husika
(e) Kiwango cha mahudhurio ya mkutano mkuu yanayowezesha kukutana ni asilimia hamsini (50%) ya wajumbe walioalikwa walio na haki ya kuhudhuria na kupiga kura halali katika mkutano mkuu katika ngazi ya wilaya husika kwa mujibu wa katiba ya ngazi ya kutohusika iwapo imesajiliwa kwa vyovyote vile idadi ya wajumbe wa mkutano mkuu isipungue wajumbe thelathini (30) kila kikao
Mkutano mkuu katika ngazi ya kati husika unaweza kukasimu baadhi ya mamlaka yake kwa kamati ya uongozi kwa jambo ambalo umeanza kulifanyia kazi lakini haujalitolea maamuzi pale utakapoona si busara kusubiri hadi kikao kingine cha mkutano mkuu katika ngazi ya wilaya husika
(g) Taarifa ya maandishi ya kuitisha mkutano mkuu itatolewa walau siku kumi na nne (14) kabla ya kikao cha mkutano mkuu kufanyika katika ngazi ya wilaya husika
(h) Taarifa ya wito wa kuhudhuria kikao cha mkutano mkuu itaoonyesha Tarehe, muda na mahali ambapo mkutano mkuu utafanyika katika ngazi ya wilaya husika
(i) Taarifa ya kuitisha kikao cha mkutano mkuu itatoewa na mratbu baada ya kushauriana na mwenyekiti na kuwasilishwa kwa makatibu wa mwaviwata katika ngazi ya wilaya husika
(j) Katibu wa mwaviwawata katika ngazi ya wilaya husika atasambaza taarifa ya mkutano kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu katika ngazi za wilaya na ngazi za msingi yaani kata katika eneo lake
(k) Kila mjumbe wa mkutano mkuu anayehudhuria kikao halali atakuwa na kura moja ya siri .Iwapo kura zita fungana kati ya makundi mawili mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi
(l) Mkutano mkuu wa dharura wa shirika utaitishwa wakati wowote kunapotokea jambo la dharura ambalo linahitaji kufanyiwa maamuzi ya haraka na mkutano mkuu katika ngazi ya wiaya husika
(m) Mratibu kwa azimio la kamati ya uongozi ataitisha kikao cha mkutano mkuu wa dharura katika ngazi ya wilaya husika
(n) Mratibu kwa azimio la kamati ya uongozi ataitisha kikao cha mkutano mkuu wa dharura katika ngazi ya wilaya husika
(o) Mkutano mkuu wa dharura katika ngazi husika utaitishwa na wanachama iwapo theluthi mbili ya wajumbe halali wa mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba hii kutoka walau wilaya tatu katika ngazi ya mkoa au ngazi tatu (3) za msingi katika ngazi ya wilaya wataafiki kwa kuwasilisha azimio la maandishi lenye majina ,anwani na saini zao na lenye kutaja ajenda za kikao cha mkutano mkuu wa dharura litakapowasilishwa kwa mratibu kwa lengo la kumtaka aitishe kikao cha mkutano mkuu wa dharura mara moja
(p) Taarifa ya wito wa kuhudhuria mkutano mkuu wa dharura itatolewa si chini ya siku tatu (3) kabla ya kikao cha mkutano mkuu wa dharura kufanyika katika ngazi ya wilaya husika
(q) Mkutano mkuu wa dharura utakapoitishwa na idadi ya wajumbe kutimia utafanya shughuli zake kama mkutano mkuu wa kawaida katika ngazi ya kati husika na kutoa maamuzi ,maagizo au maelekezo baada ya kujadili ajenda zilizowasilishwa katika azimio a kuitisha mkutano huo
(r) Ieleweke wazi kuwa mkutano mkuu wa dharura hautakuwa na Mamlaka ya kujadili na kutolea maamuzi,maagizo au maelekezo ajenda yoyote au jambo jingine lolote mbali ya ajenda iiyoainishwa katika wito kuitishwa kwa mkutano mkuu huo wa dharura katika ngazi ya kati husika

Tazama mashirika ambayo yapo karibu